Kwa takwimu hizi za sensa hapa Tanzania na duniani, agizo la Quran kuoa mpaka wanawake wanne halitekelezeki

Kwa takwimu hizi za sensa hapa Tanzania na duniani, agizo la Quran kuoa mpaka wanawake wanne halitekelezeki

Kuna mambo yanafikirisha pale baadhi ya vitabu vya kale kutoa maelekezo ambayo yanapingana na uhalisia wa dunia.

Tanzania (mwaka 2022)
Wanawake 31,687,990
Wanaume 30,053,130

Duniani (mwaka 2021)
Wanaume: 3,970,238,390 (bilioni 3.97 sawa na asilimia 50.42%)
Wanawake: 3,904,727,342 (bilioni 3.905 sawa na asilimia 49.58%)

Kwahiyo hapa duniani, kwa kila wanawake 100 wanaozaliwa kuna wanaume 106 wanazaliwa. Wanaume ni wengi kuliko wanawake kwa mujibu wa takwimu zinazotambulika.

Wanaume wakiamua kuoa wake wanne kama Quran inavyoruhusu basi itabidi hao wanawake wawe wa shirikisho kwa wanaume. Hii haikubaliki katika jamii nyingi ulimwenguni.

Allah atakuwa alitoa agizo hili bila kuifahamu dunia maana tungetegemea wanawake wawe wengi sana kuliko wanaume. Tunaweza kuhitimisha kwamba hakuifahamu dunia.
Hapa najitahidi nisiweke hisia au imani. Kuna fact. Hapo nakwama niseme nini. Ila naomba yasitumike maneno ya kuudhi please. Uwe mjadala wa kisomi.
 
Kuna mambo yanafikirisha pale baadhi ya vitabu vya kale kutoa maelekezo ambayo yanapingana na uhalisia wa dunia.

Tanzania (mwaka 2022)
Wanawake 31,687,990
Wanaume 30,053,130

Duniani (mwaka 2021)
Wanaume: 3,970,238,390 (bilioni 3.97 sawa na asilimia 50.42%)
Wanawake: 3,904,727,342 (bilioni 3.905 sawa na asilimia 49.58%)

Kwahiyo hapa duniani, kwa kila wanawake 100 wanaozaliwa kuna wanaume 106 wanazaliwa. Wanaume ni wengi kuliko wanawake kwa mujibu wa takwimu zinazotambulika.

Wanaume wakiamua kuoa wake wanne kama Quran inavyoruhusu basi itabidi hao wanawake wawe wa shirikisho kwa wanaume. Hii haikubaliki katika jamii nyingi ulimwenguni.

Allah atakuwa alitoa agizo hili bila kuifahamu dunia maana tungetegemea wanawake wawe wengi sana kuliko wanaume. Tunaweza kuhitimisha kwamba hakuifahamu dunia.
Ukiangalia historia ya uislamu na amri zeke ni kwamba hyo amri ya wanaume kuoa wanawake wanne ilikuja baada ya waislamu kwenda kwenye vita na wanaume wengi walipoteza maisha hvyo kukubaki wajane wengi sana ndio mungu akaamrisha wanaume waoe wanawake wanne ili kuwanusuru wajane ambao wanaume zao walipoteza maisha vitani na wala hakuna la ziada lango la wake lilikuwa kuwanusuru wanawake wajane ambao waume wamekufa either kwa vita au kwa ajali au kwa njia nyingineyo wala hakukuwa na lengo jingine zaidi ya hlo sio kama vile anavyofanya manara anachezea wanawake kila siku anaoa na kuacha.
 
Ukiangalia historia ya uislamu na amri zeke ni kwamba hyo amri ya wanaume kuoa wanawake wanne ilikuja baada ya waislamu kwenda kwenye vita na wanaume wengi walipoteza maisha hvyo kukubaki wajane wengi sana ndio mungu akaamrisha wanaume waoe wanawake wanne ili kuwanusuru wajane ambao wanaume zao walipoteza maisha vitani na wala hakuna la ziada lango la wake lilikuwa kuwanusuru wanawake wajane ambao waume wamekufa either kwa vita au kwa ajali au kwa njia nyingineyo wala hakukuwa na lengo jingine zaidi ya hlo sio kama vile anavyofanya manara anachezea wanawake kila siku anaoa na kuacha.
Ni mbumbumbu tu ndio atakubaliana na mleta mada kuwa wanaume ni wengi kuliko wanawake..nenda hospital au kituo chochote Cha afya kaombe ratio wa watoto wanaozaliwa Kati ya wakike na wakiume then urudi...
 
Ni mbumbumbu tu ndio atakubaliana na mleta mada kuwa wanaume ni wengi kuliko wanawake..nenda hospital au kituo chochote Cha afya kaombe ratio wa watoto wanaozaliwa Kati ya wakike na wakiume then urudi...
Yaani hata tungekuwa sawa bado wanaume ni wachache hapo kuna vichaa hapo na mapadre sijui kuna wengine wapo jela kuna kina juma lokole hapo yaani tabu tupu yaani wanaume waliopo timamu kiakili kiuchumi na waliopo uraiani ni wachache sana .
 
