Hata hivyo binafsi naona Trump kawastahi sana, kama angetaka angeweza kuwadhalilisha zaidi, kumbukeni genge hili la viongozi wa EU na Uingereza ndilo linampiga vita vya chini chini Trump hawataki afanikiwe kufanya usuruhishi/sitisha vita huko Ukraine, wanamvimbisha kichwa Zelensky kubishana bishana na Trump wanampatia ushauri potofu nini cha kuzungumza na Trump, halafu kibaya zaidi wanag'ang'aniza kwamba lazima na wao wawe wanashirikishwa kwenye mikutano yote baina ya Trump na Zelensky as if Ukraine ni koloni la EU na Uingereza!!
Jamaa hawa jeuri sana na kujisikia -
hata hivyo naona hapo Trump kawastahi sana angeweza kuwatimulia mbali kwani tatizo liko wapi? Si wao wanapania ku-undermine juhudi za Trump kumaliza mgogoro wa Ukraine, yote hayo Trump amekwisha gundua ndio maana hawakukarishwa huko Alaska.
Hivi kwa akili za kawaida walitegemea Trump ata react vipi to cut them to SIZE hasa baada ya wao kuitisha mkutano wa waandishi wa habari kupinga mapendekezo ya Trump siku mmoja kabla ya mkutano wa Trump na Putin huko Alaska, hizo zilikuwa ni hujuma za wazi wazu zenye lengo ovu sana, wao deep down wanataka vita hii iendelee huko Ukraine ili viwanda vya silaha huko Ifaransa,Ujerumani na Uingereza viendelee kufaidika kwa kuuza silaha lakini Trump anataka vita visitishwe ili kuokoa maisha ya raia na wanajeshi wanao kufa kwa maelfu kila siku.
Viongozi hawa wa EU na Uingereza hata wafanye mbinu gani za kuhujumu juhudi za Trump za kusitisha vita hii binafsi bado nina imani kwamba Trump atabuni njia za kuwakomesha, kuwakalisha kwenye bench kama wanaomba ajira hiyo ni njia moja wapo ya kidiplomasia kufikisha ujumbe kwamba hapendelei/anapinga tabia zao za kitoto.