Kwa nini tuwaombee waliokufa?

Kwa nini tuwaombee waliokufa?

tatizo lako unategemea wikipedi inayoandikwa na wenye uelewa finyu kama wewe...mwishowe unaanza kutukana. Kama ni povu weewe ndiye unaanza kulimwaga.....calvin na martin luther wapi na wapi? theolojia yako ina mushkeli mkubwa sana. kwa kuwa umeanza kutukana basi inatosha. tafuta mwenye akili timamu nitaendeleza mjadala naye si wewe

Hapana tafadhari..tuwe watu safi wa MUNGU na tufundishane hapa,tusifikie kulushiana maneno na tukapoteza point..tuludi penye msingi wa uzi wangu kwa wote tupate majibu ya kulidhisha juu ya kuwaombea wafu na kupeleka shida zetu kwa wafu kama kuna umaana wowote wa kufanya hivyo...
 
Mkuu, shida si madhehebu tu. Shida ni baadhi ya watu kuuogopa ukweli. Ibada za wafu ni upagani. watu wanaogopa kuacha mabaya wanayoyatenda wanategemea ibada za wafu kuwa zitawatoa motoni?......unless Mungu stops to be God ndipo nitaamini ibada za wafu. Kwangu ni sawa na uganga wa kienyeji ambapo unakwenda kumwomba mganga/mchawi akunyenyulie roho ya bibi au babu au ndugu wa karibu aliyekufa ili akukinge na mabaya.

Tuwe jasiri kuface mapungufu yetu, tulijue Neno la Mungu na tuishi katika kweli. Falsafa mfu za makanisa na madhehebu yetu zilizotungwa na watu kwa kuangalia na kuyapalilia mapungufu yao ambazo zinapishana na Maandiko hazitatusaidia chochote.

Waebrani 9:27.........Baada ya kifo ni hukumu. Au andiko hili linyofolewe litolewe kwenye Maandiko?
Hapa mkuu naona kama unaongelea ibada za aina mbili tofauti . Kuna hii inayofanywa na madhehebu ya kikatoliki na inayofanywa na makabila ie matambiko. Ni kweli matambiko ni ibada ya kishetani na ni dhambi kufanya hivyo. Pia sidhani kama kuna mtu anakaa kwa kutegemea kuwa akifa ataombewa na dhambi zake zitasamehewa yaani aishi ktk dhambi ili akifa aombewe mmmmh mtu huyo atakua amepotea.

Ieleweke kuwa Mungu wetu ni mtakatifu sana na mwenye huruma mno sasa kuna dhambi waweza kufa nayo iliyo juu ya ufahamu wako lkn umeishi maisha yako kikamilifu . Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu sana hawezi kukupokea na hapo ndo inapokuja hii imani ya kuwaombea waliotangulia. Tukiomba wanasamehewa, haya yote ni mambo ya imani ikiwa huamini ktk hili basi kwako usilifanye na ikiwa waaamini hili ni vizuri ukifanya.
 
Hapo kwenye RED

Wakatoliki hawajawahi na wala hawato kuja kujaribu kupunguza neno lolote katika Biblia....Biblia ilikuwa na vitabu 73 na itakuwa hivyo mpaka mwisho..
Najua hivyo mkuu lkn waengine wanafikiri tuliondoa vitabu anyway nashukuru kwa somo zuri lbd litasaidia wengine kuelewa . Mkuu hapo juu nimeomba maelezo kuhusu petro alipomuona elia na musa na kusema na tujenge vibanda vitatu.

Kama tunasema hakuna uhusiano wa walio hai na waliolala je ni kwanini hawa walionekana. Naamini kwa uelewa wako waweza kulielezea hili vema na kulilinganisha na mada iliyopo mezani. Tafadhali naomba utupe darasa.
 
Hizo ni Ibada za Matambiko, wanaposema wanaenda kuwaombea marehemu basi ujue wao ndo wanapeleka hoja kwa marehemu ili wasafishiwe mambo yao.

Ni inahusu na Ibada za Mizimu, ni somo pana sana kuhusu Mizimu, hii huwa inaabudiwa kizazi hadi kizazi. Mungu alieumba Mbingu na Nchi kamwe hasikilizi maombi ya Wafu na kupitia Biblia Mungu hajaruhusu maombi ya Wafu.

