Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Nimekusoma mkuu,nakua nafikili sana jambo hili na tena wafanyao haya ni wale wale tunaowaona wanaingia kwenye nyumba za ibada kila mala,mizimu ni kitu gani?na kama ni wafu nini kinachofanya kazi kwao juu walio hai,iweje babu wa babu alikua mzinzi,mlevi,mchawi na kila aina ya dhambi na mtu anajua lakini anaenda kumuomba makaburini amsaidie,napata shida hapa labda nielimishwe vyema

Hakuna shida ukiwaomba wafu waliokufa katika hali ya neema....
 
ni wazi ya kua MUNGU ni mwenye huruma na upendo na anasikiliza maombi yetu,nasi tumemjua MUNGU kwa kupitia vitabu vyake vitakatifu,kwa upande wetu tumemjua MUNGU kwa Biblia takatifu,na katika Biblia hio tumeambiwa kila kilichoandikwa kule kimetoka kwa MUNGU na kimeakikishwa na kinatufaa sisi katika mafundisho,, katika Biblia takatifu kitabu cha wamakabayo 12;38-45 ukisoma kwa makini na kwa minajili ya kuelewa hautakuwa na sababu ya kuwa na shaka kumuambea marehemu msamaha kwa MUNGU kwa yale alioyafanya yalio kinyume na mapenzi yake MUNGU kama alivyofanya huyo Yuda katika kitabuhicho cha wamakabayo,na kusauri G'taxi ukakisome kwa vyovyote vile kitafute katika Biblia ile iliokamilifu na sio ile yenye vitabu pungufu. kila la heri ndugu.

Unaamini vipi pale MUNGU anapokutaka utubu kwa makosa yako kabla ya kufa kwako? iwapo utakufa ukiwa ktk dhambi hutakua na muda tena wa kutubu isipokua kusubili hukumu..sasa kama umekufa katika dhambi vipi nikuijie na shida zangu kwa maombi unitatulie? au vipi nikuombee usamehewe dhambi huko uliko ilihali hakuna mtu hai anaejua maisha baada ya kufa kuna nini tuendako?

binafsi unaamini ibada hii? unawezaje kumuombea mfu aliejulikana kua aliua, aliiba,alikua na kila aina ya ubaya eti atasamehewa na hakutubu yeye mwenyewe kwa ridhaa yake kabla ya kufa..kwanza tukirudi kwenye imani bado inasema 1 Thessalonian 4:13 inasema sio kwamba hawataki tusijue habali ya waliolala mauti..inaendelea kusema tusije tukahuzunika kama wengine wasio na matumaini,ni vyema ndugu usemayo maana tunapeana kujua lakini sijalidhika bado
 
Last edited by a moderator:
ni wazi ya kua MUNGU ni mwenye huruma na upendo na anasikiliza maombi yetu,nasi tumemjua MUNGU kwa kupitia vitabu vyake vitakatifu,kwa upande wetu tumemjua MUNGU kwa Biblia takatifu,na katika Biblia hio tumeambiwa kila kilichoandikwa kule kimetoka kwa MUNGU na kimeakikishwa na kinatufaa sisi katika mafundisho,, katika Biblia takatifu kitabu cha wamakabayo 12;38-45 ukisoma kwa makini na kwa minajili ya kuelewa hautakuwa na sababu ya kuwa na shaka kumuambea marehemu msamaha kwa MUNGU kwa yale alioyafanya yalio kinyume na mapenzi yake MUNGU kama alivyofanya huyo Yuda katika kitabuhicho cha wamakabayo,na kusauri G'taxi ukakisome kwa vyovyote vile kitafute katika Biblia ile iliokamilifu na sio ile yenye vitabu pungufu. kila la heri ndugu.

