KERO Kwa takriban mwezi mmoja na nusu sasa, Wanachi wa Manispaa ya Musoma tunapata shida ya maji

KERO Kwa takriban mwezi mmoja na nusu sasa, Wanachi wa Manispaa ya Musoma tunapata shida ya maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ni takribani mwezi na nusu sasa kumetokea changamoto ya upatikanaji wa maji katika Manispaa ya Musoma.

Mwanzoni tuliambiwa tatizo lilisababishwa na upungufu wa umeme kwenye pampu za kusukuma maji. Hata hivyo, TANESCO Mkoa ilikanusha taarifa hiyo, ikisema hakuna upungufu wowote wa umeme katika eneo la Bukanga, ambako kuna pampu za maji, na kuitaka MUWASA kushughulikia changamoto zake bila kuilaumu TANESCO.

Nahisi hapo ndipo tatizo lilipozidi kuwa kubwa. Baadaye tulishuhudia mabadiliko ya wakurugenzi wa mamlaka ya maji, ambapo aliyekuwa Mkurugenzi wa MUWASA alihamishiwa Kasulu na Musoma akaletewa aliyekuwa Mkurugenzi wa Maji Bunda. Tangu alipokuja, hali imekuwa mbaya zaidi. Maji yakakatika kabisa, hata yale yaliyokuwa yakitoka usiku yakakoma.

Baada ya wananchi kulalamika sana, MUWASA ilitoa taarifa kuwa pampu ya kusukuma maji imepata hitilafu, na kutangaza ratiba kali ya mgao wa maji. Kwa mfano, baadhi ya maeneo hukaa bila maji hadi siku tano, huku mengine yakikosa maji kwa siku nne.

Swali langu ni: Je, MUWASA haina vifaa vya akiba au pampu mbadala? Inawezekanaje maji kuwa tatizo kwa zaidi ya mwezi mmoja wakati Manispaa ya Musoma imezungukwa na Ziwa Victoria?

Hapa nieleweke, siyo ubaguzi. Lakini kama serikali inapanga kusogeza maji ya Ziwa Victoria hadi Dodoma, tungependa pia maeneo ambayo maji yanatoka yawe kipaumbele katika kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma hiyo. Baada ya hapo, wengine wafuate, kwa sababu sisi sote ni Watanzania na maji ni uhai.

Screenshot_20260828_123739_WhatsApp.jpg
 
Back
Top Bottom