Kwa nini Urusi haina maendeleo makubwa. Je, Margaret Thatcher yupo sahihi ?

Kwa nini Urusi haina maendeleo makubwa. Je, Margaret Thatcher yupo sahihi ?

Mwenge na siasa za umax zilizoegemea kitu inaitwa ujamaa na kujitegemea
ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi.
 
Wapi nimesema Urusi masikini ?

Nachosema Rasilimali alizonazo Russia hakupaswa kuwa pale alipo.

Huu ni ukweli ukiwa na akili timamu utakili kuna jambo halipo sawa ndani ya Russia
Walipaswa wawe wapi?
 
Ni kweli Tanzania ni masikini wa kutupwa sijawahi kupinga hilo.

Hata maelezo ya hiyo video fupi yamegusia mfano wa nchi kama Tanzania na hali yake pamoja ya utitiri wa rasilimali iliyo nayo.

Kwani hutaki Urusi kujadiliwa ?
Labda kapata kibali toka JF mada zote tu check na yeye kwanza ndio tulete hapa.
 
Scandvian countries sijui kama ipo hata moja yenye mwenge.
Na ni nchi zinazoongoza kwa upendo na uzalendo wa raia kwa mataifa yao,tofauti na sisi tunauhubiri ujamaa
lakini tukipewa nafasi kutumikia umma,tunaishia kuiba na kuwekeza kwenye chi za kibepari.
 
Hakuna mahali nimesema Russia masikini.

Hivi unasoma kweli nacho andika ?

Nani hawamtaki Urusi ?

si hao wakubwa wa G20 , Mrusi anaangalia mahitaji ya raia wake, hospitali , elimu , makaazi na mahitaji ya lazima, ukija huko Marekani watu kwa maelfu wanalala barabarani wengine wakiambulia chakula cha kugaiwa na wengine wakijilimbikizia madeni yenye mariba wapate kuishi hayo ndiyo maisha ya west , tumeishi huko tunayajuwa
 
Kitendo cha urusi kupata msaada kutoka korea kaskazini ili kupigana na ukraine,
kwa mtu yeyote mwenye akili atajua ukubwa wa pua siyo wingi wa makamasi.
Naungana na huyo mama kusema urusi ni maskini.
 
Zaidi ya pombe ya Batlika, Vodka hakuna kitu cha mrusi Kariakoo, labda jeshini huko, mafuta hata Saudia yapo. Yaani kujimwambafai wamezidi kuliko hali halisi.
 
China,Marekani ni nchi ndogo ?
Top 10 largest countries in the world 2024
  • Argentina - 2,780,400km²
  • India - 3,287,263km²
  • Australia - 7,741,220km²
  • Brazil - 8,515,770km²
  • China - 9,596,960km²
  • The USA - 9,833,517km²
  • Canada - 9,984,670km²
  • Russia - 17,098,242km²
 
Attachments

Inawezekana, Russia ilipambana WW2 mwanzo mwisho, wakitumia fedha yao, na nguvu kazi yao, walipigana kiume na Hiller hadi wanaingia Germany wakitokea mashariki, huku magharibi wakiwa US, UK, France n.k....

Hivyo kuwa na heshima na shukuru kwa mchango wao.

UK yenyewe toka hio vita hadi leo hawajawahi recover, hio vita ilimnufaisha US.
 
Marekani, China na Urusi hazipo kwenye uzani na Urusi kimaendeleo makubwa ya kiuchumi.

Maendeleo gani unayo zungumzia
Nchi zote hizo 3 Usa/China/Urusi hazina Maendeleo sawa Nchi nzima, ni watu wachache wenye uchumi mkubwa ambao wanabeba nchi nzima, for this Case Usa na China wana matajiri wakubwa wengi kuliko Urusi.

China miji yake ya Baharini ina Gdp sawa na Nchi za ulaya madon wote Wakubwa wapo huko ila ukiingia Ndani kuna miji kama Africa tu kiuchumi, wanajitahidi kupeleka huko Maendeleo ila still nchi kubwa sana.

