Kwa nini Mkuu wa Mkoa atamani Ubunge ambao kimamlaka ni Cheo Cha chini kulinganisha na RC?

Kwa nini Mkuu wa Mkoa atamani Ubunge ambao kimamlaka ni Cheo Cha chini kulinganisha na RC?

Hamjambo hapo Arusha?

JeNi kwa sababu ipi,

Kisha Ili iweje?

Na aliyemteua RC atajisikiaje akipata habari kuwa, RC hafurahii Nafasi aliyopewa na Rais, anaitamani Nafasi ya kupewa na wananchi( ubunge)?

Kila siku unatoka na kutwambia WEWE ni mwakilishi wa Rais, una mamlaka juu ya mkoa nzima, unaweza hata kumweka ndani mbunge, nyuma ya pazia unatengeneza mazingira uje ugombee ubunge huo huo Ili uje kuwa chini ya RC?


Mwenye majibu aje kunisaidia🙏
Tamaa ya ubunge imelenga, marupurupu na cheo cha uwaziri (misifa kibao) isiyokuwepo kupitia ulaghai wa siasa
 
Kuchaguliwa na wanachi ni heshima zaidi kuliko kuteuliwa. Kama sikosei hata marupurupu ya mbunge ni makubwa kuliko ya RC.
 
Ukifuatila kwa makini utagundua ubunge ni kama sehemu ya kwenda kupumzika tu na kufanya biashara, pressure yake ipo wakati wa kugombea ukishapata basi na unahamia Dar, wakati mkuu wa mkoa kila siku unapaswa kuwa ofisini na unashughulika na kero za mkoa mzima na karibu idara zote za mkoa zipo chini yako hivyo hata figisu ni nyingi sana hivyo kudumu kwenye kiti inategemea sana kudra za mwenyezi Mungu.
 
Hamjambo hapo Arusha?

JeNi kwa sababu ipi,

Kisha Ili iweje?

Na aliyemteua RC atajisikiaje akipata habari kuwa, RC hafurahii Nafasi aliyopewa na Rais, anaitamani Nafasi ya kupewa na wananchi( ubunge)?

Kila siku unatoka na kutwambia WEWE ni mwakilishi wa Rais, una mamlaka juu ya mkoa nzima, unaweza hata kumweka ndani mbunge, nyuma ya pazia unatengeneza mazingira uje ugombee ubunge huo huo Ili uje kuwa chini ya RC?


Mwenye majibu aje kunisaidia🙏
Inatakiwa Makonda awe Mbunge harafu Gambo arudishwe kuwa RC
 
Basi mamlaka teuzi impe ubunge wa kusukumiziwa kwenye Nafasi zile za kando kama Mbatia.
 
Kumbe hauwezi kuwa liwali ukiwa RC?

Lakini liwali ni mteule wa Rais kama tu RC, hii ni tamaa,

Mtu wa aina hii hatosheki, akipata uliwali, ataanza safari ya kutamani kiti Cha Mkuu wa maliwali.


Hafai.
Ndio maana hayati mh Jiwe alihakikisha kijana huyo mwenye tamaa hatoboi ubunge kigamboni 2020
 
Mbunge yupo Bungeni anaonana na Mawaziri wengi.
Madili ni mengi huko kama unataka connection kwenye miradi ya kila siku
Ubunge unalipa kwa wanaopenda vya mteremko
 
Ndio maana hayati mh Jiwe alihakikisha kijana huyo mwenye tamaa hatoboi ubunge kigamboni 2020
Mfano mzuri ni Ile nafasi ya chama.

Haukita muda, naye akaanza kutembea na msafara na kukodi waandishi.
 
Mbunge hapangiwi sana kama mkuu wa mkoa au DC mbunge anapata joto baada ya miaka minne ya uchaguzi,

Mkuu wa mkoa kudumu kwa miaka zaidi ya mitatu ni nadra sana
RC ni cheo ambacho hakina mkataba, mwenyewe anaweza kuku-delete hata baada ya wiki mbili tu. Ubunge ni mkataba mzuri wa kikatiba, unachowaza ni jinsi ya kupata mitano ijayo, na ndani ya bunge fursa ziko nyingi sana za kupata pesa nono ya ziada.
 
Kweli kabisa lakini mbunge anaonana na mawaziri kila siku akitaka.
Na wanakunywa chai pamoja na kupeana mawili matatu

La kuonana na Rais ni sawa ila madili yapo huku chini
Kumbe kuna biashara kwenye ubunge na u RC?

Nilidhani ni utumishi wa umma!
 
Back
Top Bottom