Hiyo dini ilitokana na jamaa ambaye alikuwa hajui kusoma wala kuandika hivyo lazima mambo mengi yawe upotoshaji mkubwa.

Ngoja niwaite hawa waje kumpigania Allah. FaizaFoxy Mohamed Said Kisai ETUGRUL BEY JumaKilumbi The Icebreaker professional Driver medisonmuta

Na mkuu Mokiti na Che mittoga wataongezea nondo.
Mtume Muhammad hakujuwa kusoma wala kuandika ni hoja na kuna hekima zake


(i)Mtume Muhammad (s.a.w) Kutojua Kusoma na Kuandika:
Iwazi mno katika historia yake kuwa Mtume (s.a.w) hakujua kusoma wala kuandika. Ukweli huu wa historia unathibitishwa na aya za Qur-an zifuatazo:
"Sema (Wewe Nabii Muhammad): Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Allah kwenu nyinyi nyote, (Allah) ambaye ana ufalme wa mbingu na ardhi, hapana aabudiwaye (kwa haki) ila Yeye, Ndiye ahuishaye na ndiye afishaye.Basi mwaminini Allah na Mtume wake, aliye Nabii Ummy, (asiyejua kusoma wala kuandika), ambaye humwamini Allah na maneno yake na mfuateni yeye ili mpate kuongoka." (7:158)
"Na hukuwa mwenye kusoma kitabu chochote kabla ya hiki, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kuume, ingekuwa hivyo wangefanya shaka wale wanaotaka kubadilisha (haki)." (29:48)

Sababu ya Mtume (s.a.w) kutojua kusoma wala kuandika imebainishwa wazi katika aya hii ya (29:48) kuwa angelijua kusoma na kuandika watu wakaidi wasio tayari kumwamini Mtume na kuamini Qu-ran kwa sababu si maneno ya Allah(s.w) bali ni maneno aliyoyatunga Mtume (s.a.w) au ni maneno aliyoyanakili kutoka kwenye vitabu vya kale au ni maneno aliyofundishwa na watunga mashairi mashuhuri na kuyanukuu kwenye kitabu. Mtume (s.a.w) angalijua kusoma na kuandika ingalikuwa vigumu sana kuonesha udhaifu wa madai haya.
Lakini kutojua kusoma wala kuandika kwa Mtume (s.a.w) kumewafanya wapinzani wengi wakose hoja ya uwazi ya kukataa kuwa Qur-an si Kitabu cha Allah (s.w).Hata hivyo, pamoja na ukweli wa historia kuwa Mtume (s.a.w) hakuwa ni mwenye kujua kusoma wala kuandika, walitokea watu waliojitia upofu na kudai kuwa Qur-an ni maneno ya Muhammad (s.a.w). Ili kuwahuzunisha na kuwaonesha kuwa ni waongo katika madai yao hayo, Allah (s.w) aliwawekea watu hao na walimwengu kwa ujumla changa moto ambayo tutaiona katika kipengele cha (ix).

Kwa hiyo Mtume Muhammad (s.a.w) kutojua kwake kusoma wala kuandika na bado akawasilisha kwa watu ujumbe mzito wenye hekima kubwa na wenye kumuongoza mwanaadamu kwa usahihi katika kila kipengele cha maisha yake, ujumbe ambao hapana yeyote anayeweza kuleta mfano wake ni ushahidi mkubwa kuwa Qur-an yote kama ilivyo ni maneno ya Allah (s.w).
 
Quran haikuchukuliwa kutoka kwenye biblia


(b)Dai la Kunakili Biblia


Aidha wengine wanasema Muhammad alinakili mafundisho ya biblia na halafu akadai kuwa yanatoka kwa Allah (s.w). Lakini inadaiwa kuwa hakunakili kila kitu bali alichagua sehemu fulani fulani alizoziona nzuri. Ushahidi wanaoutoa ni kuwa zipo sehemu katika Qur-an ambazo zinafanana na zile zilizomo katika Biblia. Hivyo, kwa kuwa ilitangulia Biblia kabla ya Qur-an ni wazi kuwa Qur-an ndiyo iliyochota kutoka katika Biblia. Madai haya ni dhaifu kwa sababu zifuatazo:

(i)Muhammad (s.a.w) alisema na kusisitiza kuwa Qur-an imetoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w).

(ii)Muhammad hakujua kusoma wala kuandika.

(iii)Nakala ya kwanza ya Agano la Kale (Old Testament) kufasiriwa kwa lugha ya Kiarabu ilipatikana mwaka 900 A.D.Wakati huo ilikuwa imekwishapita miaka 200 tangu Muhamad kutawafu. Ama Agano Jipya (New Testament) lilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1616, miaka elfu baada ya Muhammad (s.a.w) kufariki dunia!

