Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
KWA SASA WANAWAKE WENGI WANAJIAAMINI SANA KULIKO WANAUME; VIJANA WENGI WAMEKUWA MAZUZU!
Anaandika, Robert Heriel
Ili mwanaume asijiamini itampasa awe na mapungufu Kati ya haya;
i) Upungufu wa Akili/ uwezo mdogo wa kufikiri.
Uwezo mdogo wa kufikiri ni moja ya sababu zinazopelekea kijana kutokujiamini.
Upungufu wa Akili unaathari ya Moja Kwa moja katika maisha ya kijana.
Kuanzia utafutaji wa fedha na Mali, kujitambua, mahusiano yake na watu wengine, kujilinda na kutunza heshima yake. n.k
Kama mzazi unaowajibu wa kumuandaa mtoto wa kiume hasa katika kipengele cha Akili, uwezo wa kuchambua, kutafakari, kuchanganua, kutatua changamoto, kuthmini, na kutoa maamuzi.
Kushindwa kutongoza binti au kumchombeza Binti hasa Mrembo ni moja ya mambo yanayowasumbua Vijana WA Zama hizi.
Wasichana WA siku hizi wamejikuta katika hali ngumu Kwa kukosa Haki zao za kutongozwa Kwa ushawishi wa hali ya juu.
Zingatia, Kwa Wanawake kushindwa kutongoza Kwa inahesabika kama kutokujiamini, kutokuwa na uwezo mzuri wa Akili,
Mwanamke kadiri unavyoshindwa kumshawishi ndivyo anavyozidi kujiamini Mbele yako.
Elewa kuwa, Mwanamke unapomuita Mbele yako kitu cha Kwanza atakachokifanya ni kujitutumua na kuishawishi Akili yako kuwa yeye ni wathamani Sana na kitendo cha yeye kusimama Mbele yako basi hiyo uiite bahati kwako.
Sio ajabu Akaja anakunyali au anadengua, huku akikuuliza unashida gani, na akijifanya anaharaka Sana.
Hiyo yote ni mbinu Yao ya asili kupima kama Mwanaume aliyesimama Mbele yake ni mwanaume kweli au sio.
Akili na ubongo ndio humfanya MTU ajiamini. Ubongo ndio unatawala Kwa kiasi kikubwa Matendo ya Mwili.
Tukija kwenye ishu za Familia Kwa Wakubwa,
Wababa WA siku hizi wengi tumekwama, tunahitaji maboresho turudi katika mifumo yetu.
Akili yako endapo itaruhusu kutingishwa na Mkeo mara Kwa mara jua anajaribu kuondoa kujiamini kwako.
Vitisho, mashambulizi ya mara Kwa mara ya kukutingisha, Makosa yakujirudia rudia sio Rafiki katika Ndoa.
Watu wa uswahilini wanasema, anajaribu Dawa.
Hiyo itakufanya usijiamini.
2. Ukosefu wa KAZI.
Mwanaume kama Hana kazi hawezi kamwe kujiamini.
Moja ya majukumu ya mwanaume ni kuwa na Kazi. Kazi ndio uanaume wenyewe.
Amri ya kufanya kazi katika mfumo wa binadamu inamhusu Mwanaume.
Katika Maisha yako, ogopa kukosa Akili(kuw mjinga) na pili, ogopa kukosa kazi.
Vijana wengi Kwa sasa wamepoteza kujiamini Kwa sababu wengi wao Hawana kazi. Yaani wanaishi kindegendege.
Alafu Mbaya zaidi Wanawake wengi wao ndio wanahangaika kufanya kazi. Hata kama ni vijikazi vyenye kipato kidogo lakini vinawasogez hivyohivyo.
Lazima ieleweke kuwa Mwanaume asiye na kazi hawezi jiamini mbele ya Mwanamke mwenye kujihudumia mwenyewe, mwenye kazi.
Hata kama kazi yake ni Saluni, au Mama ntilie ilimradi Mwanamke anajihudumia, ni ngumu Sana Mwanamke wa hivyo kuwa low key dhidi ya mwanaume asiye na kazi.
Kijana wangu, Taikon nakushauri ili uitwe mwanaume kamili ni lazima uwe na Akili, kisha uwe na Kazi.
Kazi ndio uanaume wenyewe. Kwamba utapewa MAJUKUMU, utatwishwa majukumu.
Mwanamke anapokuja kwako elewa kuwa anakuja kukutishwa mambo yaliyomshinda, mizigo yake.
Sasa kama hauna hata kazi utaweza kweli kusimama mbele yake.
Utasimama kama Nani?
