Kwa sababu ya umasikini wangu wazazi wa binti wamenikataa

Dogo pole sana.
Ipo hivi.

Unapokua katika Hali uliyonayo wewe, unakua na Imani kwamba huyo binti ndio mzuri na anafaa kuliko wote duniani. Unakua unapata picha Kwa mba ukimuacha unaweza usipate mwingine kama yeye.

Wengi tumepitia hali hiyo. Mimi nilikuja kutambua kua yule alikua kiazi sana yaan kiazi haswa. Kama ningemuoa, ndoa ingenishinda na kama ningekomaa, ningekua mtumwa wa ndoa, yaan ndoa ingenie desha Sana na bila shaka ningekua mtu wa ajabu nisiye na maono ya wapi naenda.

Katika Dunia, Mungu kaumba wa kufanana. Changamoto huja pale anapomchelewesha kwako, yeye Mungu anakua na kusudi zuri tu, akija usimpoteze, akukute umejipanga na umeenea, sio ki pesa au mali, hapana, ki mawazo na utu uzima.

Jikaze, Sali sana, Muombe sana Mungu akuvushe salama.

Hujachelewa hata kidogo. Jipange kiutafutaji sana. Angalia channel zako za pesa zifanyie kazi haswa. Achana na kukimbizana na mapenzi, mpenzi kama huyo atakufanya ukimbizane na mapenzi kumridhisha yeye na sio kujenga maisha yenu ya baadae.

Alie wako atakuelewa vyema na mtayajenga yaliyo yenu.
 
Sasa usilaumu wazazi wako maana jukumu lao kwako liliisha ulipo fikisha miaka 18 tu..sasa hadi unafika late 20s means una 29 utuambie miaka yotee 11ulikuwa unafanya nini hadi uendelee kubaki ulivyo..
 
Well said, niliwaza hvyo pia. Mahusiano ya binti yao ni transaction.
Shukran san
 
Umeenyooka, napenda hard truth.
Naappreciate namna umenikaanga, bless.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…