(iv)Qur-an (4:82) imesema kuwa lau kama hii Qur-an ingetoka kwa asiye kuwa Allah ingekuwa na khitilafu nyingi. Hivyo mtu mwenye shaka na aitumie fursa hiyo kutafuta khitilafu katika Qur-an.
(v) Isitoshe, ikiwa kuna tungo mbili au vitabu viwili vimefanana, kufanana huko peke yake si ushahidi wa kutosha kuwa kitabu kimoja kimenakili kutoka katika kitabu cha kwanza kuandikwa. Hii ni kwa sababu yawezekana pia kuwa vitabu vyote viwili vikawa vimetegemea au kunakili kutoka katika kitabu cha tatu ambacho sisi hatukijui. Ilivyo ni kuwa Taurati, Injili na Quran ni vitabu vya Mwenyezi Mungu. Hivyo ni wazi kuwa kama Biblia imenukuu aya halisi za Tourati na Injili lazima aya hizo zitafanana na aya za Qur-an,kwa vile zote zinatokana na Allah(s.w).

Isitoshe utafiti uliofanywa na baadhi ya wanazuoni umeonesha kuwa amri kumi za Mungu zilizomo katika Agano la Kale kwa mfano, zimekuwemo katika vitabu vya Wahindu kabla ya kuja kwa Agano hilo la kale. Je, tuseme biblia ilinakili amri hizo kutoka kwa Wahindu? Si lazima iwe hivyo. Pamoja na kufanana huko katika baadhi ya sehemu bado kimsingi Biblia na Qur-an zimetofautiana kiasi kikubwa.

Tofauti za Kimsingi Kati ya Qur-an na Biblia

(1)Biblia si kitabu kimoja bali ni mkusanyiko wa vitabu 73 kwa mujibu wa madhehebu ya Wakatoliki au vitabu 66 kwa mujibu wa madhehebu ya Waprotestanti. Vitabu hivyo viliandikwa na waandishi wasiopungua 40. Qur-an ni kitabu kimoja kilichotoka kwa Mwenyezi Mungu na aya zake zote ziliandikwa mara tu baada ya kushuka.

(2)Biblia ni kitabu chenye mchanganyiko wa maneno ya Mwenyezi Mungu, Mitume na maoni ya wanahistoria. Qur-an ni neno la Allah (s.w) tu peke yake. Hata maneno ya Muhammad (s.a.w) hayamo katika Qur-an.
(3)Katika Agano la Kale na Jipya yapo maelezo juu ya historia ya maisha ya Mitume. Kumbukumbu la Torati siyo tu ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu bali pia historia ya maisha ya nabii Mussa (a.s). Injili ya Mathayo, Luka, Marko na Yohana zinaelezea historia ya Yesu kama ilivyosimuliwa na wanafunzi wake. Qur-an inataja habari za mitume waliopita ili kutoa mafundisho kwa watu lakini sio kama sira (biography) za mitume hao.

(4)Biblia inavyo vitabu kadhaa ambavyo viliandikwa miaka mingi sana baada ya kutawafu mitume hao. Ndio maana wanazuoni Wakikristo hupata matatizo sana katika uchambuzi wa maandiko hayo kwani hushindwa kumjua nani mwandishi na aliandika lini. Kwa mfano katika Biblia iliyotolewa na Collins iitwayo: Revised Standad Version ya 1971 uk. 12-17 imeandikwa kuwa Mwandishi wa 1 Samweli hajulikani, pia hajulikani mwandishi wa kitabu cha 2 Samweli, 1 Wafalme, 1 Mambo ya Nyakati, Esta, Ayubu, Yona na Habakuki.Hali kadhalika mpaka leo kuna wasiwasi kama kitabu cha Waebrania kiliandikwa na Paulo au na mtu mwengine.Na Encyclopaedia Britannica inakiri kuwa mpaka hivi hatuna uhakika jinsi au wapi vitabu 4 vya Injili vilizuka. Kinyume chake Qur-an yote iliandikwa wakati wa uhai wa Muhammad (s.a.w) na ikahifadhiwa vifuani na mamia ya watu.

(5)Injili 4 zilizomo katika Agano Jipya siyo Injili zote zilizoandikwa. Zilikuwapo Injili nyingine nyingi. Ilifanyika Sinodi (mkutano wa wawakilishi wa makanisa) mwaka 325 ili kuamua Injili zipi zichukuliwe na zipi zikataliwe. Injili ya Barnabas ilikataliwa.Na katika historia ya Kanisa viko vitabu vilivyokubaliwa na baadaye kukataliwa na kinyume chake. Ni binaadamu waliokuja baadaye ndio waliokuwa na uwezo wa kuamua lipi liwe neno la Mungu na lipi lisiwe. Katika Uislamu hakukuwa na Ijitimai yoyote iliyokaa kuamua sura ipi iwe Qur-an ama isiwe.
 