Kitabu cha makabayo ni kitabu cha historia ya vita vya Israeli baada ya Alexander the Great kufa na ufalme wake kugawanywa kwa majenerali wake wanne na atiochus epiphane kulinajisi hekalu. Na kiliondolewa na kanisa kutoka katika canonical books kuwa hakina uvuvio wa roho mtakatifu maana ni historia tu ya vita. (aliyekiondoa.....kanisa katoliki) hii ni pamoja na vitabu vingine kumi kama sehemu ya kitabu cha ester, tobiti etc....unapovisoma vitabu hivyo ni kama unasoma vitabu vya historia ya israeli vilivyoandikwa na Josefus (kama nimepatia jina)....Kama Wamakabayo unaiona kuwa ni kitabu chenye uvuvioa basi hata machapisho ya Josefus kwako ni ya kiroho.

Mtu anayemwombea marehemu vitani kwa uchungu wa kuwa amepoteza mpiganaji huwezi kuichukua hiyo kuwa sala rasmi....kumbuka matendo humtangulia mtu, yeye anayafuata tu. Hiyo ndiyo hukumu ya Mungu.

Ni vyema wewe mwenyewe ukaanza kujiombea kabla hujafa na matendo yako yakawa mema na si usubiri wazinzi, makahaba, na wenye dhambi wengine eti waje wakuombee ukiisha kufa....Hajiri alimwomba Mungu amlinde mwanawe Ishmaeli (Mwanzo 21:14-19)....hakusubiri mpaka Ishmaeli afe.

Biblia inasema...Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. kinachotakiwa ni ukiri wako wewe mwenyewe si ukiri wa watu wengine kwa niaba yako ukishakufa.

Ukishakufa kinachofuata ni hukumu tu, instantly....mengine yote yanayofanyika duniani ni mbwembwe za maombolezo na kutulizana pressure kwa ndugu wa mfiwa na hayana impact yoyote kwa marehemu.
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti,bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu..... Warumi 6:23
 
Ngoja nilale kwanza kisha nitarudi kuchangia hii mada...

By the time ngoja niwaite akina Ntuzu, Mkuu wa chuo, Ablessed, Barnabas Shadrack, Blue G hippocratessocrates na wengineo waendelee na mjadala huu....

Hii Ibada ya kuombea wafu, naona Utingo ameelezea kwa uzuri, Ukiliangalia hili andiko la Waebrania linasema baada ya kufa ni hukumu, sasa hii ya kuombea wafu ili kuwaondolea dhambi sijui imekaaje

Waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
 
ni mbwembwe tu za siasa na falsafa za viongozi wa dini na makanisa ili kutulizana pressure za ndugu wa mfiwa/wafiwa na kupata pesa. Si unajua ibada lazima iendane na matoleo?
 
Hii Ibada ya kuombea wafu, naona Utingo ameelezea kwa uzuri, Ukiliangalia hili andiko la Waebrania linasema baada ya kufa ni hukumu, sasa hii ya kuombea wafu ili kuwaondolea dhambi sijui imekaaje

Waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
Mkuu unasemaje juu ya mamlaka ya kufunga na kufungua? Pia naomba unisaidie iwapo mtu ameishi maisha yake ya uchaji wa Mungu kikamilifu na ikatokea wakati anakufa alikua na hasira au hakuweza kumsamehe mtu flani, je mtu huyo ataenda jehanamu? Mimi naamini kuwa nikiwaombea wafu Mungu aweza kuwasamehe hasa nikiomba kwa imani. Kama tujuavyo kwa wale waamini kuwa Mungu bado huonyesha maono so ukisoma wamakabayo utaona wenzetu walivyofanya. Na kwa upande mwingne ukiangalia agano jipya halijatuwekea limit ya maombi hasa inaposema ombeni jambo lolote kwa jina langu ........ na hata sasa hamjaomba ombeni ili furaha yenu iwe timilifu. Je Mungu anajicontradict mwenyewe au wewe nini maoni yako juu ya haya.

Kumbuka: Hautahesabiwa dhambi usipowaombea wafu amani iamue moyoni mwako ikiwa waona sawa basi fanya ikiwa waona si sawa acha usiwaombee . Ni vema ukaishi maisha yako kikamilifu kwani tumeambiwa amani iamue moyoni mwetu , naamini nawe unae huyo mfalme wa amani. Mungu akubariki tuazidi kuichuchumilia taji na kupiga vita vya imani kwa imani thabiti
 
Bado ni mkanganyiko..hujasema kama kuna umaana wa kwenda kuwaomba wafu watutatulie matatizo yetu hapa duniani kama wengi wafanyavyo mala kadhaa makabulini kwa mababu,kama tu ilisemwa na alaaniwe amtegemeaye mwanadamu vipi amtegemeaye mtu alieisha kufa?
 
