Kwa nini kuupinga Mkataba wa Bandari inaitwa "udini" lakini kuunga mkono sio udini?

KWA NINI KUUPINGA MKATABA WA BANDARI INAITWA "UDINI" LAKINI KUUNGA MKONO SIO UDINI? MSIWE WAPUMBAVU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Wanasiasa moja ya mambo yanayowashushia heshima ni kigeugeu na unafiki wao.
Wanasiasa wakisifiwa na viongozi wa dini hawasemi dini imeingizwa kwenye Siasa lakini wakikosolewe hapo utasikia Dini imeingizwa kwenye Siasa.

Wanasiasa wakitaka kuombewa na viongozi wa dini hiyo hawaiti dini imeingizwa kwenye Siasa. Wao wanataka tuu Sifa na utukufu Kutoka Kwa dini lakini wakikosolewa na kupondwa hapo wanaleta shida.

Tabia hiyo ya hovyo na kinafiki imekomaa Sana katika Nchi yetu. Na sasa tupo kwenye sakata la mkataba WA Bandari.

Viongozi wa dini waliosifia mkataba huu wao hawaambiwi kuwa ni UDINI. Lakini wanaoukosoa wanaambiwa ni udini. Hivi tutaacha lini huo upumbavu.

Kwa nini tusiangalie hoja ya msingi. Huo mkataba kama ni mbovu Kwa nini usibadilishwe? Kama kweli nia ni yakweli ya kutetea maslahi ya nchi. Kwa nini huo mkataba usiboreshwe vifungu vyenye utata?

Kujitetea kwa kujificha kwenye kichaka cha udini hakutabadili Jambo lolote.

Hekima na busara zitumike, kama kweli lengo ni kulinda maslahi ya Taifa letu na maslahi ya Watu wetu na rasilimali zetu.
Mtu akipinga Jambo kama anahoja ya msingi lazima asikilizwe.

kwanza hizo dini zenyewe tumeletewa.
pili, tupo watanzania wengi ambao hatuamini Kati hizo dini zenu za kigeni. Ingawaje tunawatambua na kuheshimu wanaoziamini.
Sasa msitake kuzifanya hizo dini zenu zinaumuhimu kuliko taifa letu.

Mnapojadiliana ishu za taifa msijifanye mnajificha kwenye udini. Oooh! Yule Mkristo ndio maana anakosoa. Lakini akisifia huwezi sikia Jambo Hilo.
Angalieni kinachokosolewa, je kina uhalali wa kukosolewa? Kama jibu ni ndio,basi fanyieni maboresho.

Uwe Mkristo au muislam, uwe wakabila gani, uwe Mtibeli kama Mimi au mpagani. Kwetu haina maana yoyote Ile. Tunachotaka ni kulinda maslahi ya nchi yetu na sio genge Fulani la Watu. Ni lazima tuangalie kizazi chetu kilichopo na kinachokuja.
Dini yako, au Cheo chako au mamlaka yako haina maana yoyote kwetu ikiwa unataka kuliingiza taifa katika hasara na ubinafsi wa hovyo.

Acheni upumbavu! Mtu akitoa hoja isikilizwe hoja yake na sio ni wadini gani.

Kama mkataba haufai, urekebishwe. Hiyo ndio hoja. Mambo ya sijui Amani, sijui mgawanyiko, hayo yote yataletwa na watu wabinafsi na wasiotaka kusikiliza wengine.
Mgawanyiko ni muhimu ikiwa tunatofautiana. Hiyo iwekwe wazi. Kama Watu hawataki wawe wamoja, kujaribu kuwaunganisha Watu wasiofanana ndio ukosefu wa Amani, mitafaruku, unyanyasaji na ukatili. Hatuwezi lazimisha umoja wa kinyonyaji, umoja wa wengine wanafaidi wengine wanasota, huo umoja haupogo labda kinafiki.

Nisikilizeni, umoja unaletwa Kwa kuangalia wengi wanasema nini, lakini pia Kwa kuzingatia maslahi ya taifa na kizazi kijacho.

Upendo, Haki, Ukweli na Akili hiyo ndio namna ya kuwaweka Watu pamoja. Utibeli.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Aristotle believed man was a "political animal" because he is a social creature with the power of speech and moral reasoning: Hence it is evident that the state is a creation of nature, and that man is by nature a political animal. Hata uende wapi siasa ni kila kitu.
 