Haikufundisha Mtume Muhammad quran kwa lengo la kurekebisha tabia za waarabu


(vii)Dai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur-an ili kuleta Umoja na Ukombozi wa Waarabu:

Wako baadhi ya watu wanaodai kuwa Muhammad(s.a.w) aliitunga Qur-an ili awaunganishe na kuwakomboa Waarabu. Dai hili pia halina nguvu kwa sababu zifuatazo:

Kwanza, lau dai hilo lingekuwa la kweli basi hapana shaka kuwa Qur-an ingetia msisitizo mkubwa sana katika mada ya umoja na ukombozi wa Waarabu. Kwa hakika hakuna aya hata moja katika Qur-an nzima inayolingania umoja na ukombozi wa taifa la Kiarabu. Itayumkinikaje basi Muhammad (s.a.w) atunge Kitabu kwa lengo la kujenga utaifa wa Waarabu na kusiweko katika kitabu hicho hata aya moja juu ya suala hilo?

Pili, msingi wa umma (taifa) unaofundishwa na Qur-an umejengwa juu ya itikadi ya haki na Qur-an inapinga hisia zote za utaifa kwa kufuata misingi ya rangi au kabila. Kila anayekubali itikadi ya Uislamu anakubalika katika umma wa Waislamu bila ya kujali rangi au kabila, au damu. Umoja uliodhihiri Arabia baada ya kushamiri kwa Uislamu ulikuwa umejengwa juu ya misingi ya Uislamu na siyo utaifa wa Kiarabu.

Tatu, lau umoja wa Waarabu ungekuwa ndilo jambo lililomsukuma Muhammad (s.a.w) hapana shaka angekubali kuwa mfalme wa Waarabu ili atumie fursa hiyo kujenga umoja wa taifa la Waarabu. Lakini tunaona alikataa ufalme pale wakuu wa Kikuraysh walipotaka kumrubuni ili aache kuutangaza Uislamu.

Nne, zipo aya katika Qur-an zinazolikanusha dai hilo. Aya mojawapo ya Qur-an yasema:
"Na (kumbuka) Malaika waliposema: Ewe Maryamu! Kwa hakika
Allah amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake wa ulimwengu (wote)." (3:42)
Aya hii inamzungumzia Maryamu, mama yake Nabii Isa (a.s). Maryamu alikuwa ni Myahudi.Na Wayahudi walikuwa wanadharau Waarabu kuwa ni taifa duni. Muhammad (s.a.w) alikuwa ni Mwarabu na Qur-an imeshuka kwa lugha ya Kiarabu na watu wa mwanzo kusomewa hii Qur-an walikuwa Waarabu.

Swali ni hili: Ikiwa Muhammad (s.a.w) alitaka kukuza hisia za utaifa wa Waarabu vipi basi aweke katika Qur-an aya hii inayomsifu mwanamke wa Kiyahudi kuwa amechaguliwa, ametakaswa na kutukuzwa na Allah(s.w) kuliko wanawake wote? Kwa nini asimsifie mama yake au mwanamke mwingine yeyote wa Kiarabu?
Aya nyingine ni hii ifuatayo:
Enyi kizazi cha Israili (Mayahudi)! Kumbukeni neema zangu nilizokuneemesheni, na nikakutukuzeni kuliko viumbe wengine. (2:47)
Mifano hii yaonesha kuwa haiingii akilini kuwa Muhammad (s.a.w) awe ametunga Qur-an kwa lengo la kuleta umoja na utukufu wa taifa la Waarabu halafu ndani ya hiyo hiyo Qur-an akasifia kwa sifa za kipeo cha juu kabisa watu walio maadui wa Waarabu!
 