Mkuu unasemaje juu ya mamlaka ya kufunga na kufungua? Pia naomba unisaidie iwapo mtu ameishi maisha yake ya uchaji wa Mungu kikamilifu na ikatokea wakati anakufa alikua na hasira au hakuweza kumsamehe mtu flani, je mtu huyo ataenda jehanamu? Mimi naamini kuwa nikiwaombea wafu Mungu aweza kuwasamehe hasa nikiomba kwa imani. Kama tujuavyo kwa wale waamini kuwa Mungu bado huonyesha maono so ukisoma wamakabayo utaona wenzetu walivyofanya. Na kwa upande mwingne ukiangalia agano jipya halijatuwekea limit ya maombi hasa inaposema ombeni jambo lolote kwa jina langu ........ na hata sasa hamjaomba ombeni ili furaha yenu iwe timilifu. Je Mungu anajicontradict mwenyewe au wewe nini maoni yako juu ya haya.

Kumbuka: Hautahesabiwa dhambi usipowaombea wafu amani iamue moyoni mwako ikiwa waona sawa basi fanya ikiwa waona si sawa acha usiwaombee . Ni vema ukaishi maisha yako kikamilifu kwani tumeambiwa amani iamue moyoni mwetu , naamini nawe unae huyo mfalme wa amani. Mungu akubariki tuazidi kuichuchumilia taji na kupiga vita vya imani kwa imani thabiti

Umuombee mtu mfu kwa lipi kwa mfano? Asamehewe dhambi au unamuombea nini? Au unaomba kwa mtu aliekufa upate mibaraka?
 
Mkuu unasemaje juu ya mamlaka ya kufunga na kufungua? Pia naomba unisaidie iwapo mtu ameishi maisha yake ya uchaji wa Mungu kikamilifu na ikatokea wakati anakufa alikua na hasira au hakuweza kumsamehe mtu flani, je mtu huyo ataenda jehanamu? Mimi naamini kuwa nikiwaombea wafu Mungu aweza kuwasamehe hasa nikiomba kwa imani. Kama tujuavyo kwa wale waamini kuwa Mungu bado huonyesha maono so ukisoma wamakabayo utaona wenzetu walivyofanya. Na kwa upande mwingne ukiangalia agano jipya halijatuwekea limit ya maombi hasa inaposema ombeni jambo lolote kwa jina langu ........ na hata sasa hamjaomba ombeni ili furaha yenu iwe timilifu. Je Mungu anajicontradict mwenyewe au wewe nini maoni yako juu ya haya.

Kumbuka: Hautahesabiwa dhambi usipowaombea wafu amani iamue moyoni mwako ikiwa waona sawa basi fanya ikiwa waona si sawa acha usiwaombee . Ni vema ukaishi maisha yako kikamilifu kwani tumeambiwa amani iamue moyoni mwetu , naamini nawe unae huyo mfalme wa amani. Mungu akubariki tuazidi kuichuchumilia taji na kupiga vita vya imani kwa imani thabiti

Kwenye Blue: Suala la mtu kwenda mbinguni au kutokwenda...God has limited us to know as it is another dimension. Tafsiri yako ya mtu kuwa na hasira inawezekana ni ujinga wa wewe mwenyewe kutojua maana ya hasira? Kama unamhukumu mtu kuwa alikuwa na hasira wakati anakufa (which is awkward argument)...Nami nikuulize Yesu alipomfokea Petro hata akasema rudi nyuma yangu shetani, uungu wa Yesu ulikoma na hivyo Yesu alikoma kuwa mwana wa Mungu kwa sababu alifoka kuonyesha hasira yake?

