Swala si kizazi ni mtu kuingia mkataba mbovu. Nashangaa watu kila mara wanadai kizazi. Lakini kiukweli kizazi kilichopita ndo kulikuwa na misimamo haswa. Kumbuka Bunge lilivyokuwa moto enzi hata za chama kimoja.
Wabunge bila kuogopa walisimama na kudai Tanganyika. Leo watathubutu?
Wakati Loliondo inauzwa Waandishi wa habari kama akina Katabaro, Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema, alisimamia swala na kuandika ukweli hadi akauwawa kwa mazingira ya ajabu pale ofisini kwake mitaa ya mnazi mmoja.
Leo waandishi waandishi wanaotumia digital ndo kwanza wanausifia mkataba. Waandishi wa habari wamekuwa wa kujikomba hasa wa kizazi hiki.
Kuna watu walikuwa hawamuogopi Rais, ndani ya CCM akina Munasa Sabbi Munasa, huyu alikuwa akisema nami nachukua fomu ya kugombea Urais. Hakumwogopa Nyerere.
Zamani hakukuwa na uchawa. Vijana sikuhizi wamekuwa machawa. Hata kama jambo ni la kipumbavu wanashadadia. Hiyo miaka unayoisema upumbavu huu haukuwepo.
Zamani hakukuwa na muheshimiwa, watu walitumia neno ndugu, ati siku hizi uheshimiwa ndo umewekwa mbele watu wanalambwa miguu. Upuuzi huu haukuwepo.
Hivyo acheni kupondea kizazi cha zamani ukadhani watu walikuwa wajinga. Zamani watu tulifundishwa uzalendo. Tunakimbia mchakamchaka, nyimbo za uzalendo. Kwanza zamani tuliifaidi serikali sana.
Matibabu yalikuwa bure, kusoma bure hadi vitabu na madaftari wapewa skuli. Watu wa sekondari na chuo walisafirishwa na serikali wakati wa likizo kwenda na kurudi.
Ebu acheni kuwa mnataka kudharirisha miaka ya zamani mkadhani tulikuwa wajinga. Miaka hiyo kulikuwa na park, au garden karibu kila mkoa. Siku hizi mmejenga kila sehemu, mnauza tu maeneo Dar haina hata sehemu ya kupumlia.
Ebu acheni kuona watu wa zamani kama ndo walikuwa wajinga. Nambia hiyo zamani unayoiponda ulisikia kuna mikataba ya kipumbavu kama hii inayoingiwa leo? Ha ha ha, acheni kusema miaka ya zamani ukadhani watu walikuwa wajinga. Wanaopinga hiyo mikataba leo wote ndio hao wa zamani wanao waelimisha ninyi vijana wa miaka ya 90 na 2000.