Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!

Kama wanavyohangaika kina kinana na chogolo kutetea mkataba. Hii halijawahi kutokea.
Wanachotembeza Ni kibovu, hakinunuliki. Ni Kama pweza aliyechina.

Ulichokiandika ni ukweli.

Yaani wana CCM na wafanyakazi serikalini wanalazimishwa kwenda kupigia kampeni ugawaji wa maliasili za Taifa.

Haijawahi kutokea tangu kuzaliwa kwa Tanzania!
 
Rais wa mpito ndivyo walivyo

Nadhani kuweka wote katika kapu moja ni kukosea. Kuna Marais wengine wa mpito ambao huijua vizuri kazi yao na mazingira yake ambapo hupelekea kufanikiwa.

Rais Samia hana hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi!
 
Mzee #Kinana anasema “wabunge wetu wanalipwa pesa kidogo sana”[emoji848][emoji848][emoji27][emoji27][emoji3596]

MISHAHARA YA WABUNGE NI WIZI NA UNYANG'ANYI WA HALI YA JUU KABISA TANZANIA.

Suala la Mishahara ya Wabunge analoliongea @HecheJohn linaumiza roho sana.

Mwalimu wa Tanzania mwenye TGTS D1 mwenye mshahara take home 531,000 kwa mwezi, akifanya kazi kwa miaka 38 atalipwa shilingi 242,136,000 (milioni 242).

MBUNGE wa Tanzania kwa mwaka mmoja analipwa shilingi 240,300,000 (milioni 240 bila posho za kamati).

Yani mwalimu wa Tanzania mwenye degree analazimika kufanya kazi kwa miaka 38 ili aweze kupata malipo anayopewa mbunge wake (ANAYETAKIWA KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA TU) kwa mwaka mmoja tu. Ndio uzalendo huu?????? @SuluhuSamia

YANI IPO HIVI,
Mbunge anayelala tu bungeni @bunge_tz analipwa;

Posho za vikao kwa mwaka ni sh. 42,300,000 (milioni 42.3)
Mshahara na marupurupu kila mwezi 16,500,000 × miezi 12 = 198,000,000 (milioni 198).
Jumla kwa mwaka mmoja ni sh. 240,300,000 (milioni 240, hii haihusishi posho za kamati za kudumu).

Kwa miaka mitano, mbunge wa Tanzania analipwa 1,201,500,000 (Bilioni moja na milioni 200) bila kuhusisha posho za kamati.

TUCHANGANUE MALIPO YA MBUNGE VIZURI.

Sitting Allowance - 220,000
Per Diem - 250,000
Jumla kila siku mbunge analipwa 470,000/= (haijalishi ameongea au lah).
Mshahara na marupurupu kwa mwezi - 16,500,000/=

Mshahara wa mbunge kwa mwaka mmoja ni shilingi 198,000,000 (milioni 198).
Mshahara wa mbunge kwa miaka mitano ni shilingi 990,000,000 (milioni 990).
Bado kila baada ya miaka mitano huyu mbunge analipwa kiinua mgongo milioni Mia mbili (200,000,000).

Vikao vya Bunge

Kikao cha Januari 31 - Feb 10 = siku 11
Kikao cha bajeti April 4 - June 30 = siku za vikao 59
Mkutano wa tisa wa bunge mwaka 2022 Nov 1-11 = siku 10
Mkutano wa nane kuanzia Sept 13-23 = siku 10
Jumla ya siku za vikao vya bunge ni siku 90.

Siku 90 za vikao × 470,000 = 42,300,000
42,300,000 za vikao × miaka 5 = 211,500,000

JUMLA KWA MIAKA MITANO
1,201,500,000 (Bilioni moja na milioni 200) bila kuhusisha posho za kamati.

TUANGALIE MSHAHARA WA MWALIMU KWA MIAKA MITANO

Mwl. mwenye TGTS D1 mshahara wake basic ni shilingi 771,000 kwa mwezi, ukitoa makato, take home ya mwalimu huyu no shilingi 531,000.

Mshahara wa huyu mwalimu kwa mwaka 531,000 × miezi 12 = 6,372,000 mara miaka mitano = 31,860,000 (huu ni mshahara wa Mia I miwili wa mbunge).

Kwa miaka 38 mwalimu analipwa 6,372,000 * 38 = 242,136,000 (sawa na mshahara wa mwaka mmoja wa mbunge).