Kwenye Red: nikujibu kirahisi....pengine hujui maana ya imani. imani ni kutarajia yajayo wewe binafsi ukiwa hapa duniani. Imani yako wewe uliye duniani haiwezi kubadili hukumu ya mtu aliyekwisha kufa na kuhukumiwa....soma Biblia uielewe. Fate ya mwanadamu iko mikononi mwake yeye mwenyewe na si kwa mtu mwingine. Ndiyo maana Biblia inasema atendaye uovu na azidi kutenda na atendaye haki azidi kutenda haki....maana kila tendo analolitenda mwanadamu awapo duniani lina malipo na hukumu...wewe huwezi kumshawishi Mungu abadili mshahara wa mtu, wakati mtu mwenyewe alisaini contract......ndiyo sababu tunashauriwa kumwomba Mungu atuwezeshe kushinda dhambi kila siku na atusamehe. If you cant do that ukitegemea sala za wafu...POLE
REMEMBER: You are the master of your own destiny, God only fulfills it.
 
Mkuu unasemaje juu ya mamlaka ya kufunga na kufungua?
Mkuu unaongelea haya maandiko ama!?

Mathayo 16:19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni

Mathayo 18:18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.

Mathayo 18:19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.

Pia naomba unisaidie iwapo mtu ameishi maisha yake ya uchaji wa Mungu kikamilifu na ikatokea wakati anakufa alikua na hasira au hakuweza kumsamehe mtu flani, je mtu huyo ataenda jehanamu?
Hili mkuu lipo katika case ya kuhukumu ambayo siyo kazi yangu...

1 Timotheo 5:21 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.

Yakobo 4:12 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?

Mimi naamini kuwa nikiwaombea wafu Mungu aweza kuwasamehe hasa nikiomba kwa imani. Kama tujuavyo kwa wale waamini kuwa Mungu bado huonyesha maono so ukisoma wamakabayo utaona wenzetu walivyofanya. Na kwa upande mwingne ukiangalia agano jipya halijatuwekea limit ya maombi hasa inaposema ombeni jambo lolote kwa jina langu ........ na hata sasa hamjaomba ombeni ili furaha yenu iwe timilifu. Je Mungu anajicontradict mwenyewe au wewe nini maoni yako juu ya haya.
Labda hapa ningependa kujua unawaombea wafu ya kwamba ili wasamehewe dhambi wapate kuurithi uzima wa milele au!? Lakini principle ya uzima wa milele ni hii

Yohana 3:36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Warumi 6:22 Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.

Hapo juu naona umetoa mfano ila kwa maelezo yako kuna uwezekano kwamba basi tunaweza tukafanya hivi wakaondolewa dhambi halafu wakaurithi Ufalme wa Mungu... Lakini mkuu Ufalme wa Mungu una Principle zake...

Kumbuka: Hautahesabiwa dhambi usipowaombea wafu amani iamue moyoni mwako ikiwa waona sawa basi fanya ikiwa waona si sawa acha usiwaombee . Ni vema ukaishi maisha yako kikamilifu kwani tumeambiwa amani iamue moyoni mwetu , naamini nawe unae huyo mfalme wa amani. Mungu akubariki tuazidi kuichuchumilia taji na kupiga vita vya imani kwa imani thabiti
Ubarikiwe pia mkuu, lakini hii ni sawa umelima shamba wakati wa mavuno nakuja mimi halafu naanza kukupangia haya weka ghalani haya nenda kauze, haya mahindi weka ya kuchoma, nadhani sitokuwa nimefanya kosa ila wewe ndio utaamua uchukue mawazo yangu ninayokung'ang'aniza au ufanye kama ulivyopanga mwenyewe, na mimi sitokulaumu kwanini hujanifuatiliza mimi...

Kabla ya kuendelea kuna verses nimeweka mwanzoni kabisa kuhusiana na lile swala la Kufunga na kufungua, ningependa pia kuona mawazo ya hawa wakuu tuweze kujadili, pia kujadili na hili la kuombea wafu wasamehewe dhambi Eiyer, Ishmael, 2013, Kichwa Ndio Mtu...
 
