Kwa sasa shetani ndiyo Kiongozi Mkuu wa DINI zote

BujiBuji umetisha. Wewe ni Makamu wa Mshana Jr kwenye haya mambo. Bandiko ni bora kabisa kwa ajili ya kupata ilimu.
 
Ni kweli kabisa.
Kwa sababu dini zote zina Siasa(maslahi ya kikundi fulani) na huo ndio ushetani wenyewé.

Dini ni suala la mtu na Mungu wake. Na sio vikundi au magenge ya Watu kukaa pamoja
Imani ndio suala la mtu binafsi na anachokiamini lakini dini lazima iwe ni muafaka wa kiimani katika jamii fulani.

Dini ni taasisi ya kijamii lakini imani ni mawasiliano kati ya kiumbe kimoja na kingine.

Hivyo, dini zimehodhi mawasiliano baina ya nguvu ya uumbaji na viumbe vyake.

Kimantiki, huwezi kuwa na dini isiyokuwa na imani lakini unaweza kuwa na imani bila kuwa na dini yoyote.

Dini zimekuwa zikifanya jinai ya kiroho kwa kulazimisha viumbe wenye namna/njia tofauti za mawasiliano kuwasiliana kwa namna/njia zinazofanana.

Kila mwanadamu anamsimbo wake wa kuziamsha nguvu alizojengwa nazo kutoka kwa muumba.

Chukulia mfano, matunda, kila tunda lina virutubisho vyake ambavyo ni tofauti na matunda mengine. Suala hili linayafanya matunda tofauti tofauti kuwa na uwezo wa kukabiliana na magonjwa tofauti katika mwili wa mwanadamu au kiumbe chochote.

Kwa wanadamu ipo hivyo pia, kila mmoja ana nguvu/kipawa chake ambapo atalazimika kukitunza kwa namna/mawasiliano yake binafsi na muumbaji.

Huwa sitaki mtu aje kunihubiria masuala ya dini yake, ijapokuwa sikatazi watu kushiriki ibada za dini zao.

Tukitaka kuamsha nguvu ya mawasiliano baina ya mwanadamu na muumba wake katika taifa hili, tutaanza kufanya censorship ya mahubiri katika nyumba za ibada, yaendane na namna sisi tunavyotaka kwa maslahi ya kizazi kijacho.

Asante

Mshana Jr Kiranga @mwifa Da'Vinci LIKUD Zitto jr
Jumong S Rakims walter walker
 
Hizi dini ni za kwao, na watu weusi tulizipokea maanake tuliridhia na tulikubali mapokeo yake.....Leo wanapoleta instructions zao ambazo zinapingana na Mila zetu tusiite 'ni shetani'
 
Hizi dini ni za kwao, na watu weusi tulizipokea maanake tuliridhia na tulikubali mapokeo yake.....Leo wanapoleta instructions zao ambazo zinapingana na Mila zetu tusiite 'ni shetani'
Tuwaite watakatifu, au sio ?
 
Hili kuifahamu dini ya uisilamu lazima uwe msomi wa qur,aan na sunna umesoma aya gani na hadithi namba ngapi inayo sema kuwa uisilamu ulikuja miaka 600 baada ya kuondoka yesu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…