Kwa nini watu wa mikoa ya Mara na Kilimanjaro wanapenda sana kufuatilia siasa za Kenya?

Kwa nini watu wa mikoa ya Mara na Kilimanjaro wanapenda sana kufuatilia siasa za Kenya?

Umetishaaaa
Unakumbuka Radio citizen kipindi cha Christmas? Kulikua na kampen flan iv yenye vibe sanaaa inaitwa Patapata.
Jpili ilikua naskilizaga sana Je huu ni ungwana?
Mpira nilikua naskiliza Radio jambo zaid(nilikua naskilizia Citizen before🤣)
Mzaz Willy Tuva je?😄😄

Station za bongo zilikua almost amna
Mimi nilkiwa mdogo nilikuwa siijui hata Tanzania
Maana radio ,TV za TV zilikuwa kwetu hazishuki
Niliumia Sana siku nilijua Mimi mtz
 
Nimeishi mikoa yote hiyo hapo juu,nimeona idadi kubwa ya watu wa huko wanapenda sana kufuatilia siasa za kenya.

Yani ukiwa mara au kilimanjaro radio station nyingi zinazosikilizwa huko ni za kenya,TV station zinazotazamwa sana ni za kenya.watu wa huko wana details nyingi sana kuhusu nchi ya kenya.huenda mtu akawa anamjua waziri wa elimu wa kenya lkn asimjue waziri wa elimu wa Tanzania.

Je ni sababu gani inayowafanya watu wa hiyo mikoa kuwa na interest na mambo ya kenya kuliko hata ya Tanzania?
Kwasababu wapo mipakani na nchi ya Kenya na wengine wanakua na ndugu huko
 
Mimi nilikuwa Holili pale 2009 nilikuwa nasikiliza zaidi radio Cetizen, vyombo vya habari vya Kenya vina uhuru sana walikuwa wanajadili issue ya William Ruto kufanya ufisadi wa mahindi ya msaada kama sijakosea alikuwa waziri wa Kilimo na wananchi wanachangia kweli kweli.

Pia miaka ya 2000 Jumapili nilikuwa nasikiliza kupindi cha jee huu ni Ungwana cha Leonard Mambombotela nikiwa kwetu Marangu. Bora mkoa wetu ungekuwa Kenya tu kwa sababu hata lugha yetu na Wataita Taveta tunaelewana kiasi fulani.

Wazee wetu wengi waliishi Mombasa na tuna ndugu waliozaliwa huko maeneo ya Likoni, Kisauni na kadhalika.
 
Redio.za Tanzania ni michezo asubuhi umbea na muziki mchana jion michezo ,usiku mapenzi.siku imeisha
Kuna vipindi vile baada ya michezo ya asubuhi wale wanaongea kama mashog. Kina kumbuka mambo ya uswazi. Yaani vinakera hadi baasi
 
Tarakea nimekaa sehemu moja inaitwa mashati kama sijakosea, aisee pombe zitawauaaaa chalii
Hapana umekosea rombo Kuna Tarakea, usseri, mashati, mkuu na mengwe

👉 Ni kweli Kuna pombe ya asili mbege safi

👉Lakini pia Kuna viwanda vinavyotengeneza pombe zitokanazo na ndizi kama banana ya Arusha, Kuna kimorali, kiboboswa n.k

👉 Unakuta wengi wanakunywa hizi pombe kama kimorali plus chang'aa kwa wingi mpk kupitiliza huku hawali chakula wakashiba matokeo yake ni htr kwa afya!

👉Chupa ya kimorali Tzs 500 bohora/chibuku ya mbege ni 700-1000 kwahiyo mtu anakimbilia cheap bila kujua huko ndo anaharibu. Mwili wake,
 
Mfano mimi nafahamu siasa za kenya kuliko tz
Kila siku lazima nitazame morning break ya citizens tv au capitalfm
 
Back
Top Bottom