Hija ya kuaga kwa mtume, na hutuba ya mwisho aliyotowa mtume katika hija


Mwaka mmoja baada ya msafara wa Tabuuk Bara Arab zima ilikuwa chini ya Dola ya Kiislamu. Kutokana na ujumbe wa Suratun- Nasr, sura ya mwisho kushuka, iliyoshuka baada ya Fat-h-Makka, na ukizingatia makundi ya watu kutoka makabila mbali mbali yalivyomininika Madinah kuja kusilimu na kujifunza Uislamu, baada ya msafara wa Tabuuk, ilikuwa wazi kwa Mtume(s.a.w) kuwa ujumbe wake umekamilika na kazi yake ya Utume imekaribia kwisha.
Itakapofika nusura ya Mwenyezi Mungu na kushinda. Na ukawaona watu wakiingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi. Basi hapo mtakase Mola wako pamoja na kumsifu, umuombe maghufira (msamaha); hakika Yeye ndiye Apokeaye toba. (110:1-3)
Mtume(s.a.w) hakuweza kushiriki kwenye Hija ya kwanza iliyofanyika 9 A.H. kutokana na shughuli nzito aliyokuwa nayo ya kupokea makundi kwa makundi ya makabila mbali mbali yaliyomiminika Madinah kuja kusilimu. Badala yake alimteua Abubakar kuongoza msafara wa Hija hiyo. Mwaka 10 A.H. Mtume(s.a.w) alinuia kufanya Hija kubwa na kuwajumuisha Waislamu wengi iwezekanavyo. Alituma wajumbe kwenda kwenye kona zote za Bara Arab kuwatangazia Waislamu kuwa waje kujiunga naye kwenye msafara wa Hija. Waislamu waliitikia wito na waliojiunga na msafara wa Hija ya Mtume kutoka Madinah ni 100,000 na jumla ya Waislamu waliosimama Arafa mwaka ule ni 120,000.
Hutuba ya Mtume(s.a.w) Katika Uwanja wa ‘Arafa, 9 Dhul-Hijjah 10 A.H.
Mchana wa 9 Dhul-Hijjah, Mtume(s.a.w.) akiwa juu ya ngamia wake alitoa hutuba ya kihistoria kwa mkusanyiko wa Waislamu laki moja na zaidi kama ifuatavyo:
“Sifa zote anastahiki Allah, Tunamshukuru na tunamtaka msaada na msamaha na tunatubu kwake, Tunajikinga kwa Allah (s.w.) kutokana na uovu wetu na kutokana na ubaya unaotokana na matendo yetu (maovu). Hapana awezaye kumpoteza aliyeongozwa na Allah na hapana awezaye kumuongoza aliyepotezwa na Allah. Ninashuhudia kuwa hapana Mola ila Allah pekee asiye na mshirika. Ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja na Mtume wake. Ninawausia enyi waja wa Mwenyezi Mungu, kumcha Mwenyezi Mungu na ninakusisitizeni kumtii Allah. Ninafungua khutuba yangu hii, na lile lililo zuri”.
“Enyi watu, sikilizeni ujumbe ninaokupeni. Sijui kama nitapata fursa nyingine ya kukutana na nyinyi baada ya mwaka huu.
“Enyi watu, hakika damu yenu (yaani uhai wenu), mali zenu na heshima yenu ni vitu vitukufu, katu visiharibiwe hadi mtakaposimamishwa mbele ya Mola wenu, kwani utukufu wa vitu hivyo ni kama ilivyo utukufu wa siku hii, wa mwezi huu na wa mji huu. Kwa hakika mtakutana na Mola wenu na atakuulizeni juu ya vitendo vyenu. Je, nimefikisha ujumbe? Ewe Mwenyezi Mungu shuhudia”.
“Hivyo, kila aliye na amana yoyote, hana budi kumrejeshea mwenyewe”
“Kumbukeni, hakuna atakayebeba lawama kwa kosa lolote isipokuwa yule aliyelitenda kosa hilo. Mtoto hawezi kulaumiwa kwa kosa la baba wala baba kwa kosa la mwanawe”.
“Enyi watu, yasikilizeni maneno yangu na yazingatieni. Fahamuni kuwa Muislamu ni ndugu wa Muislamu, na Waislamu wote ni ndugu wamoja. Si halali kwa Muislamu kuchukua chochote kutoka kwa nduguye Muislamu isipokuwa kile alichoruhusiwa. Hivyo msioneane. Yaa Allah, nimefikisha ujumbe?”