Usa Asilimia 50 ya population wanamiliki just 2.6% ya utajiri wa Usa. Tupige hesabu kidogo Gdp ya Usa ni dola Trilioni 27, asilimia 2.6 ni kama dola Bilioni 700, nusu ya watu Marekani ni Milioni 167 ukigawanya hapo roughly unapata dola 4200, So ukichukua Nusu ya Usa ya wasio nacho watu millioni 167 na kuwaleta Africa watakuwa hata hawapo Top 10 ya Nchi zenye kipato kikubwa cha mtu mmoja mmoja Africa.

Same kwa Urusi Moscow ni Bonge la mji sawa na Miji mingine ya Urusi Magharibi, ila Mashariki ni majanga in short Eneo lote la Urusi ambalo lipo Asia maendeleo ni madogo na Contribution yake pia ni ndogo sana kiuchumi.

Compare hizo Nchi 3 na nchi yoyote Ulaya iliyoendelea utofauti ni Mbingu na Ardhi.
 
Kitendo cha urusi kupata msaada kutoka korea kaskazini ili kupigana na ukraine,
kwa mtu yeyote mwenye akili atajua ukubwa wa pua siyo wingi wa makamasi.
Naungana na huyo mama kusema urusi ni maskini.
Vipi West walipoungana kuja kumpiga Gaddafi ina maana ni masikini na wao..

Operation desert storm nchini Iraq ilikuwa na msafara wa nchi EU yote wakiongozwa na US, je US pia alishindwa kuikabili Iraq pekee na kumuangusha Sadam Hussein? majibu tafadhali...
 
Nchi zote hizo 3 Usa/China/Urusi hazina Maendeleo sawa Nchi nzima, ni watu wachache wenye uchumi mkubwa ambao wanabeba nchi nzima, for this Case Usa na China wana matajiri wakubwa wengi kuliko Urusi.

China miji yake ya Baharini ina Gdp sawa na Nchi za ulaya madon wote Wakubwa wapo huko ila ukiingia Ndani kuna miji kama Africa tu kiuchumi, wanajitahidi kupeleka huko Maendeleo ila still nchi kubwa sana.

Usa Asilimia 50 ya population wanamiliki just 2.6% ya utajiri wa Usa. Tupige hesabu kidogo Gdp ya Usa ni dola Trilioni 27, asilimia 2.6 ni kama dola Bilioni 700, nusu ya watu Marekani ni Milioni 167 ukigawanya hapo roughly unapata dola 4200, So ukichukua Nusu ya Usa ya wasio nacho watu millioni 167 na kuwaleta Africa watakuwa hata hawapo Top 10 ya Nchi zenye kipato kikubwa cha mtu mmoja mmoja Africa.

Same kwa Urusi Moscow ni Bonge la mji sawa na Miji mingine ya Urusi Magharibi, ila Mashariki ni majanga in short Eneo lote la Urusi ambalo lipo Asia maendeleo ni madogo na Contribution yake pia ni ndogo sana kiuchumi.

Compare hizo Nchi 3 na nchi yoyote Ulaya iliyoendelea utofauti ni Mbingu na Ardhi.
Hapo la kumjibu ni moja tu, kwa sababu Russia sio mwizi anaye print dollar na kulazimisha nchi zenye mafuta kutumia dollar katika mauzo, US ina print dollar kama magazeti au vitabu....

Uchumi wa EU na US ni ujanja ujanja na wizi kitu ambacho Russia hawana.
 
Umesikiliza kilicho zungumzwa ?

Hakuna excuse yoyote ya kuitetea Urusi na utitiri wa rasilimali ilizonazo
Kwani ww ulitaka Urusi iweje ambapo ww unapataka.
Alafu kabla ya kuongea ulisha wahi kufika Urusi?
 
Back
Top Bottom