Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

Kwa sasa, mita nyingi za Luku zinaondolewa Tariff Zero

Tarif D1 ni na watu wa vijijini, matumizi ya nyumbani na wasiozidi wastanu wa matumizi ya unit 75 kwa miezi mitatu mfulizo
Hapa unamaanisha nini? Watu wa vijijini, kwa hiyo mimi wa mjini hata kama matumizi yangu ni pungufu ya unit 75 hiyo huduma sipati?
 
Elimu bure, flyovers, mishahara, barabara za lami, ndege, SGR, Bwawa la Nyerere, madawa, madaraja, mwendokasi, njia nane e.t.c. vinahitaji kulipiwa na sisi wenyewe.
KULIPA KODI NI WAJIBU WA KILA MWANANCHI.
Sawa, lakini kwa utaratibu mzuri sio kukurupushana km vile wezi.
 
Tafadhali fika ofisi za eneo lako kwa taratibu na masharti kama utaonekana unakidhi utawekwa
Hapa ndipo mnatengeneza nafasi ya rushwa. Amesema anatumia chini ya unit 75 kwa mwezi. Masharti gani tena mengine mnataka?
 
Pole sana. Mimi jamaa waliniondoa, ila wamenipa miezi mitatu ya matazamio. Ikiwa matumizi yatakuwa chini badi nitajaza fomu upya! Nasubiria!asa
Asante. Ngoja na mimi nifanye utaratibu
 
Nadhani suluhisho hapa ni@tanesco kuja hapa na kutumbia ukweli kuwa watu wa mjini hii huduma haituhusu kuliko kuleta uongo wenu hapa
 
Ndugu Tanesco kuna swala moja hutoi maelezo yaliyonyooka. Mimi wa Mjini kama Dar au Arusha au Morogoro nikija kuomba kuingizwa kwenye huo mfumo wa matumizi madogo ya umeme wa 9150 mnakubali au hamkubali?
 
Pole sana. Mimi jamaa waliniondoa, ila wamenipa miezi mitatu ya matazamio. Ikiwa matumizi yatakuwa chini basi nitajaza fomu upya! Nasubiria!
Asante sana. Ngoja na mimi nilishughulikie
 
Mimu tangu 2016 nauziwa unit kwa bei zaid ya 200 wakat matumiz yangu ni chin ya unit 30 kwa mwezi mf nikinunua umeme wa shiling 1000 napata unit 2.8 wakat huo jiran kwa hiyohiyo 1000 anapata zaid ya unit 7 inakuaje hapo???
Watanzania tumekuwa soft sana, hawa jamaa wa Tanesco ni wezi wakubwa, inawezekanaje kwa mfano mini niko hapa eneo kata moja na mtu ambaye yeye analipia umeme chini zaidi kuliko mimi ? yaani huwa naniona mimi kama lofa fulani, mimi nikununua umeme wa shilingi elfu 10 nautumia wiki 2, yeye akinunua umeme wa shs 5000 anautumia mwezi mmoja na nusu, na ni juzi tu nimenunua umeme wa shs 10000 nikapata units 25 sio 28 kama ilivyokuwa siku za nyuma, maana yake ni kwamba wameongeza charges/unit bila hata kutoa taarifa, tungeunganisha nguvu zetu tukawagomea hawa tanesco wabaki na umeme wao, bila kutumia mishumaa,
 
Watanzania tumekuwa soft sana, hawa jamaa wa tanesco ni wezi wakubwa, inawezekanaje kwa mfano mini niko hapa eneo kata moja na mtu ambaye yeye analipia umeme chini zaidi kuliko mimi ? yaani huwa naniona mimi kama lofa fulani, mimi nikununua umeme wa shilingi elfu 10 nautumia wiki 2, yeye akinunua umeme wa shs 5000 anautumia mwezi mmoja na nusu, na ni juzi tu nimenunua umeme wa shs 10000 nikapata units 25 sio 28 kama ilivyokuwa siku za nyuma, maana yake ni kwamba wameongeza charges/unit bila hata kutoa taarifa, tungeunganisha nguvu zetu tukawagomea hawa tanesco wabaki na umeme wao, bila kutumia mishumaa,
Tafadhali onesha namba ya mita kwa ufafanuzi na elimu zaidi
 