Elewa kuwa wapo Wanawake wanauchumi mzuri kukuzidi sasa hawezi kuwa na wewe kama huna Akili anayoiona ni kubwa kuliko yake ili muishi wote.
Ni aidha uwe na Akili kubwa, au uwe na Kazi inayohudumia matumizi yake ya msingi.
Sasa Vijana WA siku hizi mmekuwa majinga Sana. ATI unatafuta Mwanamke atakayekupenda Kwa dhati alafu Wakati huohuo huna Akili wala huna kazi.Looh! Nakusikitikia Sana! Utatafuta hautopata Maisha yako yote. Mwanamke hanaga kitu inaitwa mapenzi ya dhati.
Sisi wanaume ndio tunauwezo WA kuwapenda wao Kwa mioyo yetu yote.
Wao wameumbwa Kutii na kuheshimu, Sisi tumeumbwa kupenda.
"Fanya kazi kwa siku sits kisha ya saba pumzika". Sijui unaelewa hiyo sentensi. Yaani katika siku Saba, basi sita piga kazi. Yaani piga kazi haswa. Muda wa kupumzika uwe NI mdogo.
Kazi gani sasa? Mbona hakuna Ajira.
Kazi zipo, anzia kazi ndogondogo zinazodharaulika hizohizo utashangaa.
3. Kupenda vitu rahisi na vyaburebure.
Moja ya Tabia ya MTU asiyejiamini ni kupenda vitu vya burebure na rahisirahisi.
Vijana WA siku hizi Kwa vile Akili zao zimeshaharibika wanaanza kuwa na mawazo ya Kike. Kupenda mambo rahisi rahisi. Burebure.
Kijana anaogopa kufanya kazi ngumu, kijana anaogopa kudai Haki zake😂😂
Yaani kijana kafanya kazi alafu anazungushwa zungushwa kama Zuzu 😊 hiyo haitoshi bado anajibiwa nyokonyoko, yaani kazi yake umfanyie, jasho lako litoke, Pesa yako usipewe na matusi na kejeli upewe. Alafu unachekacheka kama Boya.
Aiseee! Vijana lazima muwe wakali, msikubali MTU akadharau ujana wenu. Hasa jasho lako.
Hivi MTU kama amedharau kazi uliyoifanya anakutukana atakavyo, wewe uanaume wako ni upi hapo. Mtia mabanzi, Waajiri wakijua kuwa Vijana WA nchi hii hawataki mchezo, dharau za kijinga hawawezi kuwafanyia Michezo ya kipuuzi.
Oooh! Kuna kulazwa sijui Polisi, ndio kulazwa kupo. Lakini Usiwe na busara kupitiliza hasa ukiwa umri wa ujana. Utakwama!
4. Kupigania urembo
Yaani Wakati Wanawake wakihangaika kuutafuta uanaume Kwa kutaka Haki ya kufanya kazi(kumbuka Kufanya KAZI ni KWAAJILI ya wanaume) ninyi Vijana mnapigana vikumbo kupigania urembo, ATI uwe handsome boy, uwe sijui shalobaro, sijui mavimavi gani.
Hivi uliwahi ona shalobaro asiye na kazi na kichwa kikiwa Empty Set akawa anajiamini?
Unatafuta kuwa mchawi na mlozi.
Maana huwezi kuwa shalobaro alafu huna kazi alafu usiwe Mlozi.
Unataka kuwawekea Wake za Watu madawa ya kienyeji kama mbinu kupandisha self-esteem yako.
Kijana, elewa kuwa Mwanaume hasifiwi uzuri, utanashati, au Sifa zingine za like. Mwanaume anasifiwa KAZI na AKILI.
Wanawake wengi siku hizi wataendelea kuwatesa Kwa sababu wao wanapigania wawe kama Sisi WANAUME. Na ukishakuwa mwanaume kamili lazima ujiamini.
Sasa kama Mwanamke ni Mrembo (anaweza kujiremba kwa Pesa yake) na anakazi, anahudumia waliochini yake ambalo ni jukumu la Sisi wanaume ataachaje kujiamini?
Unaishia kusema tuu oooh! Kichwa cha nyumba, sijui mwanaume ni mwanaume.
Hivi hujui ndani ya kichwa kuna ubongo wenye Akili.
Unapoambiwa mwanaume ni kichwa cha nyumba wenzako wanamaanisha mwanaume ni Akili ya nyumba.
Kama huna Akili ya kutosha hiyo Sifa huna.
Vijana, ni Wakati wetu kurejesha Ile heshima yetu itakayotufanya tujiamini.
Nipumzike SASA.
Nawatakia maandalizi mema ya SABATO.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

- jinsi unavyoongea,
- jinsi unavyosimama,
- jinsi unavyomtazama.