Huyu mwalimu akidai nyongeza ya mshahara anaambiwa "KUWA MZALENDO." Kama sio wizi huu ni nini????

Wakati mbunge wa Tanzania anaogelea kwenye bwawa la utajiri wa kodi za walala hoi, mtoto wa mtanzania maskini anashindwa kujengewa hata choo cha tundu kwenye shule yake; hata dawati la shilingi elfu 50 tu limeshindikana; hata kitabu cha elfu kumi tu imeshindikana.

IFIKE MAHALI TUACHE HUU UFALA WA KUENDELEA KUFUMBIA MACHO UDHALIMU WAKATI TUNAOUMIA NI SISI NA WATOTO WETU. MABADILIKO YA KWELI YATAKUJA PALE WATU WA CHINI TUTAKAPOSIMAMA KUPINGA UDHALIMU.
 
umeandika ukweli, nimethibitisha leo hapa mwanza. ccm inakufa kifo kibaya sana. wanaoisemea hawana uwezo wowote, wala ushawishi kabsa

Eti Mzee Wassira ndiye “kinara” kitaifa ndani ya CCM kwa sasa!

Yaani CCM wana hali mbaya sana!
 
Sukuma gang unahangaika sana. Vipi ule uzi wako kuhusu miga?
 

Mkuu, mimi nipo na shukrani kwa andiko lako.

Tuzidi kukubali kutokubaliana juu ya Marehemu Magufuli.

Sikuwahi “kumpelekesha” Magu bali niliyokuwa yanaandika na kuyafanya yaliangazia picha kwa ukubwa wake.

Nakubali Magu alikuwa na mapungufu yake kama binadamu lakini hakuwahi kutiliwa shaka kuhusu ulinzi wa maliasili zetu.

Ni kweli kuna mengine hasi yanayotokea kwa sasa nchini ni chimbuko la alichokifanya.
 
Mama anakipeleka chama kubaya Kama JK 2010, namwangalia Kinana anavyoongea kama amekata tamaa Ila hana jinsi ndio ameachiwa jukumu hilo huku mwenyekiti wake akienda kubarizi Dubai na Saudia

Huu ni mwaka wa pili kwa serikali ya Rais Samia wameishachoka!
 
Natamani jamii forum wangeruhusu kudownload uzi ili huu niupitie kila muda kuikumbusha akili yangu kuwa taifa limepata kiongozi wa hovyo kuwahi kutokea

Mkuu, unaweza kupakua kama una apps za kupakua bila kujali kama Jamiiforums hawaruhusu.
 
Hao ni wapuuzi wanajifariji tuu ila wasisahau tunawakumbusha tuu
 
Ulichokiandika ni ukweli.

Yaani wana CCM na wafanyakazi serikalini wanalazimishwa kwenda kupigia kampeni ugawaji wa maliasili za Taifa.

Haijawahi kutokea tangu kuzaliwa kwa Tanzania!
Hiyo gia haiwezi kuwavusha hamna ajenda mtaishia kuliwa vichwa na kula hasara kama kawaida yenu
 
Haihitaji kusubiria 2025, mwakani hapo Kuna uchaguzi wa Serikali za mitaa Chadema mtapata majibu yenu
 
Aliyevujisha mkataba huu wa Kimangungo ahesabiwe shujaa wa Taifa, vinginevyo tungeujua wakati tayari utumwa wa Waarabu ulishajikita. Shujaa huyu abarikiwe sana.
 
Sasa kwanini kila siku kutwa kutukana mimatusi humu,ukubwa Jalala,kwanini wewe unashindwaga kutoa maoni yako kwa lugha za kiungwana,heshima na staha.? Kwani ni vipi matusi yako unayotoagaa yanaongeza uzito wa hoja zako?
Wewe ni zero kabisa, maoni yako kila siku ni mashudu.
 
CCM hawategemei sanduku la kura, sanduku lao la kura ni TISS na Polisi.



Yanamwisho hayo!

Itafika mahala Mwenyezi Mungu atazidi kuchukizwa na kuamua kuingilia kati kuwavuruga na kufanya atakavyo ktk kuhakikisha haki za wananchi zinapatikana.
 

Hakika ukiukubali ukweli utakufanya uwe huru!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…