Tafadhali onesha namba ya mita kwa ufafanuzi na elimu zaidi
Hata mm hilo tatizo linanikuta namba zangu za meter ni 24212397632 jirani yangu kwa shiling 1000 anapata unit zaid ya 5+ lakin mm kwa hiyohiyo 1000 napat unit 2.8 na nlipoenda tanesco waliniambia nirud sku nyingne na wanaleta indication za rushwa tu nikajiulza hiv hawawez kutatua hili tatzo nikiwa nyumbani?? mm naishi mbali na tanesco gharma za usafiri kwenda na kurud zaid ni sh 15000..
 
Kama yapi tafadhali? Weka maelezo kamili tukupatie ufafanuzi tafadhali.
Kwa mfano mwezi uliokwisha tulinunua umeme badala ya kupewa unit sahihi tukakuta zimepungua mno , kutafakari na kupiga hesabu tukakuta tumekatwa 6000 Yani kumbe Tanesco mmekata Kodi ya nyumba miezi 6 , wakati hatuna deni tumekuwa tukikatwa Kila mwezi mwaka Jana Toka mwezi wa 7 mpk Dec. Je kwanini mumkate mteja miezi 6 kisa amenunua umeme wake wa mwezi ? Mngekata 1000 yenu tu ya Jan.
 
Kwa wateja wote wa maeneo ya mijini wanapaswa kuwa Tarifa 1 ambayo ni matumizi ya nyumbani hadi unit 7500 kwa mwezi, wateja wa maeneo ya vijijini wanapaswa kuwa tarif 1 au tarif D1 kutokana na wastani wa matumizi yao wao wanaozidi wastani wa manunuzi ya unit 75 kwa miezi mitatu mfululizo wanakuwa T1 na wale ambao hawazidi na wapo vijijini wanakuwa D1.
Naleta lalamiko kwenu Tanesco, Niko Kilimanjaro , walikuja watu wa Tanesco mwaka Jana kutaka kukagua mita na kuandikisha mita Kwa ajili ya kukata Kodi ya majengo, wakashindwa kupanda mpk nikawatolea stuli 2 Ili waweze kuifikia mita yangu.Nikawambia nimeshawaambia Tanesco Mita iteremshwe chini lkn imekuwa ni hadithi, wakasema sisi tutashughulikia wiki ijayo tu, wakanipa na no yake ya simu, kumbe wametoa no ya uongo, mpk Leo sijaona Tanesco wakija kushughulikia kuishusha hiyo mita Tena, Je hii ni haki Kwa wateja wenu???
 
Naleta lalamiko kwenu Tanesco, Niko Kilimanjaro , walikuja watu wa Tanesco mwaka Jana kutaka kukagua mita na kuandikisha mita Kwa ajili ya kukata Kodi ya majengo, wakashindwa kupanda mpk nikawatolea stuli 2 Ili waweze kuifikia mita yangu.Nikawambia nimeshawaambia Tanesco Mita iteremshwe chini lkn imekuwa ni hadithi, wakasema sisi tutashughulikia wiki ijayo tu, wakanipa na no yake ya simu, kumbe wametoa no ya uongo, mpk Leo sijaona Tanesco wakija kushughulikia kuishusha hiyo mita Tena, Je hii ni haki Kwa wateja wenu???
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
 
Ndugu wapendwa wateja wetu!

Wateja wetu wote wanawekwa kwenye makundi ya matumizi yanayoendana na matumizi yao kwa kuzingatia wastani wa matumizi na eneo alilopo.

Ifahamike kuwa hakuna mteja wa matumizi ya nyumbani anayeweza kuwekwa kwenye kundi la matumizi ya viwanda.
Mimi kila nikijaribu kununua umeme naambiwa mita namba haitambuliki naombeni msaada tanesco
 
Back
Top Bottom