Last edited by a moderator:
Nimekua najiuliza ni kwa nini mala nyingi hasa mwisho wa mwaka utasikia watu wengi wanakimbia majumbani mwao hasa vijijini na lengo ni kwenda kuwaombea ndugu walioishatangulia kwa maana ya kufa.

Wanaenda mbali na kupeleka maombi yao juu ya maisha yanayowazunguka kwa hao waliokufa,ni kweli kuna maana yoyote au kuna ulazima wa kufanya hili?kama ni kweli MUNGU tunaemuabudu na kuamini kua yupo na ndiyo alietuumba anapata nafasi ipi iwapo tutafikia kupeleka shida zetu kwa wafu?
Kwa ufupi tu:

Maombi kwa ajili ya wafu.
viongozi wengi hufundisha kwamba hakuna kuokoka duniani na hao hao mtu akifa wanamwombea kwamba alazwe pema peponi kana kwamba kuna wokovu baada ya kufa. Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu.(Waebrania 9:27).

-Ndugu zangu hakuna mtumishi, mchungaji, nabii, padri au askofu aliye mkweli kuliko neno la MUNGU. Sasa hizi habari za kuombea wafu tena wafu wengine ambao ni maarufu au viongozi wa serikali huombewa kila mwaka ili wahamie pema peponi. Hii ni kujidanganya na kujifariji ubatili.

-Kanisa haliwezi kuomba mfu kupumzika kwa amani pema peponi, Ndugu zangu wakati wa wokovu ni sasa hivyo baada ya kufa ni hukumu. Watakie kupumzika kwa amani wafu ila tambua kwamba huwezi kuwabadilishia makao yao ya milele, kama ni mbinguni ni mbinguni tu na kama ni motoni ni motoni tu.

*Kuombea wafu huwafanya wenye dhambi kuendelea kutenda dhambi wakiamini kwamba baada ya kufa kanisa litaomba ili wao waingie mbinguni. Ndugu nakuambia tena WOKOVU NI SASA.

Katika Luka 16:26…Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.'' Biblia inatuonyesha watu waliokufa wengine wako pema peponi na wengine wako kuzimu,'' ''

MUNGU humpokea mwenye dhambi ambaye hutubu kwa woyo na kujitakasa kwa msingi wa imani peke yake katika damu ya YESU KRISTO. Hivyo humpa uzima wa milele. 2 Kor 6:2''(Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa) ''

Wakati wa wokovu ni sasa

Wakati wa kuokolewa/kuokoka ni sasa

Wakati huu ndio unatakiwa kuokolewa sio baada ya kufa.
 
kama wanafanikiwa wakiwaomba wafu mi nasema na waendelee tu.
 
kuanzia mleta mada na wote waliochangia kwa mtazamo pingamizi mnachotakiwa ni kujitafakari kama mna Roho wa Mungu wakati mnapo ya tafsiri maandiko matakatifu, sio kwa kufuata hisia zenu au mitazamo yenu mkajua ndivyo ilivyo, kumbukeni ya kuwa MUNGU ni mwenye huruma na upendo na hugairi hasira yake.

kama mimi kwa imani ni tamuomba MUNGU kwa jina la YESU KRISTO ya kua kipindi kile atakaporudi BWANA marehemu baba yangu au mama yangu au mkristo mwenzangu nae akawe miongoni mwa wale wakumlaki BWANA, kwa kua nae aliamini kuwa KRISTO ni BWANA na akabatizwa katika maji na Roho, pale aliposhindwa kutimiza wajibu wake kwa namna yoyote basi kwa sadaka hii ya Misa takatifu akasamehewe.

hapo mimi nitakuwa na kosa gani,ni wapi nilipomuomba huyo aliekufa au nivipi labda nimefanya matambiko kwa mzimu? kumbukeni MUNGU hughairi mabaya na humsikiliza yule amuombae kwa imani na pia mkijua ya kua huyo aliekufa hawezi kuomba tena sasa kuna ubaya gani mimi nilie hai nikimuombea? JITAFAKARINI JE MNA ROHO WA MUNGU?.
 
