Kama viwanja vya karibu vinaweza kufanya kazi ambayo inatakiwa kufanywa na uwanja wa ndege wa Chato kuna umuhimu gani kutumia mabilioni ya walipa kodi kujenga uwanja kijijini kwa Rais?Umeshaelezwa kwa kirefu ni kwanini uwanja wa Chato ni muhimu kwa uwanja wa Mwanza, hakuna aliyesema viwanja vya Shinyanga na Musoma sio muhimu kumbuka kuwa viwanja vyote vya ndege vinakarabatiwa kwa ujumla.
Hayo ya mume mwenza kupewa tenda ni story ulizosikia kwa watu ambazo huwezi kuuweka wazi ushahidi.
Mkuu yanafanyika mengi sana ya kimaendeleo uwanja wa Chato ni sehemu ndogo sana.
Ameshutumiwa Rais kumpa tenda hiyo mume mwenza, kama ya vitambulisho amejibu, ya majimbo amejibu ya kujenga uwanja nyumbani kwake amejibu, kwa nini hii hakanushi kama haina ukweli? Hujioni una mapungufu kichwani mwako kulazimisha nyeupe ionekane nyeusi?
Msemaji mkuu wa serikali hawezi kujibu, Polepole hawezi kujibu, ila wewe unalazimisha kututia ujinga, huna kazi ya kufanya zaidi ya kutetea yasiyoteteka?