Hivi wakati wa kuzika mbona zinapigwa sala kibao na ibada zinaendeshwa? Huku nako sio kuombea marehemu au kuombea waliokufa kama mada inavyosema? Kama inaruhusiwa wakati wa kumzika kwa nini iwe sio sawa akishazikwa? Kama biblia inasema hakuna kuombea marehemu/wafu si tungekuwa tunazika kama wagonjwa waliokufa kwa ebola tu yanaisha?
 
kwani mungu yupo? Waache wapeleke kwa wafu tu shida zao..angalau wamewahi kuwepo!!

1: Wafu wanasaidia...!?

2: Kila kionekanacho ndicho chenye kufuatwa/ kuogopewa....!?

3: Wafu na wazima wengi ni wepi....!?

4: Dini/ Imani ni nini....!?
 
Hivi wakati wa kuzika mbona zinapigwa sala kibao na ibada zinaendeshwa? Huku nako sio kuombea marehemu au kuombea waliokufa kama mada inavyosema? Kama inaruhusiwa wakati wa kumzika kwa nini iwe sio sawa akishazikwa? Kama biblia inasema hakuna kuombea marehemu/wafu si tungekuwa tunazika kama wagonjwa waliokufa kwa ebola tu yanaisha?
Mkuu umenifanya nicheke yaani ingekua unazika kimya kimya na kuondoka eti. Unajua haya mambo yanachanganya sana kama utakumbuka zamani hizo picha za Yesu zilipingwa mno lkn leo hii zinaonyeshwa na waliokua wanazipinga sasa na hili itafikia wakati watalikubali tu na watasema walikua wanajua ila wanafanya kwa tofauti.

Neno linaposema tuombe neno lolote ili furaha yetu iwe timilifu na mamlaka tuliyopewa ya kufunga na kufungua kilicho duniani na mbingu je hiki si kimojawapo. Uzuri wa neno la Mungu ukisema kwangu kula nyama ni dhambi basi unapewa sawa sawa na unavyoamini.
 
Tatizo Biblia yenyewe haiko 'consistent' na inajipinga katika baadhi ya mambo na hivyo kuleta utata katika mambo hayo. Jambo moja linaweza kuonyeshwa kuwa linakubaliwa katika kitabu au mstari mmoja wa Biblia hali jambo hilo hilo linakataliwa katika kitabu au mstari mwingine wa Biblia. Kwa hiyo siyo vema kushikilia mstari mmoja wa Biblia au kusikiliza mchungaji mmoja anayesimamia baadhi tu ya mistari, bali ni muhimu kuangalia na kutathmini Biblia yote kwa undani kuhusu jambo unalotaka kulielewa lakini vilevile kuangalia muktadha (context) wa uandishi wa kitabu husika au mstari husika wa biblia.

Kuwepo kwa Biblia mbili au tuseme tatu, yaani moja yenye vitabu 66 ambayo inakubaliwa na kutumiwa na makanisa ya kiprotestanti na ya kipentekoste na ile yenye vitabu 73 inayokubaliwa na kutumiwa na katoliki ni tatizo mojawapo la msingi. Lakini vile vile biblia ya ziada iliyoandikwa kutokana na vitabu vilivyokusanywa na kuandikwa kutokana na maandiko mbalimbali ya wafuasi wa Yesu ambayo yaliachwa nje ya biblia za mwanzo inayotumiwa na kanisa la Yesu la watakatifu wa baadae (The Church of Jesus Christ of Later Saints) ni tatizo jingine. Ndani ya biblia yenyewe kuna mambo yenye utata mfano kuhusu kama kunywa pombe ni dhambi au la - sehemu moja ya biblia inaruhusu kunywa pombe (divai/mvinyo) hata yesu anatengeneza divai kwa muujiza; sehemu nyingine inakataza watu kunywa pombe. Vile vile biblia hiyo hiyo inaruhusu watu kuoa wake wengi huku sehemu nyingine inataka mtu kuoa mke mmoja n.k.

