Kwa sasa kuna kila dalili Kamala Harris huenda atamshinda Trump kirahisi kabisa!

Umeongea vizur mkuu. Kamala, hawezi kumshinda mnyama Donald. Labda mtoa mada hapo juu, hajui vision na mission , na pia trend za dunia. Digital currency ndio Donald anatakiwa kuinua na sio huo ushoga.Na jana mnyama alikuwa, kwenye conference ya Bitcoin.
Uchumi wa US unaenda kucrush Trump akiwa rais, stocks markets zitacrush pia, infact jamaa ataongoza US kwenye mazingira magumu sana, yes upo sahihi US digital currency itakuja pia enzi ya Trump.
 
Biden hakupingwa kwa sababu ni mzee ila alipingwa kwa sababu ya kutokujitambua na uwezo mdogo wa akili...

Kumtambua Rais wa Ukraine zelensky kama Vladmir Putin
Kuanguka anguka ovyo
Kumuita makamu wake kamala harris "Vice president trump
Kushindwa kushuka jukwaani na kushikwa mkono..
Kushika mkono hewa...
Biden ameshinikizwa atoke sababu ameshindwa kuipa nguvu israel dhidi ya hamas, pia USA inaelekea kushindwa katika vita na URUSI Kupitia UKRAINE !
 
Usipate tabu mkuu zile katuni maarufu zilishatabiri trump president hawajawahi kukosea walitabiri kifo cha malkia wa uingereza wakatabiri maafa walitabiri corona kiufupi zile katuni ni za watu wa system huyo mama muunga mkono mashoga muache akampikie mumewe kwanza.
Utamaduni wa wenzetu ni tofauti sana, wenzetu kupika siyo kazi ya mwanamke tu ni ya wote!

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Kinyang'anyiro cha mbio za urais huko Marekani kimeshika kasi, na upepo wa kisiasa ukibadilika karibu kila wiki. Na sasa habari kubwa ni kuhusu Kamala Harris kuanza kuuvuta upepo wa kisiasa kuibeba Democrat.

Tangu mwanzoni Kamala Harris hakupewa nafasi yoyote ya kuwa mbadala wa Biden. Biden alipoanza kupoteza uungwaji mkono bado Kamala Harris hakupewa faida ya kuwa mbadala wa Biden na hata mara baada ya Biden kuhitimisha mbio zake na kutangaza kuachia ngazi huku akimpendekeza Kamala Harris kuwa mbadala wake bado watu wengi walikuwa na wasiwasi wa Kamala Harris kama ataweza kupambana na Trump na wengi wakisema wanasubiri kwanza kinyang'anyiro cha wagombea wa Democrat kifikie mwisho ili kujua nani ataweza kupitishwa!

Wiki moja tu baada ya Kamala Harris kutangaza kuingia kwenye kinyang'anyiro cha mbio za urais wa Marekani kwa tiketi ya Democrat tayari mawimbi ya bahari kwa upande wa Democrat yameanza kutulia na upepo umeanza kuvuma kwa kasi nzuri kumbeba mwanamama Kamala Harris. Hili halijatokea kwa bahati mbaya, lina sababu zake, na hapa tutalijadili.

Hizi ndio sababu za kwanini Kamala Harris huenda akamshinda Trump kirahisi tofauti na vile isivyotegemewa.

1. Wamerekani wengi bado wana imani kubwa na Democrat na mgombea yoyote kutoka Democrat wangeweza kumuunga mkono. Na huo ni mtaji mzuri wa Kamala Harris. Hali ni tofauti kwa Republican ambapo wanaamini bila Trump huenda republican isiambulie ushindi, hivyo yoyote mwenye nguvu, sifa na uwezo wa kukabiliana na Trump kwenye siasa za majukwaani basi automatically anawashinda Republican, na mwelekeo wa siasa za majukwaani kwa siku hizi chache unaonekana kuwa na neema kwa Kamala Harris.

2. Kamala Harris amepata bahati kubwa ya kuingizwa kwenye kinyang'anyiro kwa lazima na kupewa uungwaji mkono wa moja kwa moja na wademocrat wengi kabla ya kupitishwa kwenye misukosuko ya kuchuana na kuchafuana vilivyo na wagombea wengine wa Democrat katika kinyang'anyiro cha kuteuliwa. Inavyoonekana ni kama wademocrat wote wameamua wambebe Kamala Harris ili washinde. Siku zote umoja ni ushindi.

3. Wapiga kura wazuri na wenye kuamua mshindi wa kiti cha urais wa Marekani ni watu wenye msimamo wa wastani ambao wengi wao hawampendi Trump na walianza kupoteza imani kwa Biden kwa sababu ya matatizo ya uzee wake. Ujio wa Kamala Harris umewaamsha upya na kuwapa nguvu ya kwenda kupiga kura. Hii ndio habari njema kwa Democrat.

