Uchaguzi 2020 Kwa press hii, Polepole anakivuruga chama, atafutwe mtu mwingine wa kufanya press

Uchaguzi 2020 Kwa press hii, Polepole anakivuruga chama, atafutwe mtu mwingine wa kufanya press

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Uchaguzi na propaganda ukaa pamoja siku zote. Lakini propaganda zisivyopangiliwa vyema zinaweza kuwa mwiba kwa anayesimuliwa.

CCM fanyeni maamuzi magumu, kubalini kuwa Polepole amepwaya kwenye hiyo nafasi, kubalini kuwa ni kipindi Cha kutafuta wabobezi waingie kazini si kuruhusu watu kama Polepole kukitetea chama.

Hoja ya uwanja wa Chato haijibiki hata Kama utakodi magwiji wa siasa Duniani, tukubali tulikosea.

Hoja ya ununuzi wa ndege za biashara haina majibu, tukubali tulikosea. Ndege ni kitu chema ila tulikosea kuingia kwenye usiri wakati tunachonunua siyo ndege za jeshi, ni za biashara. Lazima tukubali kuwa usiri uliowekwa utaliua shirika maana akija Rais mwingine hatokubali kuendelea na huo usiri bali ataamua kuweka wazi usiri uliopo au kuachana na biashara hii kama awamu ya tano ilivyoachana na miradi iliyokosewa na awamu ya nne.

Mradi wa reli ni janga kubwa pia hasa pale ambapo kuna sintofahamu kuhusu chanzo cha fedha na upatikanaji wa wakandarasi.

Kinachoiumiza awamu ya tano siyo uthubutu wa kutenda, kinachoiumiza awamu ya tano ni USIRI KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA WANANCHI.

Wanachosimamia upinzani ni dhana ya mali ya umma ambapo kimsingi kabisa mali ya umma hupangwa na kuliwa na umma. Mipango hiyo hupangwa kupitia Bunge na hukaguliwa kupitia CAG na pale inapoibuka ubadhirifu maamuzi hutolewa na mahakama.

Polepole USIRI WA MATUMIZI YA UMMA HAUNA PROPAGANDA UNAHITAJI FACT
 
'Endereeeeeni kutuamini ndg wananchi,ahadi zetu zote tumezitekerezaaaaaa'.
Screenshot_2020-09-24-19-55-15-1.jpg
 
Hivi kweli chama changu ccm mnamtuma polepole awawakilishe kujibu tuhuma? Hamko serious

Sijaona cha maana alichozungumza mnazidi kuwadhalilisha waandishi wa habari
Nimekubali kweli huu ujinga uyumsemaji wa chama cha jiwe anaudhunisha kweli
 
Back
Top Bottom