Acha uongo wako hapa na upotoshaji wako hapa wa kijinga.
Rais samia anakubalika ,kupendwa na kuungwa mkono na watanzania wa makundi yote kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ndani ya muda mfupi wa uongozi wake.
Katika kugusa maisha ya wananchi wa kipato cha chini ambao wengi wao ni wakulima ,Rais samia aliamua kuchukua hatua za makusudi na za kijasiri kwa kuhakikisha kuwa anawapatia mbolea za Ruzuku zinazogharimu Takribani Billion mia moja hamsini ,hali iliyopelekea mbolea kushuka bei sokoni,,mfano mbolea ya DAP iliyokuwa ikiuzwa laki na 40 ikaanza kupatikana kwa Elfu 70 tu,.sasa ni mkulima yupi au mwananchi yupi atakaye shindwa kumshukuru Rais samia hasa kwa kuzingatia asilimia kubwa ni wakulima? Alifanya hivi kwa kutambua ukweli kuwa uchumi mzuri ni ule unaowagusa watu wengi ,na hapa Tanzania ili uwaguse watu wengi nisharti uwekeze katika shughuli za kilimo kama alivyofanya rais samia ,ikiwepo kuongeza bajeti kufikia billion 970.
Ukija kwa vijana nako ni kicheko furaha na Tabasamu ,hasa baada ya kumwaga maelfu ya ajira mitaani katika ndani ya muda mfupi,lakini pia miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikijengwa hapa nchini imechochea ajira nyingi sana kupatikana kwa vijana,lakini pia kwa vijana wanaomaliza kidato cha sita wanapewa mikopo bila shida ,na wawapo vyuoni ni raha tupu na Tabasamu hasa baada ya kuongeza fedha ya kujikimu kufikia elfu kumi kwa siku.
Ukienda kwa wafanyabishara nako ni matumaini kibao ,ambapo kwa sasa kila mfanyabiashara anajisikia fahari kufanyia biashara hapa nchini,kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya biashara hapa nchini,sasa wafanyabishara wanakadiriwa mapato kwa haki na palipo na dosari milango ipo wazi kwa mazungumzo,hali hii ndio imepelekea mapato kwa mwezi kupanda kufikia Trioni 2. Wafanyabishara kwa sasa wanajiona huru kuweka fedha zao benki bila wasiwasi wa kuchotewa fedha zao bila utaratibu wa kisheria au kibenki.
Ukija kwa watumishi wa umma unakuta nako ni shangwe ,nderemo na vifijo hasa baada ya mama wa shoka kuwapandishia mishahara kwa 23% hasa wa kima cha chini,kuwapandisha madaraja,kuwapa nyongeza ya mishahara ya kila mwaka,kuwalipa malimbikizo ya madeni yao na maboresho mengine mengi tu.
Sasa ukitaka kufungua hata biashara katika mwaka wako wa kwanza husumbuliwi na ulipaji wa mapato,kwa kuwa serikali imetoa nafasi ya kukuwa kimtaji na kupata uzoefu wa biashara na kusimama kibiashara.
Ukienda katika huduma za kijamii unakuta Rais samia amegusa kila eneo na kila mahali,iwe ni katika miradi ya maji au umeme au miundombinu una ona namna alivyowekeza vya kutosha ,ndio maana imefika hatua bwawa la nyerere linaanza mapema mwakani kuzalisha umeme.
Ni kundi lipi ambalo halijaguswa na utendaji wa Rais samia? Lipi ambalo halijafikiwa? Lipi ambalo halijatazamwa?
Masuala ya Tozo, je nchi gani ya ulaya au Marekani au zilizoendelea zilizopata maendeleo yake kwa kushushwa kutoka angani? Ni wapi ambako watu wake hawakujibana bana kulipa Tozo ili wajenge nchi zao? Ni wapi huko ambako mataifa yao na wananchi wao walikaa na kubweteka kusubiri wenzao kutoka mataifa mengine walipe Tozo na kodi ili wao wapewe maendeleo.
Watanzania hawajawahi kupinga Tozo na wakati wote wameunga mpango huo wa serikali,ndio maana walikuwa Tayari kuijenga nchi yetu kwa mikono yao ,maana waliona ni aibu kusubiri misaada kwa ajili ya kujengea matundu ya vyoo vya wanafunzi wetu mashuleni. Matokeo chanya ya Tozo hizo ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya Elfu ishirini nchini kwote yaliyopelekea wanafunzi wote wanaofaulu kuanza masomo kwa wakati mmoja, utolewaji wa Elimu bure hadi kidato cha sita,Ujenzi wa vituo vya Afya kila kona ya nchi ikiwepo 234 miezi michache iliyopita ,utolewaji wa Ruzuku ya billion mia moja kila mwezi katika mafuta wakati wa mfumuko wa bei ya mafuta Duniani uliokuwa umesababishwa na vita vya ukrein, n.k.
Mambo aliyoyafanya Rais samia huwezi kumaliza kuandika hapa maana ni mengi sana ,hapo sijazungumzia namna alivyokuza uchumi wetu na kupelekea mzunguko mzuri wa fedha mitaani,kukuza na kuimarisha Demokrasia n.k