kuanzia mleta mada na wote waliochangia kwa mtazamo pingamizi mnachotakiwa ni kujitafakari kama mna Roho wa Mungu wakati mnapo ya tafsiri maandiko matakatifu, sio kwa kufuata hisia zenu au mitazamo yenu mkajua ndivyo ilivyo, kumbukeni ya kuwa MUNGU ni mwenye huruma na upendo na hugairi hasira yake.kama mimi kwa imani ni tamuomba MUNGU kwa jina la YESU KRISTO ya kua kipindi kile atakaporudi BWANA marehemu baba yangu au mama yangu au mkristo mwenzangu nae akawe miongoni mwa wale wakumlaki BWANA, kwa kua nae aliamini kuwa KRISTO ni BWANA na akabatizwa katika maji na Roho,pale aliposhindwa kutimiza wajibu wake kwa namna yoyote basi kwa sadaka hii ya Misa takatifu akasamehewe. hapo mimi nitakuwa na kosa gani,ni wapi nilipomuomba huyo aliekufa au nivipi labda nimefanya matambiko kwa mzimu? kumbukeni MUNGU hughairi mabaya na humsikiliza yule amuombae kwa imani na pia mkijua ya kua huyo aliekufa hawezi kuomba tena sasa kuna ubaya gani mimi nilie hai nikimuombea? JITAFAKARINI JE MNA ROHO WA MUNGU?.

Ndugu pendael usijedhani unasoma uzi na michango ya wasiyomjua MUNGU..ibaya ya kuombea wafu na kutambika kwa wafu wakutatulie matatizo yako panamashaka makubwa kukubalika kwake,kama tu kumtegemea mwanadamu ni laana leo iwe mtu alieishatangulia mauti?
 
Sasa nimeielewa mada kumbe inazungumzia ibada ya matambiko na vitu kama hivyo basi si sawa/ibada hii si sahihi.
 
kuanzia mleta mada na wote waliochangia kwa mtazamo pingamizi mnachotakiwa ni kujitafakari kama mna Roho wa Mungu wakati mnapo ya tafsiri maandiko matakatifu, sio kwa kufuata hisia zenu au mitazamo yenu mkajua ndivyo ilivyo, kumbukeni ya kuwa MUNGU ni mwenye huruma na upendo na hugairi hasira yake.kama mimi kwa imani ni tamuomba MUNGU kwa jina la YESU KRISTO ya kua kipindi kile atakaporudi BWANA marehemu baba yangu au mama yangu au mkristo mwenzangu nae akawe miongoni mwa wale wakumlaki BWANA, kwa kua nae aliamini kuwa KRISTO ni BWANA na akabatizwa katika maji na Roho,pale aliposhindwa kutimiza wajibu wake kwa namna yoyote basi kwa sadaka hii ya Misa takatifu akasamehewe. hapo mimi nitakuwa na kosa gani,ni wapi nilipomuomba huyo aliekufa au nivipi labda nimefanya matambiko kwa mzimu? kumbukeni MUNGU hughairi mabaya na humsikiliza yule amuombae kwa imani na pia mkijua ya kua huyo aliekufa hawezi kuomba tena sasa kuna ubaya gani mimi nilie hai nikimuombea? JITAFAKARINI JE MNA ROHO WA MUNGU?.
Mkuu umeelezea vema , hapo kwenye kipengele cha Roho Mtakatifu nafikiri karibu wote wanae Roho wa Bwana shida ipo kwenye tofauti zetu za madhehebu . Na kwa jinsi hii hatutaweza kufikia muafaka.
 
Mkuu umeelezea vema , hapo kwenye kipengele cha Roho Mtakatifu nafikiri karibu wote wanae Roho wa Bwana shida ipo kwenye tofauti zetu za madhehebu . Na kwa jinsi hii hatutaweza kufikia muafaka.

Kwa nini tusifikie muafaka?we soma uzi juu utaelewa nimetaka kujua nini umaana wa kuwaombea wafu,kisha toa mawazo yako,tuko hapa kujengana uwezo na kile unachojua ndicho unachoweza kusema
 
Back
Top Bottom