Ndio haya mambo yaishe sasa viongozi wa dini wabakie kwenye field zao ni hatari wao kuongia kwenye siasa na nyakati zinaonyesha hivyo kwa sasa tunahitaji serikali imara leo kesho na keshokutwa sisi na viongozi wa dini na waumini na waamini yetu ni kwenye sanduku la kura na kutoa maoni yetu tu ila sio kuiendesha serikali kwa rimoti na kupush agenda zenye maslahi na taasisi zetu.

Kwa hiyo viongozi wa kisiasa wakipuyanga unataka viongozi wa dini wakae kimya?
 
Mkuu nadhani na kanisa kuna kitu wanapigania🤔
Tuendelee kula mtori nyama zipo chini
if that is true tuseme kuna conflict of interests between third parties? Au kule kiotani hawakujua huu waraka utatoka? Ila twende mbele turudi nyuma., tec huwa hawakurupuki kutoka na nyaraka . Anyway acha tule shingo .Vipapatio tutavikuta chini.
 
Aristotle believed man was a "political animal" because he is a social creature with the power of speech and moral reasoning: Hence it is evident that the state is a creation of nature, and that man is by nature a political animal. Hata uende wapi siasa ni kila kitu.

Siasa chanzo chake ni Dini.
 
Kuwa ccm ni laana tosha yaani hadi viongozi wao ni wa hovyo na hawatumii akili, yaani watu wengi tu wametoka mbele kuunga mkono hii hoja hawajaitwa wadini ili ukipinga tu ni udini, kingine cha kushangaza kiongozi anakwenda kufungua kanisa anasema tusichanganye dini na siasa wakati anaongelea mambo ya siasa akiwa kanisani akili zao ni za ajabu sana
 
KWA NINI KUUPINGA MKATABA WA BANDARI INAITWA "UDINI" LAKINI KUUNGA MKONO SIO UDINI? MSIWE WAPUMBAVU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Wanasiasa moja ya mambo yanayowashushia heshima ni kigeugeu na unafiki wao.
Wanasiasa wakisifiwa na viongozi wa dini hawasemi dini imeingizwa kwenye Siasa lakini wakikosolewe hapo utasikia Dini imeingizwa kwenye Siasa.

Wanasiasa wakitaka kuombewa na viongozi wa dini hiyo hawaiti dini imeingizwa kwenye Siasa. Wao wanataka tuu Sifa na utukufu Kutoka Kwa dini lakini wakikosolewa na kupondwa hapo wanaleta shida.

Tabia hiyo ya hovyo na kinafiki imekomaa Sana katika Nchi yetu. Na sasa tupo kwenye sakata la mkataba WA Bandari.

Viongozi wa dini waliosifia mkataba huu wao hawaambiwi kuwa ni UDINI. Lakini wanaoukosoa wanaambiwa ni udini. Hivi tutaacha lini huo upumbavu.

Kwa nini tusiangalie hoja ya msingi. Huo mkataba kama ni mbovu Kwa nini usibadilishwe? Kama kweli nia ni yakweli ya kutetea maslahi ya nchi. Kwa nini huo mkataba usiboreshwe vifungu vyenye utata?

Kujitetea kwa kujificha kwenye kichaka cha udini hakutabadili Jambo lolote.

Hekima na busara zitumike, kama kweli lengo ni kulinda maslahi ya Taifa letu na maslahi ya Watu wetu na rasilimali zetu.
Mtu akipinga Jambo kama anahoja ya msingi lazima asikilizwe.

kwanza hizo dini zenyewe tumeletewa.
pili, tupo watanzania wengi ambao hatuamini Kati hizo dini zenu za kigeni. Ingawaje tunawatambua na kuheshimu wanaoziamini.
Sasa msitake kuzifanya hizo dini zenu zinaumuhimu kuliko taifa letu.

Mnapojadiliana ishu za taifa msijifanye mnajificha kwenye udini. Oooh! Yule Mkristo ndio maana anakosoa. Lakini akisifia huwezi sikia Jambo Hilo.
Angalieni kinachokosolewa, je kina uhalali wa kukosolewa? Kama jibu ni ndio,basi fanyieni maboresho.

Uwe Mkristo au muislam, uwe wakabila gani, uwe Mtibeli kama Mimi au mpagani. Kwetu haina maana yoyote Ile. Tunachotaka ni kulinda maslahi ya nchi yetu na sio genge Fulani la Watu. Ni lazima tuangalie kizazi chetu kilichopo na kinachokuja.
Dini yako, au Cheo chako au mamlaka yako haina maana yoyote kwetu ikiwa unataka kuliingiza taifa katika hasara na ubinafsi wa hovyo.

Acheni upumbavu! Mtu akitoa hoja isikilizwe hoja yake na sio ni wadini gani.

