Uchaguzi 2020 Kwa press hii, Polepole anakivuruga chama, atafutwe mtu mwingine wa kufanya press

Uchaguzi 2020 Kwa press hii, Polepole anakivuruga chama, atafutwe mtu mwingine wa kufanya press

Mobutu ni Mobutu na Tanzania ni Tanzania.

Jana Pole Pole kaziweka wazi kumbukumbu za bunge kuidhinisha ujenzi wa uwanja wa ndege.

Kama Mobutu kiwanja alichojenga huko kwao hakikuidhinishwa na bunge lao hilo ni tatizo lao.
Historia ni mwalim mzur tusiipuuze
 
Kwani ni nani alileta msemo: "Ukinunua kitu dai Risiti, ukiuza kitu toa Risiti?" Kutokana na maneno haya ya Magufuli, watu wakinunua chochote wanadai Risiti na kuhifadhi mahali salama hata panya asiguse lakini ikihitajiwa na yeyote inafukuliwa aonyeshwe maana siyo siri. Wananchi kwa wakati tofauti wamehoji manunuzi fulanifulani ya Serikali ikiwa ni pamoja na yanayofanywa na Rais lakini wamekuwa hawapati majibu kabisa na kujiona kama wanapuuzwa au kuna kitu kinafichwa. Polepole yuko karibu na Mwenyekiti wa Chama na anaweza kumjibia hoja fulanifulani siyo zote lakini yuko mbali sana Rais kwa hiyo siyo jukumu lake kabisa kujibu hoja au tuhuma zote zinazomhusu Rais au Serikali yake maana kuna watu wa kazi hiyo hata ni vizuri zaidi akijibu mwenyewe. Rais anatakiwa awe mfano mzuri kwa mambo mengi bahati mbaya sana maneno yake mwenyewe ya mara kwa mara yanafanya wengi hata wanamdharau na kutomwamini. Miradi inayotajwa na mleta comment haikutekelezwa na Awamu hii yenye usiri mkubwa kwa mengi hadi kufanya watu wahoji au kuwa na wasiwasi na weledi wa kiongozi wa sasa kutokana na anavyozunguka na mabulungutu ya fedha akiwagawia maswaiba wake.
Rubbish!
 
Back
Top Bottom