“Fahamuni, mambo yote ya ujahili yamewekwa chini ya nyayo zangu. Visasi vya damu vya zama za jahiliya vimeondolewa. Hakika, kisasi cha damu cha kwanza ninachokifuta ni kile cha Ibn Rabi’ah ibn Harith aliyelelewa na kabila la Sa’d na ambaye Wa-Hudhail walimwua.
Riba za kipindi cha jahiliya zimefutwa. Lakini mtapata mtaji wenu. Msidhulumu nanyi hamtadhulumiwa. Allah amekataza riba. Riba ya kwanza ninayoifuta ni ile ya Abbas ibn Abdul Muttalib. Imefutwa moja kwa moja.
“Enyi watu, mcheni Allah kuhusiana na wanawake. Mmewaoa kwa amana ya Allah na mnawaingilia kwa amri ya Allah.
Hakika mnazo haki kutoka kwao na wanawake wanazo haki kutoka kwenu. Haki zenu kwao ni kwamba wasimruhusu mtu yeyote kuvuruga vitanda vyenu na wasimruhusu mtu yeyote msiyemridhia kuingia katika nyumba zenu. Wakifanya hivyo Allah amewaruhusu nyinyi kuwakemea, kutengana nao vitanda na kuwapiga lakini siyo kwa nguvu, wakijirekebisha basi na wapewe kwa haki chakula chao na mavazi yao kutoka kwenu.
Yapokeeni kwa wema mafundisho haya juu ya wanawake. Kwani wao ni wasaidizi wenu. Hawamiliki kwa ajili ya nafsi zao chochote, nanyi hamwezi kumiliki chochote kutoka kwao kisichokuwa hicho. Wakikutiini basi kaeni nao kwa wema. Je, sijafikisha ujumbe?
“Enyi watu, msikilizeni na mtiini Amiri anayetekeleza kitabu cha Allah miongoni mwenu hata kama atakuwa ni mtuwa wa Kihabeshi”.
“Enyi watu, hakika Allah amekadiria kila mtu riziki yake. Wasia haujuzu kwa mrithi na wasia si halali ukiwa zaidi ya theluthi ya mali”.
“Mtoto ni wa kitanda cha halali na mzinifu arujumiwe. Mtu anayejinasibisha (ukoo wake) kwa asiyekuwa baba yake humshukia laana ya Allah, Malaika na watu wote. Allah hatakubali kutoka kwa mtu kama huyo toba wala amali njema. Enyi watu, shetani amehuzunishwa sana kwa kutoabudiwa tena katika hii nchi yenu. Lakini anatosheka na kule kutiiwa katika mambo ambayo nyinyi mnadhani ni madogo. Hivyo kuweni waangalifu sana katika dini yenu.
Kwa hakika nimekuachieni vitu viwili ambavyo iwapo mtavishika katu hamtapotea – Kitabu cha Allah na Sunnah za Mjumbe wake.
“Enyi watu, Jibril amenijia, amenisomea salaam kutoka kwa Mola wangu na amesema, Hakika Allah amewasamehe watu wa ‘Arafat na wa Ka’abah na amechukua dhamana ya kuwasamehe upungufu wao”.
‘Umar-ibnul Khattab akasimama na kuuliza: “Ya Rasulullahi, msamaha huo ni kwa ajili yetu sisi tu?” Akajibu: “Ni kwa ajili yenu na kwa ajili ya wale watakaokuja baada yenu hadi siku ya Kiyama”.
“Na mtaulizwa juu yangu, mtajibu vipi?” Wakasema: “Tunashuhudia kwamba umefikisha ujumbe, umetimiza wajibu wako na umetunasihi.”
Halafu akasema hali ya kuwa amekiinua kidole chake cha pete na kukielekeza mbinguni: “Ya Allah shuhudia, Yaa Allah, Shuhudia, Yaa Allah, Shuhudia”.22
Baada ya hutuba hii Mtume(s.a.w.) alimuamuru Bilal atoe adhana kisha wakaswali jamaa ya Adhuhuri pamoja na Asr kwa rakaa mbili mbili (Qasr). Baada ya swala Mtume(s.a.w.) alishushiwa Wahay unaokamilisha kazi yake na akasoma aya hiyo mbele ya watu wote waliohudhuria Hija mwaka ule:

