Kwa nini mabosi au Watu wenye hela nyingi hawajengi kwao? Mkienda kuzika mpaka unaona aibu

Kwa nini mabosi au Watu wenye hela nyingi hawajengi kwao? Mkienda kuzika mpaka unaona aibu

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Hii n changamoto sana hapa mjini kwa kwelii.....Najiuliza kwa nini mabosi wengi maofisini wana shida kubwa hawajengi makwao wanapotoka??[sio wote] Na sasa hadi wafanyabiashara wakubwa wanajaza majumba Dar wanazikwa kijijinI. Majuzi kati nilienda kumzika bossi mmoja Tanga aisee nilishtuka.


Dar ana nyumba kama 3 nzuri, kufika tunakunja kona tunasimama gafla kushoto nyumba za udongo kulia same zimechoka mbaya, nkauliza tumefika nkaambiwa ndio. Tukashuka kuweka kubeba maiti kuingiza ndan dah nasikia kama nyumba inataka kubomoka tukambiwa ndan tupungue jaman

Hewa nzito dah nkakimbia nje fasta. Hakika.Tujifunze kujenga nyumban kuna raha zake. Unajitenga na aibu

Uunasaidia wanao hata kuwa na nguvu ya kukaribisha marafiki


Kazi ipoo


Tujemge nyumban
 
Kilichokupeleka ni kuzika tu sio kuchora maisha ya mtu ni giza
 
Huwa wanatia aibu yan mnapeleka maiti huku mnasafisha njia
 
1. Tangu lini maiti ikaona aibu?
2.Hiyo nyumba unayojenga kijijini Aishi nani sasa?
3. Kwa kifupi acha mawazo ya kizamani. Hakuna umuhimu wowote wa kujenga nyumba kijijini na Wala hakuna ulazima wa kuzikwa kijijini ukifariki.
 
Back
Top Bottom