Mkuu unasemaje juu ya mamlaka ya kufunga na kufungua?
Mkuu unaongelea haya maandiko ama!?
Mathayo 16:19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni
Mathayo 18:18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
Mathayo 18:19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Pia naomba unisaidie iwapo mtu ameishi maisha yake ya uchaji wa Mungu kikamilifu na ikatokea wakati anakufa alikua na hasira au hakuweza kumsamehe mtu flani, je mtu huyo ataenda jehanamu?
Hili mkuu lipo katika case ya kuhukumu ambayo siyo kazi yangu...
1 Timotheo 5:21 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.
Yakobo 4:12 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?
Mimi naamini kuwa nikiwaombea wafu Mungu aweza kuwasamehe hasa nikiomba kwa imani. Kama tujuavyo kwa wale waamini kuwa Mungu bado huonyesha maono so ukisoma wamakabayo utaona wenzetu walivyofanya. Na kwa upande mwingne ukiangalia agano jipya halijatuwekea limit ya maombi hasa inaposema ombeni jambo lolote kwa jina langu ........ na hata sasa hamjaomba ombeni ili furaha yenu iwe timilifu. Je Mungu anajicontradict mwenyewe au wewe nini maoni yako juu ya haya.
Labda hapa ningependa kujua unawaombea wafu ya kwamba ili wasamehewe dhambi wapate kuurithi uzima wa milele au!? Lakini principle ya uzima wa milele ni hii
Yohana 3:36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Warumi 6:22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
Hapo juu naona umetoa mfano ila kwa maelezo yako kuna uwezekano kwamba basi tunaweza tukafanya hivi wakaondolewa dhambi halafu wakaurithi Ufalme wa Mungu... Lakini mkuu Ufalme wa Mungu una Principle zake...
Kumbuka: Hautahesabiwa dhambi usipowaombea wafu amani iamue moyoni mwako ikiwa waona sawa basi fanya ikiwa waona si sawa acha usiwaombee . Ni vema ukaishi maisha yako kikamilifu kwani tumeambiwa amani iamue moyoni mwetu , naamini nawe unae huyo mfalme wa amani. Mungu akubariki tuazidi kuichuchumilia taji na kupiga vita vya imani kwa imani thabiti
Ubarikiwe pia mkuu, lakini hii ni sawa umelima shamba wakati wa mavuno nakuja mimi halafu naanza kukupangia haya weka ghalani haya nenda kauze, haya mahindi weka ya kuchoma, nadhani sitokuwa nimefanya kosa ila wewe ndio utaamua uchukue mawazo yangu ninayokung'ang'aniza au ufanye kama ulivyopanga mwenyewe, na mimi sitokulaumu kwanini hujanifuatiliza mimi...
Kabla ya kuendelea kuna verses nimeweka mwanzoni kabisa kuhusiana na lile swala la Kufunga na kufungua, ningependa pia kuona mawazo ya hawa wakuu tuweze kujadili, pia kujadili na hili la kuombea wafu wasamehewe dhambi
Eiyer,
Ishmael,
2013,
Kichwa Ndio Mtu...