Jambo jingine lenye utata zaidi pia ni hoja ya kwamba baraza moja lililoandika biblia ya vitabu 66 lilivuviwa na Roho Mtakatifu, je kuna uhakika na ushahidi gani kuwa baraza jingine ambalo liliandika biblia ya vitabu 73 nalo halikuvuviwa na Roho Mtakatifu na hata hilo baraza jingine lililoandika biblia ya nyongeza ya Church of Jesus Christ of Later Saints kwamba nalo halikuvuviwa na huyo huyo Roho Mtakatifu?

Vile vile kuna utata kuhusu uzito wa dhambi kana kwamba dhambi zote zina uzito sawa au zina uzito tofauti. Mfano katika biblia tunaona ikiandikwa kuwa kuna dhambi za mauti na dhambi nyinginezo (Kitabu cha waraka wa Yakobo/Yohana). Lakini watumishi wengine huzungumzia kuwa dhambi zote ni sawa. Hivyo kuleta maswali mengi kuhusu hukumu anayostahili mtu mfano aliyeua binadamu mwenzake na aliyeiba kwa mfano sindano au kuku, je wapewe hukumu na adhabu sawa? Tunaona hata katika torati adhabu zinaendana na uzito wa kosa/dhambi. Ndipo falsafa ya hell(Jehanamu), purgatory (toharani), na paradise (Heaven) [Mbinguni] inakuja. Na kwa kuzingatia kuwa Mungu ni mtakatifu na mwenye haki lazima aonekane kutenda haki kuliko mwanadamu ambaye ni mwenye dhambi. N.K.

Hii Ibada ya kuombea wafu, naona Utingo ameelezea kwa uzuri, Ukiliangalia hili andiko la Waebrania linasema baada ya kufa ni hukumu, sasa hii ya kuombea wafu ili kuwaondolea dhambi sijui imekaaje

Waebrania 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
 
Mtu akishakufa amekufa na aendi popote wala hafanyi lolote wala hawazi chochote ni kama mshumaa ukiisha umeisha so hakuna sababu yakuabudu au kuwaombea marehemu wao wameshamaliza kazi zao hapa duniani kilicho naki ni sisi kumuomba mungu na kujitengenezea njia nzuri kwa Yehova
 
Tatizo Biblia yenyewe haiko 'consistent' na inajipinga katika baadhi ya mambo na hivyo kuleta utata katika mambo hayo. Jambo moja linaweza kuonyeshwa kuwa linakubaliwa katika kitabu au mstari mmoja wa Biblia hali jambo hilo hilo linakataliwa katika kitabu au mstari mwingine wa Biblia. Kwa hiyo siyo vema kushikilia mstari mmoja wa Biblia au kusikiliza mchungaji mmoja anayesimamia baadhi tu ya mistari, bali ni muhimu kuangalia na kutathmini Biblia yote kwa undani kuhusu jambo unalotaka kulielewa lakini vilevile kuangalia muktadha (context) wa uandishi wa kitabu husika au mstari husika wa biblia.
Hii nakataa Biblia haijipingi, ila inatokana na jinsi gani ya watu wanavyofasiri maandiko na uelewa wa maandiko... Biblia haijipingi... labda ulete maandiko yanayojipinga halafu tujadili tuone kama ni kweli...

Kuwepo kwa Biblia mbili au tuseme tatu, yaani moja yenye vitabu 66 ambayo inakubaliwa na kutumiwa na makanisa ya kiprotestanti na ya kipentekoste na ile yenye vitabu 73 inayokubaliwa na kutumiwa na katoliki ni tatizo mojawapo la msingi. Lakini vile vile biblia ya ziada iliyoandikwa kutokana na vitabu vilivyokusanywa na kuandikwa kutokana na maandiko mbalimbali ya wafuasi wa Yesu ambayo yaliachwa nje ya biblia za mwanzo inayotumiwa na kanisa la Yesu la watakatifu wa baadae (The Church of Jesus Christ of Later Saints) ni tatizo jingine. Ndani ya biblia yenyewe kuna mambo yenye utata mfano kuhusu kama kunywa pombe ni dhambi au la - sehemu moja ya biblia inaruhusu kunywa pombe (divai/mvinyo) hata yesu anatengeneza divai kwa muujiza; sehemu nyingine inakataza watu kunywa pombe. Vile vile biblia hiyo hiyo inaruhusu watu kuoa wake wengi huku sehemu nyingine inataka mtu kuoa mke mmoja n.k.
kwanza hayo maelezo yako unatakiwa uelewe Biblia ni nini!? Unatakiwa uelewe ni kwanini vitabu vya Aprokifa havikuwekwa, Halafu na kina nani walioandika Biblia kama unavyosema... lakini naona Utingo amejitahidi kuelezea lakini sijui haujasoma maelezo yake...

