Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Dah umeweka kozi ninayoisoma na juzi nimefanya last installment sidaiwi sijui nikadai hela yangu
 
Ngoja tusome tu hivyo hivyo, Saivi Hali Kila la sehemu ni ngumu haijalishi umesoma au hujasoma, tena Bora aliesoma kidogo ana mwanga wa Kupambana na maisha kuliko yule ambaye hajasoma.

So degree Bado ni Bora zaidi tena Zaidi.
 
Ahsantee kwa Somo, at least niliyafanya haya kwa kiasi, leo inasaidia kwa kiasi.
Hongera mkuu kwa kushtuka mapema maana kwa wengi ni maumivu 👏🏾👏🏾
 
Na kuna watu walianza Kama wagonjwa Sasa Ni wamiliki wa Hospital,wengine kama migambo Sasa Ni maboss wa usalama wa Taifa.

Either way you are doomed.
 
Mgesema hakuna ajira lakini siyo kusema degree hazina kazi. N akujiajiri siyo lele mama, hata waliosoma entrepreneur wanashindwa kujiajiri.
 
Wewe huna mtu highly placed,ukiwa na mtu ajira ni immediate.Pole sana.
 
Mgesema hakuna ajira lakini siyo kusema degree hazina kazi. N akujiajiri siyo lele mama, hata waliosoma entrepreneur wanashindwa kujiajiri.
Kazi ya hizo degree ni ipi ikiwa tulizisoma kwa lengo la kutupatia ajira na kipato lakini zimeshindwa kutupa hizo vitu?
Zina faida gani sasa?
 
Wewe huna mtu highly placed,ukiwa na mtu ajira ni immediate.Pole sana.
Hao watu wenye high placed person wako wachache katika wengi tunaohitimu na degree zetu.
Hata kama wote tungekuwa na hizo connection bado balance ingekuwa pale pale, wengi (90%) tungekosa ajira na wachache (10%) wangepata ajira.
 
Hao watu wenye high placed person wako wachache katika wengi tunaohitimu na degree zetu.
Hata kama wote tungekuwa na hizo connection bado balance ingekuwa pale pale, wengi (90%) tungekosa ajira na wachache (10%) wangepata ajira.
Pole sana,I pity you so much.Ila kipo kitu ambacho sisi tumeshindwa kufanya:to change our mindset.Degree ilikuwa muhimu before the 1980s wakati ulikuwa unaajiriwa hata kabla ya matokeo na ulikuwa unatafutwa,sio sasa.Siku hizi ajira ni very hard to come by,kwa hiyo from early on tusi force kwenda vyuo vikuu,because it is useless.Tuji-engage in self employment activities mapema,in that case tutajiondolea stress na depression zisizo za lazima.

I would think it even better ku-opt for VETA courses na kuendelea na mfumo huo up to Diploma,degree au hata MSc kwenye mfumo wa VETA.I believe option hiyo ipo, kama haipo waanzishe.Tatizo letu ni tamaa zisizo za lazima,kwani bila kufika Chuo Kikuu huishi?
 
ELIMU ni nyenzo ELIMU ni NGAO kitu pekee ambacho sijutii ELIMU imenipa confidence ambayo wale ambao hawajasoma wanakua na excuses nakujiona inferior....

Naziona fursa nyingi sana sanaaa huko nyumbani Tanzania tena bila ya kua na mtaji sema wengi wanapenda white collar job sema wahitimu wanaenda chuoni kukariri notes ila sio kujaza maarifa 😊☺️ yakuweza kuwasaidia kutawala maisha Yao.....

Watu waendelee kusoma kutanua mbongo zao

Wasalaam
Kwa Sasa +267
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…