Kama mkataba haufai, urekebishwe. Hiyo ndio hoja. Mambo ya sijui Amani, sijui mgawanyiko, hayo yote yataletwa na watu wabinafsi na wasiotaka kusikiliza wengine.
Mgawanyiko ni muhimu ikiwa tunatofautiana. Hiyo iwekwe wazi. Kama Watu hawataki wawe wamoja, kujaribu kuwaunganisha Watu wasiofanana ndio ukosefu wa Amani, mitafaruku, unyanyasaji na ukatili. Hatuwezi lazimisha umoja wa kinyonyaji, umoja wa wengine wanafaidi wengine wanasota, huo umoja haupogo labda kinafiki.

Nisikilizeni, umoja unaletwa Kwa kuangalia wengi wanasema nini, lakini pia Kwa kuzingatia maslahi ya taifa na kizazi kijacho.

Upendo, Haki, Ukweli na Akili hiyo ndio namna ya kuwaweka Watu pamoja. Utibeli.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Tunasema ni udini kwa sababu wapingaji wakubwa ni Wakristo, tena unajadiliwa Makanisani.
Na hata waliofungua kesi wote ni wagalatia, sio bahati mbaya. Hata Padri Slaa kaibuka sasa hv ni kwa sababu tu maslahinya kanisa lake yameguswa.

Tusidanganyanye zama hz, hapo issue ni UDINI TU
 
Kuwa ccm ni laana tosha yaani hadi viongozi wao ni wa hovyo na hawatumii akili, yaani watu wengi tu wametoka mbele kuunga mkono hii hoja hawajaitwa wadini ili ukipinga tu ni udini, kingine cha kushangaza kiongozi anakwenda kufungua kanisa anasema tusichanganye dini na siasa wakati anaongelea mambo ya siasa akiwa kanisani akili zao ni za ajabu sana

😀😀
 
Huo mkataba hakuna ambaye hautaki ishu inayotakiwa ni marekebisho tuu.
Sasa tatizo lipo wapi?
... ndio waulizwe CCM sasa! Badala yake wanakimbilia udini! Hawa watu ni hatari kuliko ukoma aliosema Mwl. Nyerere ambaye hadi speech zake za kizalendo zimeondolewa kwenye media za taifa.
 
Sawa sawa,

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Mapadri washatoa waraka huko. Nenda kanisani kuna majibu yako, humu utasubiri sana
 
Kwa hiyo viongozi wa kisiasa wakipuyanga unataka viongozi wa dini wakae kimya?
Wananafasi ya kutoa ushauri ila hawanafasi ya kuweka political presha kupitia majukwaa yao ya taasisi zao kwa kuwa wakifanya hivyo wanahatarisha umoja kwa kuwa dini zipo nyingi italeta mtafaruku heri ya Zambia wanadini ya taifa ila hapa kwetu hatuna .
Na pia jamani kama wao wanatufundisha uvumilivu basi na wao waanze kuyatenda wale wanayotufundisha ukitoa ushauri usiposikilizwa kuwa mvumilivu na sio kuleta ukaidi kwa kuwa unameans za kufanya hivyo.
 
Tunasema ni udini kwa sababu wapingaji wakubwa ni Wakristo, tena unajadiliwa Makanisani.
Na hata waliofungua kesi wote ni wagalatia, sio bahati mbaya. Hata Padri Slaa kaibuka sasa hv ni kwa sababu tu maslahinya kanisa lake yameguswa.

Tusidanganyanye zama hz, hapo issue ni UDINI TU

Wakati JPM akandikiwa Waraka za kubinya Uhuru na Haki za kutoa Maoni haikuwa UDINI?

Wabadilishe vipengele vinavyolalamikiwa kisha watakaoendelea kupinga hao sasa watakuwa na matatizo
 
Wananafasi ya kutoa ushauri ila hawanafasi ya kuweka political presha kupitia majukwaa yao ya taasisi zao kwa kuwa wakifanya hivyo wanahatarisha umoja kwa kuwa dini zipo nyingi italeta mtafaruku heri ya Zambia wanadini ya taifa ila hapa kwetu hatuna .
Na pia jamani kama wao wanatufundisha uvumilivu basi na wao waanze kuyatenda wale wanayotufundisha ukitoa ushauri usiposikilizwa kuwa mvumilivu na sio kuleta ukaidi kwa kuwa unameans za kufanya hivyo.

Unajua Amani inahatarishwa na nini? Au amani inashikiliwa na nini?
 
Back
Top Bottom