Hapo nilipoweka red, Unaanza kuongelea habari za Joseph Smith nabii wa Wamormons kanisa lake alilolianzisha mwaka 1827, kwa kifupi unaanza kuingiza imani za ajabu, tunapokuja katika neno la Mungu inabidi tuangalie neno linasemaje na sio kuanza kuingiza mafundisho ya watu, msingi wetu ni neno la Mungu... ukweli huwa una njia yake, na sio kubuni vitu na kuanza kuvisapoti kuvitengenezea njia...

Yohana 8:32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

Hapo nilipoweka blue ni kama nilivyosema mwanzo ni namna gani ya kuelewa scripture... kwa hiyo bado kuna shida hapo

Hapo nilipoweka purple, Labda ungeleta maandiko hapa tunaruhusiwa kuoa wake wengi hapa mke mmoja ndio tunaweza tukajadili, lakini vinginevyo naona ni mafundisho ya watu tu, kama kina Joseph Smith...

Jambo jingine lenye utata zaidi pia ni hoja ya kwamba baraza moja lililoandika biblia ya vitabu 66 lilivuviwa na Roho Mtakatifu, je kuna uhakika na ushahidi gani kuwa baraza jingine ambalo liliandika biblia ya vitabu 73 nalo halikuvuviwa na Roho Mtakatifu na hata hilo baraza jingine lililoandika biblia ya nyongeza ya Church of Jesus Christ of Later Saints kwamba nalo halikuvuviwa na huyo huyo Roho Mtakatifu?
Nani alikwambia baraza limeandika vitabu vya kwenye Biblia!? huoni kama unachokisema sio kweli!? sidhani hata kama unajua unachokizungumza... Yaani na mafundisho ya Wa Mormons unataka yafuatwe na watu, chukua hii verse inavyosema...

2 Timotheo 3:16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

Vile vile kuna utata kuhusu uzito wa dhambi kana kwamba dhambi zote zina uzito sawa au zina uzito tofauti. Mfano katika biblia tunaona ikiandikwa kuwa kuna dhambi za mauti na dhambi nyinginezo (Kitabu cha waraka wa Yakobo/Yohana). Lakini watumishi wengine huzungumzia kuwa dhambi zote ni sawa. Hivyo kuleta maswali mengi kuhusu hukumu anayostahili mtu mfano aliyeua binadamu mwenzake na aliyeiba kwa mfano sindano au kuku, je wapewe hukumu na adhabu sawa? Tunaona hata katika torati adhabu zinaendana na uzito wa kosa/dhambi. Ndipo falsafa ya hell(Jehanamu), purgatory (toharani), na paradise (Heaven) [Mbinguni] inakuja. Na kwa kuzingatia kuwa Mungu ni mtakatifu na mwenye haki lazima aonekane kutenda haki kuliko mwanadamu ambaye ni mwenye dhambi. N.K.
Labda nikuulize swali, tunaishi kipindi cha torati au!? nani alikwambi kuna dhambi kubwa na dhambi ndogo!?

Warumi 5:20 Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;

Warumi 3:20 kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.

Warumi 6:14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.
 
Last edited by a moderator:
Najua hivyo mkuu lkn waengine wanafikiri tuliondoa vitabu anyway nashukuru kwa somo zuri lbd litasaidia wengine kuelewa . Mkuu hapo juu nimeomba maelezo kuhusu petro alipomuona elia na musa na kusema na tujenge vibanda vitatu. Kama tunasema hakuna uhusiano wa walio hai na waliolala je ni kwanini hawa walionekana. Naamini kwa uelewa wako waweza kulielezea hili vema na kulilinganisha na mada iliyopo mezani. Tafadhali naomba utupe darasa.
Hapo nilipoweka red, Hivi Eliya Mtishbi pamoja na Musa unawafanisha na wafu wengine!? kwani Musa na Eliya wapo wapi kwa sasa!? Na ni nani aliyemzika Musa!? kwani Eliya alikufa!?

