Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Kwa nini Mwamposa na mitume wenzake wa kileo wanaonekana matapeli na waamini wa dini na madhehebu mengine wakati ukifuatilia katika historia ya dini zote kubwa mbili utakuta kuna historia ndefu ya miujiza ya ajabu sana iliyofanyika kupitia mitume katika Uislamu na Ukristo?
Mifano michache kutoka katika Ukristo na Uislamu ni pamoja miujiza ya mwezi kupasuka vipande viwili na kujirudia wakati wa Muhammad, bikira kumzaa Yesu, jua kusimama kwa maombi ya Joshua, mikate kudondoka kutoka mbiguni wana Israel wakala, maji kutoka kwenye vidole vya Muhammad, Yona kumezwa na kukaa tumboni kwa Samaki siku tatu.
Mfano wa Miujiza ya Wakatoliki wa zamani ni pamoja
Mtakatifu Joseph wa Cupertino wa Wakatoliki aliyeishi miaka ya 1,600 alikuwa anapaa angani kama ndege, huyo ndio msimamazi wa marubani Wakatoliki
Mtakatifu Anthony wa Padua alikuwa anafufua watu
Mtakatifu Padre Pio wa Pietrelcina alikuwa anaweza kuonekana miji tofauti kwa wakati mmoja
Kwa nini iwe nongwa na kelele kubwa mtume Mwamposa na mitume wengine hapa Tanzania wakifanya miujiza?!