Kwa sasa sina imani kabisa na bidhaa za Azam, hususani Embe

Kwa sasa sina imani kabisa na bidhaa za Azam, hususani Embe

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Kinachonikosesha imani baada ya fantastic philip kuelezea mchanganyo wa Asobic Acid na Benzoate ambazo zikichanywa zinaleta madhara.

Vipi ikiwa Azam atachanganya kimya kimya na kwenye ingredients asiandike, je kuna vipimo vya kupimia na kujua mchanganyiko huo?

Mfano, sayona tunda tutajuaje kama hajachanganya? Mpaka tuangalie kwenye vichanganyo tu? TBS, TFDA huwa wanafanya kazi gani?
 
Hili sakata huwezi kuona waandishi wa habari za kawaida, mchezo au udaku wakilivalia njuga sababu Azam ni their dream destination. Wako radhi jamii nzima iangamie ili wao wapate mshahara wa kila mwezi.

Hata hii generation ya kwetu ni ya kipumbavu kabisa, ingekuwa ni jambo la kijinga kama ndoa ya manara, kila mtu angekomaa nalo hadi mishipa ya koo ingemtoka.
 
Kinachonikosesha imani baada ya fantastic philip kuelezea mchanganyo wa Asobic Acid na Benzoate ambazo zikichanywa zinaleta madhara.

Vipi ikiwa azam atachanganya kimya kimya na kwenye ingredients asiandike, je kuna vipimo vya kupimia na kujua mchanganyiko huo?

Mfano, sayona tunda tutajuaje kama hajachanganya? Mpaka tuangalie kwenye vichanganyo tu? TBS, TFDA huwa wanafanya kazi gani?
Kwani Azam wenyewe wanasemaje? , mbona sioni clip wakitoa maelezo kuhusu Benzene inayotokana na mchanganyika wa hiyo Sodium Benzoate na Ascorbic Acid?
 
Acheni chuki watanzania,
Unahakika gani juu ya coca cola na Pepsi kuwa ni salama?
Carbonated soft drinks zote hazikosi madhara.
Soda kila mtu anajua si salama na tumeshajua ukweli. Shida ipo kwenye hizi ambazo tuliamini ndio kimbilio kwa wale tulioacha soda, maana kaandika ‘JUISI HALISI YA MATUNDA’ , matokeo yake kumbe kaweka Sodium Benzoate na Ascorbic acid huku akijua wazi mchanganyiko huu unazalisha Benzene inayoleta Cancer..., sasa hapo tukae kimya ndugu yangu?!
 
Ni sahihi kupaza sauti ili kuokoa maisha yetu na pia huenda akatafuta namna ya kurekebisha, 👍
 
Back
Top Bottom