4. Wamerekani wengi huwa wanajivunia na kufurahia mnoo kuwa na Rais mwenye sifa, mwelekeo na mvuto katika ulimwengu wa kimataifa, wao huamini Rais wao ndio kioo cha kuwatambulisha wamerekani wote kidunia. Na katika hili wanataka kuthibitisha kwa kuwa na Rais wa kwanza mwanamke tena mwenye asili ya uafrika na uhindi ambaye ni Kamala Harris. Tofauti na hivyo itabidi wampe kura mtu mwenye sifa za utambulisho wa uhalifu na ubaguzi, yaani Trump.

5. Hoja zote za Republican zilizowapa positive political milleage dhidi ya Biden za Uzee, usahaurifu na udhoofu zimekufa kifo cha Mende. Kwa sasa inabidi Trump na Republican watengeneze agenda mpya za kutrend kwa kuwa katikati ya vita wamebadilishiwa adui ambaye yuko tofauti na adui wa mwanzo. Kwa sasa kibao kimebadilika, wamerekani wameanza kuhoji uzee, usafi wa kimaadili na utimamu wa Trump kama unastahili kukalia kiti cha urais wa Marekani.
jmushi1 Kichuguu ...
DR Mambo Jambo

Uchaguzi mgumu huu.
 
Chukua MAUA Umedadavua vizuri sana!
 
Usipate tabu mkuu zile katuni maarufu zilishatabiri trump president hawajawahi kukosea walitabiri kifo cha malkia wa uingereza wakatabiri maafa walitabiri corona kiufupi zile katuni ni za watu wa system huyo mama muunga mkono mashoga muache akampikie mumewe kwanza.
Vikatuni vya utabiri vina nguvu gani ya kuamua nani awe rais wa USA?
Yaani watu waache kupiga kura kisa wanafuatilia vikatuni?

Mbona vikatuni vya Kipanya hapa Tz huwa vinatabiri fresh tu, mbona hatuvipi airtime?
 
Tatizo jinsia ya 'KE' hawapendanagi na kuwaza kuinuana wao kwa wao.Duru ziliarifu Bi Hillary Clinton aliangushwa na Wanawake wenzie...ila walivyokuwa wana demuka na kujaa kwenye mikutano yake ya kampeni sasa!Kumbe wanamuzodoa rohoni:Kura waka mnyima.Ni kama Tanzania tu,Samia hatapata kura za Wanawake akigombea labda Viongozi wa UWT kama JOKATE na wenzake wa juu huko:Hata JF tu..Mfuatilieni- FAIZAFOX komenti zake pale anapo pandisha nyuzi Waziri DR.DOROTH GWAJIMA,anavyokuja kasi na kumpa makavu......!
Katika kura za jumla za uchaguzi, Hillary Clinton alimzidi Trump kwa mamilioni ya kura, hivyo kwa lugha rahisi, wanawake wengi walimpigia kura Hillary Clinton. Bahati mbaya sana, sheria za uchaguzi za USA mshindi hapatikani kwa wingi wa kura za ujumla!
 
Hakuna wakati Marekani itakuja kuongozwa na Mwanamke!!!

Kama alishindwa Hilary Clinton... Huyu Harris ndo hafiki hata robo....
Nani kasema Marekani haiwezi kuongozwa na Mwanamke?
Kama huku Afrika (ambapo mfumo dume umeota mizizi mirefu) kumekuwepo marais wanawake, nini kizuie USA isiwe na rais mwanamke?
 
Hata Trump anafanya makosa hayo hayo kama ya Biden ila ilikuwa kwa kiasi kidogo kuliko Bideni.

Hotuba yake ya kukubali kuwa mgombea ilijaa makosa yakiwemo kumuita makamu wa Rais Pence badała ya Harris.

Kwasasa camera zote zitaangazia uzee wake.
Hapo kwenye uzee nakupinga mana pamoja na hvy bado anaweza kufanya kazi zake vzr tofauti na Biden
 
Kumbuka tu, kwa sasa Trump ana miaka 78 (miaka mitatu tu pungufu ya umri wa Biden (miaka 81)), na ikitokea akafanikiwa kuwa mshindi maana yake muhula wake wa miaka minne utaisha akiwa na miaka 82, yaani mwaka mmoja zaidi ya umri wa Biden wa sasa wa miaka 81. Huwezi kumtenganisha Trump na uzee. Tangu Biden ajitoe, hoja ya uzee imegeuka kuwa mwiba dhidi ya Republican, hawataki tena kuizungumzia sana. Hii hoja ilianza tangu uchaguzi uliopita wakati Biden akiwa na miaka 77.
 
Moja ya jambo linamporomosha vibaya Trump mbele ya wamarekani wengi ni suala la Siasa za kimataifa. Trump haeleweki na aaminiki. Ukaribu wake na Russia, kujipendekeza kwake kwa siku za karibuni na North Korea na Kujiweka kwake karibu na siasa za Netanyau, ni mambo yanayomtafuna kwa kasi.

Nadhani huu mwiba kwa kuwa amegoma kuuchomoa tangu kitambo basi huenda akaung'ang'ania mpaka mwisho.
 
Dunia ya sasa inamtaka mwanamke awe kiongozi kwenye maeneo yote. Zama za wanaume kutawaliwa zimekaribia sana.
 
Back
Top Bottom