Yuda 1:9 Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee

Kumbukumbu la Torati 34:5-6

5 Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la Bwana.
6 Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo.
 
Mtu akishakufa amekufa na aendi popote wala hafanyi lolote wala hawazi chochote ni kama mshumaa ukiisha umeisha so hakuna sababu yakuabudu au kuwaombea marehemu wao wameshamaliza kazi zao hapa duniani kilicho naki ni sisi kumuomba mungu na kujitengenezea njia nzuri kwa Yehova

You mean lile cadaver au soul? Una uhakika kuwa wamemaliza kazi zao hapa duniani maana najua majority uwa wanaondoka huku bado wana mipango milioni na zaidi na hii dunia
 
Ntuzu
Shukraan mno kwa ulizo jema ambalo lamfaa mwenye kujibu awe na maelezo ya kina na si aelewavyo yeye.

Kama litajibiwa basi nami ntakuwa mefarsika kutia langu ulizo.

Ahsanta nipo kipembeni hapa.

Mitume walifia dini yao hivyo ni watakatifu moja kwa moja.
 
Pole sana....rudi usome upya historia ya kanisa na tafuta kuhusu mkutano wa Nicea (425 AD kama sijakosea) enzi za Constantine (aliyeanzisha rosali ndani ya kanisa), ndipo utajua nani aliviondoa na ujue kuwa wakati huo kanisa lilikuwa moja tu. Wa kwanza kujitoa alikuwa Martin Luther (miaka ya 1500) kwa hiyo kusema si kanisa katoliki waliotoa nakusamehe bure, pengine hujui, make a research. Mkutano wa Nicea ndiyo uliweka msingi mkubwa wa imani ya ukristo kikanisa-katoliki ikiwa hujui (mwulize padri au mjuzi wa historia ya kanisa katoloki atakuthibitishia hili)

KITABU cha Yakobo kinahusu Neema....Mwanzoni Martin Luther hakuwa na uelewa kuhusu neema. Na ukisoma nyaraka (thesis) zake za baadaye anakiri kuwa alitaka kufanya kosa kubwa kwa sababu ya kutomwacha Roho Mtakatiifu kumfundisha hapo mwanzo kwa kukipuuzia kitabu hiki na katika vitu ambavyo anakiri kuwa mwanzoni vilimtatizo ni neema na hakutaka kuondoa kitabu hicho tu hata kitabu cha Warumi na vingine vinavyosisitiza neema/grace. Na mwishowe anakiri kuwa Kitabu cha Yakobo ni mojawapo ya backborne za NT kwa sababu kila mtu anaokolewa kwa neema. (SIYO MAOMBI YA WAFU KAMA ULIVYOAMINISHWA NA WAPAGANI WALIOLITEKA KANISA). SO is Ufunuo, mwanzoni Luther hakuwa na ufahamu kuhusu Eschatology na hiyo mpaka sasa mapadre wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusu eschatology hata sasa.

Usijaribu kuleta mjadala tuanze kujadiliana "if"

Na elewa kuwa huu mjadala si vita ya kidini.

Hivyo vitabu vya deutrocanony ulishavisoma? vitafute uvisome kwanza ndipo utajua ni kwa nini viliondolewa na ni kwa vipi vinaweza kummislead mtu asipokuwa mwangalifu. Ni vitabu vya historia tu za vita na mapinduzi (coup) vya Israeli na watawala katika kipindi cha miaka 453 kati ya kitabu cha Malaki mpaka kuzaliwa Kristo (Mathew). Hata katika tanack havimo. vipo katika nyaraka za historia ya waisraeli kama vitabu vya Yosephas/josefus...na wengine.

Bado hujui historia ya Biblia. Waliovitoa vitabu hivyo ni wayahudi ktkt mtaguso wa Jamnia 100 AD, sababu vitabu hivyo vipo ktk lugha ya kiyunani tu.
 
Nimekua najiuliza ni kwa nini mala nyingi hasa mwisho wa mwaka utasikia watu wengi wanakimbia majumbani mwao hasa vijijini na lengo ni kwenda kuwaombea ndugu walioishatangulia kwa maana ya kufa.

