Tatizo Biblia yenyewe haiko 'consistent' na inajipinga katika baadhi ya mambo na hivyo kuleta utata katika mambo hayo. Jambo moja linaweza kuonyeshwa kuwa linakubaliwa katika kitabu au mstari mmoja wa Biblia hali jambo hilo hilo linakataliwa katika kitabu au mstari mwingine wa Biblia. Kwa hiyo siyo vema kushikilia mstari mmoja wa Biblia au kusikiliza mchungaji mmoja anayesimamia baadhi tu ya mistari, bali ni muhimu kuangalia na kutathmini Biblia yote kwa undani kuhusu jambo unalotaka kulielewa lakini vilevile kuangalia muktadha (context) wa uandishi wa kitabu husika au mstari husika wa biblia.
Hii nakataa Biblia haijipingi, ila inatokana na jinsi gani ya watu wanavyofasiri maandiko na uelewa wa maandiko... Biblia haijipingi... labda ulete maandiko yanayojipinga halafu tujadili tuone kama ni kweli...
Kuwepo kwa Biblia mbili au tuseme tatu, yaani moja yenye vitabu 66 ambayo inakubaliwa na kutumiwa na makanisa ya kiprotestanti na ya kipentekoste na ile yenye vitabu 73 inayokubaliwa na kutumiwa na katoliki ni tatizo mojawapo la msingi. Lakini vile vile biblia ya ziada iliyoandikwa kutokana na vitabu vilivyokusanywa na kuandikwa kutokana na maandiko mbalimbali ya wafuasi wa Yesu ambayo yaliachwa nje ya biblia za mwanzo inayotumiwa na kanisa la Yesu la watakatifu wa baadae (The Church of Jesus Christ of Later Saints) ni tatizo jingine. Ndani ya biblia yenyewe kuna mambo yenye utata mfano kuhusu kama kunywa pombe ni dhambi au la - sehemu moja ya biblia inaruhusu kunywa pombe (divai/mvinyo) hata yesu anatengeneza divai kwa muujiza; sehemu nyingine inakataza watu kunywa pombe. Vile vile biblia hiyo hiyo inaruhusu watu kuoa wake wengi huku sehemu nyingine inataka mtu kuoa mke mmoja n.k.
kwanza hayo maelezo yako unatakiwa uelewe Biblia ni nini!? Unatakiwa uelewe ni kwanini vitabu vya Aprokifa havikuwekwa, Halafu na kina nani walioandika Biblia kama unavyosema... lakini naona
Utingo amejitahidi kuelezea lakini sijui haujasoma maelezo yake...
Hapo nilipoweka red, Unaanza kuongelea habari za Joseph Smith nabii wa Wamormons kanisa lake alilolianzisha mwaka 1827, kwa kifupi unaanza kuingiza imani za ajabu, tunapokuja katika neno la Mungu inabidi tuangalie neno linasemaje na sio kuanza kuingiza mafundisho ya watu, msingi wetu ni neno la Mungu... ukweli huwa una njia yake, na sio kubuni vitu na kuanza kuvisapoti kuvitengenezea njia...
Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Hapo nilipoweka blue ni kama nilivyosema mwanzo ni namna gani ya kuelewa scripture... kwa hiyo bado kuna shida hapo
Hapo nilipoweka purple, Labda ungeleta maandiko hapa tunaruhusiwa kuoa wake wengi hapa mke mmoja ndio tunaweza tukajadili, lakini vinginevyo naona ni mafundisho ya watu tu, kama kina Joseph Smith...
Jambo jingine lenye utata zaidi pia ni hoja ya kwamba baraza moja lililoandika biblia ya vitabu 66 lilivuviwa na Roho Mtakatifu, je kuna uhakika na ushahidi gani kuwa baraza jingine ambalo liliandika biblia ya vitabu 73 nalo halikuvuviwa na Roho Mtakatifu na hata hilo baraza jingine lililoandika biblia ya nyongeza ya Church of Jesus Christ of Later Saints kwamba nalo halikuvuviwa na huyo huyo Roho Mtakatifu?
Nani alikwambia baraza limeandika vitabu vya kwenye Biblia!? huoni kama unachokisema sio kweli!? sidhani hata kama unajua unachokizungumza... Yaani na mafundisho ya Wa Mormons unataka yafuatwe na watu, chukua hii verse inavyosema...
2 Timotheo 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
Vile vile kuna utata kuhusu uzito wa dhambi kana kwamba dhambi zote zina uzito sawa au zina uzito tofauti. Mfano katika biblia tunaona ikiandikwa kuwa kuna dhambi za mauti na dhambi nyinginezo (Kitabu cha waraka wa Yakobo/Yohana). Lakini watumishi wengine huzungumzia kuwa dhambi zote ni sawa. Hivyo kuleta maswali mengi kuhusu hukumu anayostahili mtu mfano aliyeua binadamu mwenzake na aliyeiba kwa mfano sindano au kuku, je wapewe hukumu na adhabu sawa? Tunaona hata katika torati adhabu zinaendana na uzito wa kosa/dhambi. Ndipo falsafa ya hell(Jehanamu), purgatory (toharani), na paradise (Heaven) [Mbinguni] inakuja. Na kwa kuzingatia kuwa Mungu ni mtakatifu na mwenye haki lazima aonekane kutenda haki kuliko mwanadamu ambaye ni mwenye dhambi. N.K.
Labda nikuulize swali, tunaishi kipindi cha torati au!? nani alikwambi kuna dhambi kubwa na dhambi ndogo!?
Warumi 5:20 Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;
Warumi 3:20 kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
Warumi 6:14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.