“...........Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu, basi msiwaogope bali niogopeni mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe Dini yenu............” (5:3)
Pamoja na nasaha nzito alizotuachia katika khutuba yake ya kuaga, Mtume(s.a.w) alimalizia kwa kuwatumainisha Waislamu wa zama zote:
“Kwa hakika nimekuachieni vitu viwili ambavyo iwapo mtavishika katu hamtapotea – Kitabu cha Allah na Sunnah za mjumbe wake.”
 
Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake


Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s.a.w.) alishikwa na ugonjwa wa kuumwa kichwa na homa. Lakini muda wote alikuwa akijitokeza kufanya shughuli zake kama kawaida. Katika hali hiyo hiyo ya kuumwa, alikwenda Uhud na kuwaombea dua mashahidi waliozikwa mle. Pale alitoa khutuba ifuatayo:
“Siwahofii kuwa mtajihusisha na kuabudu masanamu baada yangu, lakini nahofia kuwa mtajihusisha sana na dunia kiasi cha kufikia hatua ya kuuana wenyewe kwa wenyewe. Kisha, mkishafanya hivyo, mtaishia kwenye maangamivu kama walivyoangamia wa kabla yenu”.
Mtume(s.a.w.) pamoja na maradhi yake aliendelea kuswalisha swala za jamaa msikiitni na bado alikuwa akitimiza ngono za wake zake wote tisa. Ugonjwa ulipozidi kushitadi, aliwaomba wakeze kuwa waje kumuuguza kwa Bibi Aysha(r.a.) palipo kuwa karibu na msikiti. Wakeze walikubali kwa moyo mkunjufu. Ugonjwa ulivyoendelea Mtume(s.a.w.) alizidi kuwa dhaifu na hatimaye alishindwa hata kuhudhuria swala za jamaa msikitini. Aliposhindwa kuhudhuria msikitini alitoa amri Abubakar awe anaongoza swala ya jamaa, alifanya hivyo kwa siku kadhaa.
Siku nne kabla ya kufariki kwake, Mtume(s.a.w.) alijisikia nafuu kidogo na akakoga kabla ya swala ya Dhuhuri. Baadaye alikuja msikitini akiwa amesaidiwa na watu wawili, Abbas(r.a.) na Ally(r.a.). Abubakar alikuwa anaendelea kuongoza swala kama kawaida. Alipomuona Mtume(s.a.w.) anakuja alianza kuondoka, lakini Mtume alimuambia abakie pale pale naye akakaa pembeni mwake. Baada ya swala alihutubia kama ifuatavyo:
“Allah amempa mja wake achague kati ya dunia na akhera. Akachagua akhera. Ninawausia, Enyi Waislamu (Muhajirina) muwe wema kwa Ansar. Hakika wametekeleza wajibu wao vizuri. Waislamu kwa ujumla wao idadi yao itaongezeka lakini Ansar watapungua na kuwa kama chumvi katika chakula. Zimeangamia umma zilizotangulia ambazo ziliabudu makaburi ya Mitume wao na ya watu wema. Ninawakatazeni kufanya hivyo. Nina deni kubwa (la Ihsani) kwa Abubakar. Kama ingekuwa nimfanye yeyote kuwa rafiki yangu, angalikuwa Abubakar, lakini uhusiano (udugu) wa Uislamu unatosha. Ee, binti yangu Fatimah na Ee, shangazi yangu mpendwa, Swafiyah, fanyeni amali kwa ajili ya akhera kwani sitaweza kuwasaidia chochote dhidi ya hukumu ya Allah.23
Hii ilikuwa khutuba ya mwisho ya Mtume (s.a.w.). Kisha ugonjwa ulishitadi. Alijisikia nafuu kidogo asubuhi ya Jumatatu ya mwezi 12 Rabi’ul-Awwal, 11 A.H, lakini ilipofika adhuhuri hali ilibadilika tena kuwa mbaya. Alikuwa akizimia kila baada ya muda mfupi. Hata alipokuwa katika hali hii ya sakaratul-maut, bado hakumsahau Mola wake. Muda wote alikuwa akisema “Nisamehe Bwana wangu”. Wakati wa alasiri alipokuwa anapumua pumzi za mwisho mwisho, alisikika kwa sauti ndogo akisema:
“Shikamana na swala na wafanyieni wema watumwa (wafungwa)”.
Palikuwa na beseni la maji lililowekwa karibu na Mtume (s.a.w.). Alikuwa akilowesha viganja vyake mara kwa mara kwenye maji haya na kufuta uso wake, huku akisema, “Enyi watu! Hakika kutoka roho kuna machungu makubwa”. Wakati huo aliingia mtu mmoja na mswaki mkononi mwake. Mtume akaashiria apewe mswaki huo. Alitafuniwa na Bibi Aysha, ambaye alimpakata mapajani mwake, na kumpa akawa anaswakia kidogo kidogo. Kisha akiwa ameashiria kwa kidole (cha shahada) na huku ametazama juu alisema mara tatu:
“Nakwenda kwa rafiki yangu mtukufu,
Nakwenda kwa rafiki yangu mtukufu,
Nakwenda kwa rafiki yangu mtukufu”.
Roho yake ilirudi kwa Bwana na Mola wake mtukufu wakati wa jioni ya Jumatatu ya mwezi 12 Rabi’ul Awwal, 11 A.H, Sawa na tarehe 8 Juni 632 A.D. Mtume(s.a.w.) alifariki akiwa na umri wa miaka 63. Mazishi yake yalifanyika siku iliyofuatia. Waliomwosha ni jamaa zake wa karibu – Fadhil bin Abbas, Ally bin Abu Talib na Usamah bin Zaid(r.a.). Kisha alizikwa kwenye chumba cha Bibi Aysha(r.a.) pale pale alipofia. Hivi sasa kaburi la Mtume(s.a.w.) limo ndani ya Msikiti wa Madinah.

“Ee Allah! Mrehemu Muhammad na wafuasi wa Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na wafuasi wa Ibrahim. Hakika wewe U-mtukufu na Msifiwa wa haki “Ee Allah! mbariki Muhammad na wafuasi wa Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na wafuasi wa Ibrahim. Hakika wewe U-mtukufu na Msifiwa wa haki.
 
Kizazi cha sasa hakikubali kukaririshwa mambo. Kwa aina hii ya kuhoji basi dini zote za ubabaishaji zitakuja kufutwa na vizazi vijavyo.
Qur'an haijaamuru wanaume kuoa wanawake wanne Bali imeweka limit kuoa mwisho wanne kwa wakati mmoja,ni ushauri na si lazima,msiwe mnarukia msiyoyajua,siku hizi watu wanachagua jinsia za watoto na wengi huchagua wa kiume,huko mbeleni patakua na uhaba wa wanawake,binaadam kuchamba kwingi watatoka na kinyesi mkononi
 
Hilo suala la kuoa wake wengi wanawake wengi hawalikubali, ila wanaume wa kiislamu wanalipenda kuliko hata kuswali..
unakuta mtu hafanyi ibada lakini kwenye kuoa Sasa wa kwanza.utasikia kuoa ni sunna waislam tumeruhusiwa😂😂😂
 
Hawajui kuwa wanazidi kuitangaza dini na kuleta 'curiosity' miongoni mwa watu kuifuatilia zaidi na hatimaye kusilimu.
Islam walioingia ukristo ni wengi sema kuna shida ya kuwa huru kusema sababu ya imani ya islam ni hatarishi sana.

Ni sawa na issue ya Ndoa, kinamama wengi wa Islam hawapendi ndoa ya wake wengi ila kwa sababu ya sheria ya dini basi wanaingia tu!.
 
Muwe mna soma imani zenu vyema msikurupuke kutukana na kuponda dini za watu. Hivi mkiulizwa kwenye bible wapi mmekatazwa kuoa wake wawili, mtaonesha aya gani.