Wanaenda mbali na kupeleka maombi yao juu ya maisha yanayowazunguka kwa hao waliokufa,ni kweli kuna maana yoyote au kuna ulazima wa kufanya hili?kama ni kweli MUNGU tunaemuabudu na kuamini kua yupo na ndiyo alietuumba anapata nafasi ipi iwapo tutafikia kupeleka shida zetu kwa wafu?

Swali lako lina sehemu mbili. Kuhusu kuombea wafu Yuda Mmakabayo alifanya hivyo ktk kitabu cha Pili cha Makabayo. Kuhusu kuwaomba wafu labda nijue imani yako juu ya watakatifu. Unaamini uwepo wao?
 
KITABU cha Yakobo kinahusu Neema....Mwanzoni Martin Luther hakuwa na uelewa kuhusu neema. Na ukisoma nyaraka (thesis) zake za baadaye anakiri kuwa alitaka kufanya kosa kubwa kwa sababu ya kutomwacha Roho Mtakatiifu kumfundisha hapo mwanzo kwa kukipuuzia kitabu hiki na katika vitu ambavyo anakiri kuwa mwanzoni vilimtatizo ni neema na hakutaka kuondoa kitabu hicho tu hata kitabu cha Warumi na vingine vinavyosisitiza neema/grace. Na mwishowe anakiri kuwa Kitabu cha Yakobo ni mojawapo ya backborne za NT kwa sababu kila mtu anaokolewa kwa neema..[/QUOTE]

Luther alitaku kuondoa kitabu hiki kwa vile kilipingana na fundisho lake la 'SOLA FIDEI'
 
Dah! Kumbe shida ni kubwa zaidi. Tafuta Biblia yenye vitabu 73 utakiona kitabu cha 2 Makabayo

Hiyo ni biblia ya wakatoliki na ukatoliki si ukristo ni uislamu unaoamini katika mungu mke kabla ya version ya pili ya uislamu amabayo vatican walimpa muhamad ili kuwatoa waarabu kwa kristo yesu.
 
Hiyo ni biblia ya wakatoliki na ukatoliki si ukristo ni uislamu unaoamini katika mungu mke kabla ya version ya pili ya uislamu amabayo vatican walimpa muhamad ili kuwatoa waarabu kwa kristo yesu.

Mswalie mtume weye! Kakudanganya nani hayo?
 
Mkuu, shida si madhehebu tu. Shida ni baadhi ya watu kuuogopa ukweli. Ibada za wafu ni upagani. watu wanaogopa kuacha mabaya wanayoyatenda wanategemea ibada za wafu kuwa zitawatoa motoni?......unless Mungu stops to be God ndipo nitaamini ibada za wafu. Kwangu ni sawa na uganga wa kienyeji ambapo unakwenda kumwomba mganga/mchawi akunyenyulie roho ya bibi au babu au ndugu wa karibu aliyekufa ili akukinge na mabaya.

Tuwe jasiri kuface mapungufu yetu, tulijue Neno la Mungu na tuishi katika kweli. Falsafa mfu za makanisa na madhehebu yetu zilizotungwa na watu kwa kuangalia na kuyapalilia mapungufu yao ambazo zinapishana na Maandiko hazitatusaidia chochote.

Waebrani 9:27.........Baada ya kifo ni hukumu. Au andiko hili linyofolewe litolewe kwenye Maandiko?

Mkuu, oanisha Waebr 9:27 na ukweli kuwa 'siku ya mwisho Yesu atawahukumu wazima na wafu' Mt 25: 31-33.
 
Mkuu kama kuna hukumu(God court) siku ya Mwisho: inamaana wako watakaoshinda kesi na wale watakaopaikana na hatia.? unaionaje hii?
Tuanze kujadili
Je kuna dhambi ya Ndogo na dhambi Kubwa. JE nini maan ya dhambi ya MAuti? Kwanini kuwe na dhambi ndogo na dhambi kubwa?
Mkuu nachotakakujua ni nini hasa lengo la dhambi ndogo na dhambi kubwa, ama dhambi ya mauti na isiyo ya mauti nini imlications zake in the afterlife?.
 
Back
Top Bottom