Kwa sasa ni nadra sana kuwakuta hawa viongozi wapo Dodoma Makao Makuu, wote imekuwa ni njia moja Dar

Hizo safari zinaligharimu taifa pesa nyingi sana. Viongozi wengi wana ofisi na makazi sehemu mbili, Dar na Dodoma. Na ubadhirifu wa kujilipa posho za safari upo, haijulikani ofisi kuu ni ipi. Na kila makazi yana huduma zote, japo za Dodoma hukaliwa kwa nadra.
 
Inasiginwa kwa sababu ya kujaa mianya ya kusiginwa, eg kuna vipengele vya kuwapa viongozi umungu mtu, haajibishwi na yeyote.
 

Nikakubaliana na wewe.
Kwa kiwango hiki hiki ambacho katiba mbovu inakanyagwa na kuto heshimiwa ndivyo itakavyokuwa kuhusiana na katiba mpya. Nayo itakanyagwa, kupuuzwa na kutoheshimiwa kwa kiwango kilekile. Hivyo tatizo halijawahi kuwa ubovu wa katiba bali ni kuto kutii katiba. Nachelea kusema kwamba matatizo ya Taifa letu (na mataifa mengine kwa ujumla) yaliyosababishwa na ubovu wa katiba na machache na mepesi, kuliko matatizo yaliyo sababishwa na kuto heshimu, kupuuza na kudharau katiba.
Jambo la kusisitiza ni jamii (kutia ndani viongozi) kuelewa faida za kutii sheria na katiba ikiwemo bila shuruti.
 
Uamuzi wa kuhamia Dodoma ulikuwa wa kukurupuka umelitia Taifa hasara sana,sasa mdogo mdogo tunarejea Dar es salaam.
 
Hayo ni matunda ya utawala wa kiimla ya dikteta Magufuli. Watendaji walijaa unafiki mtupu. Watu waliacha kufanya kazi kufuata miongozo na wakawa busy kumridhisha Magufuli huku wakitesa watanzania.
Hata mwanafunzi asipofuata matakwa ya mwalimu hufeli haiwezekani viongozi wajichagulie ya kufanya hatutafika
 
Kama katiba ya Marekani isingekuwa na vipengele vya kudhibiti maamuzi ya ajabu nani angemzuia Trump kubaki kwenye kiti cha Urais. Mara hii tumesahau vitimbwi vyake hadi mujahidina wake kuvamia bunge kuzuia uthibitisho wa ushindi wa Biden. Tujaribu kuwa na akina ya maneno.
 
Nakubaliana na wewe. Emu fikiria wengi wa viongozi wa vyama vya siasa wana katiba lakini hawaifuati wala kuheshimu. Kwa mfano mtu anakaa kwenye nafasi ya mwenyekiti au kongozi mkuu miaka nenda - rudi.
 
Acha wale maisha bhana, jipendekeze na wewe uambulie hata UDED.Hii nchi ukipata kacheo wewe kula maisha tu uzalendo baadaye
 
Kwani katiba inasemaje?tuanzie hapo kwanza mdau
 
Kweli ni gharama kubwa sn, ndiyo maana bajeti nzima 20% ndiyo fedha za maendeleo kwa maana ya miradi zingine ni kulipana posho wakubwa
 
Muda wote wapo safarini hakuna la maana wanafanya
 
Chama cha siasa cha upinzani kitakacho jipanga vizuri na kuwa na Sera za kurudisha Daisalamu kuwa ndio makao makuu ya nchi na kwenda nayo kwenye uchaguzi 2025 kitaipa taabu sana CCM.

Kuhamia Dodoma kwa msukumo ule na utapanyaji wa rasmilali nchi ili kufanikisha hilo yalikuwa ni maamuzi ya hovyo sana. Nilisema hili JPM akiishi. Ninalisema sasa akiwa haishi na nitalisema siku zijazo.
 
Sikubaliani na wewe hata kidogo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…