Kwa sasa shetani ndiyo Kiongozi Mkuu wa DINI zote

kula K-VANT nakuja kulipa mazee!!
 
Shetani akawaambia mwanamke Maana Mungu anajua siku mtakapokula tu mtafanana naye
Shida ni haya matunda ya mti wa ujuzi wa MEMA NA MABAYA
 
Unachoongea ni kweli maana shetani kutokana na maandiko ya Biblia inamwita "mdanganyifu na baba wa uongo". Shetani ni rahisi kukuaminisha kwamba hakuna Mungu na kukupa facts na wewe ukaamini na hao amewashika watu wengi tu na hawaamini kama kuna Mungu wakati ukweli uliosimama ambao hautapingika ni kwamba Mungu yupo na ndiye aliyeumba mbingu na nchi. Pia Bibilia inamuita shetani "mungu wa dunia hii". Deception ni kubwa sana hata kwa watu wa Mungu na unasikia eti ukifia dini mabikira 72 wanakusubiri au utaenda ahera kumbe mwenzangu umeshadanganyika ukifa tu ziwa la moto linakusubiri na ndivyo ilivyo uamini usiamini. Sasa hapo ndiyo ujue uongo mkubwa wa shetani. Ona jinsi alivyokuja kwa Yesu (ingawa alikuwa mwana wa Mungu) akimwambia "ukinisujudia nitakupa utajiri wote huu maana uko mikononi mwangu". Sasa kama hakuweza kumwogopa hata Yesu mwenyewe sisi kama binadamu si anatupa mali tu na kumwacha Mungu mara moja. Na hiki cha mali ndicho shetani anawafanyia watumishi wa Mungu ili waweze kupenda pesa na kuacha njia za Mungu. Mambo ni mengi lakini kwa wale wateule wa Mungu, Mungu awalinde na deception za huyu muuaji mpaka atakapokuja BWANA WETU YESU KRISTO. . Yesu alisema kwenye Yohana 10:10 " Mwizi (shetani) anakuja kuiba, kuua, na kuangamiza. Lakini mimi (Yasu mwana wa Mungu) nilikuja kuwaletea uzima, na muwe nao kwa ukamilifu".
 
Dini yoyote ile inayojikita kwenye kushika sheria, hiyo inatumika na Shetani
 
Ulichoandika hapa ni pure diarrhea - yaani kuhara kwa kufa mtu! Kuhusu papa naambatanisha document (Declaration) inayozungumziwa na uisome yote. Imeandikwa katika lugha mbalimbali. Kiingereza (angalia kuanzia ukurasa 20). Document nzima ina aya 1-45. Soma taratibu uelewe na underline mstari, sentensi au aya ambayo inaonyesha papa anasema "kanisa lihalalishe ndoa za jinsia moja" kama ulivyoandika. Hapo nitajua unasema ukweli mtupu na uwongo kwako mwiko. Otherwise, nitajua wewe ni mmoja wa mawakala wa yule mwovu mliotumwa kueneza uwongo duniani hata bila kujitambua.
 

Attachments

Sina hoja ya kupingana na wewe kwa kuwa dini ndiyo makazi ya shetani kwa sasa, ni kuachana na dini hizo zenye ushetani ndani yake. Tuutafute utakatifu na haki yeke humo kuna wokovu, dini ni mzigo
 
Naunga mkono HOJA 🙏

Yesu hakuja duniani kueneza dini,

Bali alikuja kueneza Upendo wa Mungu Kwa WANADAMU, Akileta Imani na maisha ya utakatifu,

KANISA ni Mtu mmoja aaminiye. Wakikusanyika, yanakuwa makanisa.

MWILI wangu ndilo hekalu ambalo Yesu anaishi kupitia Roho wake mtakatifu, hivyo kamwe mwili wangu hautachafuliwa na zinaa na makufuru !!

Na tukikusanyika wawili, Yesu Yu pamoja nasi!!

Dini zikijikusanya Kwa kumtumikia shetani, sisi Bado tutasimama na Imani katika Yesu Kristo,

Tutaongozwa na NENO LA MUNGU NA ROHO MTAKATIFU.

Na tutajitenga na dini zenye makufuru na maelekezo ya mashetani.

YESU tusaidie, tuitunze Imani hata urudipo.

Aaamen
 
Upo sahihi
Kwa asilimia kubwa dini zote zinatawaliwa na Shetani.
Sio wale wanaosema Shetani matendo mabaya.
Ni Shetani mwenyewe, yaani Ibirisi Lusifer na Malaika zake Majini.

Mfano kwenye Ukristo.
Akina Mackenzie wa kule Kenya
Akina Kibwetele Uganda
Akina Mfalme Zumaridi, Nabii Tito, Tanzania.
Ni kati ya hao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…