Kwa nini Waafrica hawatumii majina ya Kirusi

Kwa nini Waafrica hawatumii majina ya Kirusi

Maelezo meeengi lakini point ni moja tu. Afrika ni ombaomba. Hayo uliyotaja sijui uchumi kijamii n.k ni sababu ya upumbavu wa waafrika ndio maana mataifa yasiyokuwa na maslahi nasi tunayaona hayana influence kwasababu hawajazi mabakuli yetu
Sasa kwa nini Wasiwe ombaomba kwa Urusi?
 
Kwani katiba yetu inatamka Tanzania ni aina gani ya taifa? Kama tumetaja ujamaa basi tayari tumeshawishika na Mrusi.

Nadhani kilichomnyima nafasi ya kuwa na nafasi ni imani tulizoletewa zilitoka kwa wazungu na waarabu, ndio maana majina yao yametawala.
Katiba yetu haisemi kuwa ni nchi ya kijamaa, japo enzi za Nyerere lilikuwa limeegemea zaidi itikadi za kijamaa ila influences za kijamaa Nyerere alizipata zaidi China na sio Urusi
 
Yapo kuna

Tatiana

Natalie

Anastasia

Ivan

Nikolai
 
Sasa kwa nini Wasiwe ombaomba kwa Urusi?
Kwasababu Urusi hawezi kulea mitoto inayoishi kwa baba na mama na wakati huohuo hao wazazi hawataki kutekeleza wajibu wa malezi.

Hata huyo anayewapa misaada sio kwamba mnaenda tu mnakaa mezani mnaanza kukusanya pesa, yapo masharti ya mikopo ambayo ukiyasikia nadhani utatamani usingeyajua
 
mjuba unataka kusema hawa watoto wetu kina brown, brian, brayson, graceous, goodluck, mwajuma, mwanahamisi, ni majina ya israel na saudia? Mbona sijawahi kuona msaudia akiitwa mwajuma, au muisraeli akiitwa goodluck?
Hao akina Brown, Bryson.... madhara ya ukoloni na ni ukoloni mambo leo.
Akina Mwajuma ni asili ya kiarabu yaani mtoto wa kike aliyezaliwa Ijumaa. Ni athari za kutawaliliwa kitamaduni na kifikra na mwarabu.
Hoja hapo ni kuwa warumwa wa utamaduni wa wageni. Hiyo Israel na Saudi Arabia wawakilishi tu wa kundi la wakoloni wetu.
 
Kwa nini pamoja na umaarufu na ushawashi mkubwa wa Urusi kwa Africa kwa miongo mingi Waafrika bado hawatumii kabisa majina ya Warusi?
Kwanini wazungu hawatumii majina ya kiafrika.Mayalla,magufuli,mpina,mwamposa,Gwaji boy,kikwete,chikwidu,kipepe,Mpoto na mengineyo.
 
Kwasababu Urusi hawezi kulea mitoto inayoishi kwa baba na mama na wakati huohuo hao wazazi hawataki kutekeleza wajibu wa malezi.

Hata huyo anayewapa misaada sio kwamba mnaenda tu mnakaa mezani mnaanza kukusanya pesa, yapo masharti ya mikopo ambayo ukiyasikia nadhani utatamani usingeyajua
Urusi ambaye ni mtakatifu awape kwa masharti laini basi, mbona huko Burkina Faso anatoa msaada?
 
Katiba yetu haisemi kuwa ni nchi ya kijamaa, japo enzi za Nyerere lilikuwa limeegemea zaidi itikadi za kijamaa ila influences za kijamaa Nyerere alizipata zaidi China na sio Urusi
Asante kwa marekebisho kuhusu wapi itikadi ya ujamaa tuliipata. Lakini pia naomba ufahamu kuwa Katiba yetu imebainisha wazi kuwa sisi n wajamaa.

Sura ya kwanza, Ibara ya 3 kifungu cha 1 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) pamoja na mabadiliko yake yote.

Inatamka rasmi kuwa ni nchi ya Kidemokrasia na kijamaa, isiyo na dini na yenye mfumo wa vyana vingi.
 
Itikadi inayoongoza nchi inabadilika kutokana na wakati na aina ya utawala uliopo madarakani. Mimi sioni huo ujamaa wa Tanzania kwa mujibu wa itikadi na kanuni za kijamaa
 
Itikadi inayoongoza nchi inabadilika kutokana na wakati na aina ya utawala uliopo madarakani. Mimi sioni huo ujamaa wa Tanzania kwa mujibu wa itikadi na kanuni za kijama
Ujamaa wetu ulifeli siku nyingi, tulibaki na jina kwa kuhofia kulazimika kutamka rasmi Ubepari.
 
Kwa nini pamoja na umaarufu na ushawashi mkubwa wa Urusi kwa Africa kwa miongo mingi Waafrika bado hawatumii kabisa majina ya Warusi?
mbona sijasikia msukuma akiitwa masawe?
 
Back
Top Bottom