Natoa changamoto kwayoyote mwenye kuweza kunieleimisha na kunipa maarifa aje na aya ama mstari kutoka kitabu chochote cha kikristu unahamasisha kuoa mke mmoja tuu.

Binafsi baada ya kujifunza nimekutana na mistari hii ambayo inahamasisha na kuonesha mfano wa wanaume kuoa wake zaidi ua mmoja.

Wamegharibi wamaeugharibu ukristu kwa kujaza maadili na utamaduni wao na bahati mbaya waafrika nao wamewafata kama walivyo kwa kujiita wastaarabu.

Hapa chini naweka alama ambazo zinahamasisha wanaume kuoa wake zaidi ya mmoja kutoka katika bible ya King James.


Bible Verses About Polygamy

Bible verses related to Polygamy from the King James Version (KJV) by Relevance - Sort By Book Order.


Exodus 21:10 - If he take him another wife; her food, her raiment, and her duty of marriage, shall he not diminish.

Matthew 25:1-46 - Then shall the kingdom of heaven be likened unto ten virgins, which took their lamps, and went forth to meet the bridegroom. (Read More...)

Deuteronomy 21:15-17 - If a man have two wives, one beloved, and another hated, and they have born him children, both the beloved and the hated; and if the firstborn son be hers that was hated: (Read More...)

2 Chronicles 24:1-3 - Joash was seven years old when he began to reign, and he reigned forty years in Jerusalem. His mother's name also was Zibiah of Beersheba. (Read More...)

Isaiah 4:1 - And in that day seven women shall take hold of one man, saying, We will eat our own bread, and wear our own apparel: only let us be called by thy name, to take away our reproach.

2 Samuel 12:8 - And I gave thee thy master's house, and thy master's wives into thy bosom, and gave thee the house of Israel and of Judah; and if that had been too little, I would moreover have given unto thee such and such things.

Judges 8:30 - And Gideon had threescore and ten sons of his body begotten: for he had many wives.

2 Chronicles 13:21 - But Abijah waxed mighty, and married fourteen wives, and begat twenty and two sons, and sixteen daughters.

Genesis 4:19 - And Lamech took unto him two wives: the name of the one was Adah, and the name of the other Zillah.

1 Chronicles 3:1-9 - Now these were the sons of David, which were born unto him in Hebron; the firstborn Amnon, of Ahinoam the Jezreelitess; the second Daniel, of Abigail the Carmelitess: (Read More...)

2 Chronicles 11:21 - And Rehoboam loved Maachah the daughter of Absalom above all his wives and his concubines: (for he took eighteen wives, and threescore concubines; and begat twenty and eight sons, and threescore daughters.)

Genesis 30:9 - When Leah saw that she had left bearing, she took Zilpah her maid, and gave her Jacob to wife.

2 Chronicles 24:3 - And Jehoiada took for him two wives; and he begat sons and daughters.

1 Chronicles 4:5 - And Ashur the father of Tekoa had two wives, Helah and Naarah.

Ezekiel 23:1-4 - The word of the LORD came again unto me, saying, (Read More...)

Genesis 30:4 - And she gave him Bilhah her handmaid to wife: and Jacob went in unto her.

2 Samuel 5:13 - And David took him more concubines and wives out of Jerusalem, after he was come from Hebron: and there were yet sons and daughters born to David.

1 Samuel 1:1-2 - Now there was a certain man of Ramathaimzophim, of mount Ephraim, and his name was Elkanah, the son of Jeroham, the son of Elihu, the son of Tohu, the son of Zuph, an Ephrathite: (Read More...)

1 Corinthians 7:1-5 - Now concerning the things whereof ye wrote unto me: It is good for a man not to touch a woman. (Read More...)

Numbers 12:1 - And Miriam and Aaron spake against Moses because of the Ethiopian woman whom he had married: for he had married an Ethiopian woman.

Deuteronomy 25:5-10 - If brethren dwell together, and one of them die, and have no child, the wife of the dead shall not marry without unto a stranger: her husband's brother shall go in unto her, and take her to him to wife, and perform the duty of an husband's brother unto her. (Read More...)

1 Kings 11:1-4 - But king Solomon loved many strange women, together with the daughter of Pharaoh, women of the Moabites, Ammonites, Edomites, Zidonians, and Hittites; (Read More...)

Song of Solomon 6:8 - There are threescore queens, and fourscore concubines, and virgins without number.

Deuteronomy 17:14-20 - When thou art come unto the land which the LORD thy God giveth thee, and shalt possess it, and shalt dwell therein, and shalt say, I will set a king over me, like as all the nations that are about me; (Read More...)

Titus 1:5-8 - For this cause left I thee in Crete, that thou shouldest set in order the things that are wanting, and ordain elders in every city, as I had appointed thee: (Read More...)
Itabidi na wewe unisaidie mafungu ya agano jipya uliyoyanukuu katika Mathayo, Tito na 1Wakorintho yanahasishaje uoaji wake wengi?
 
Back
Top Bottom