Kwa Tukio lililomtokea Mama yangu 2009, Nimetokea kuuheshimu sana Ukristo na Wakristo wote

Kwa Tukio lililomtokea Mama yangu 2009, Nimetokea kuuheshimu sana Ukristo na Wakristo wote

Nikipata tatizo kubwa, mfano changamoto ya magonjwa yaliyoshindikana hospital mtu wa dini akaniponya, nitaamini anachoamini.

Jumapili iliyopita ni kiwa kwenye gari moja, nilisikia shuhuda mbalimbali toka kwenye radio ya gati, sijui ilikua radio gani, ila kuna mchungaji ana kikombe kipya, kupitia kikombe kipya, watu hupata uzazi, kuona magonjwa, biashara yako kama huuzi unauza.

Ila kilichoniacha hoi simulizi ya Dada mmoja, aliejitambulisha kwa majina mawili ambayo waislamu hutumia, Yeye ni Dada lishe alikua hauzi ila tangu apate kikombe kipya, maji yake akaenda kumwagia sehemu ya biashara, wateja wote wanakula kwake tu, kwa wengine mpaka amalize yeye.
Nikatafari nikajiuliza inayofanya kazi ni nguvu ya Yesu au nguvu ya ulozi.

Kwa ninavodhanii sikuiz watumish wapo wengii...wapo piaaa wanaotumika na nguvu za giza kwa kivuli cha dini (hii sijamshtumu mtu ila wapo wengi tu) lakini pia waliotumwa kufanya kazi ya Mungu kiukweli pia wapo...My take...tuheshimu dini za wenzetu ata kama hatuamini katika dini izo....Simama na imani yako ila heshimu dini nyingine....Kudhihaki au kushtumu dini nyingine direct ni Dhambi ya kujitakiaa kabisa
 
Siku hizi kuna vijana hasa wa kiume wana makasiriko na wivu wa ajabu kabisa.

Mtu akipata mafanikio kifedha au kupona ugonjwa wanaumia sana mioyoni mwao.

Ila angekuwa mtu kaja hapa analia matatizo, huwezi ona mtu anasema ni uongo.

Ila ndio hao wanakuwa wa kwanza kumwambia tafuta hela huku wao wanalala kwenye sebule za shemeji zao.

Roho za kichawi kabisa.
Aseee n hatar,watu hawatak habar njema,huu n uchawi wa wazizi wazi.
 
Huyo ni Muislam na mara nyingi ana kashfu Ukristo naye ni kupinga kila kitu. Dunia ni ngumu sana hii na kuna vitu kwa jinsi ya kibinadamu haiwezekani na hadi madokta wanakuambia kama una Mungu muite akusaidie. Nimeshuhudia kwa macho yangu mambo mengi sana Mungu akitenda pitia maombezi. Dunia hii watu wana shida sana kama.wewe u mzima shukuru Mungu na usilete ujuaji.
Halafu utasikia uislamu ni unyenyekevu ila matendo yao sasa!
 
Mwenyewe siamini hizo mambo ila miaka ya 2000 kuna mama jirani yetu sauti yake ilipotea kimuujiza. Yaani alikua mtu anayeweza kuongea then sauti ikapotea Kwa miaka...siku moja kakobe akaja kwenye mkutano wa injili yule mama aliongea. Na tunajua alikua na Hilo tatizo kwa miaka mingi.... Hivi vitu vinachanganya sana
Simlizi za kiimani hamna ugonjwa unao itwa sauti kupotea hizo zote ni comedy za wafuasi wa hizo imani kuvutia wengine
 
Kumetokea kundi la vijana ambalo kazi yao ni kupinga chochote kinachoelezea kuhusu Mungu. Sasa kama wao wanapinga, watuache sisi tunaofuatilia na kukiri matendo ambayo Mungu ametutendea wao waendelee na threads zingine.
Wengine wachaw humu ata usihangaike nao,zikija mda ya kipuuz wako vzur kwel kuchangia.Ila mada za maana au Mambo ya Mungu wanajua kupinga Kama Wendawazim flan ivii,mm naona nguvu ya Mungu ina wachoma.
 
Kitendo cha kuhuusisha uislam kwenye hiyo hadithi yako tiyari kunaharibu maana ya huo ushuhuda wako na kuonekana ni uongo.
Kingine huwezi kuwa mwislam alafu usijue nn maana ya kafri neno kafri sio tusi wala kashifa bali neno kafri ni neno la kiarabu lenye maana ya wapingaji kwa kiswahili sasa hapo kuna tusi gani?, Kwa hiyo kumbe chadema wakiitwa wapinzani hayo ni matusi na kashifa?
Ww ni mrokole uliye changamka ambaye umetunga uongo ili kuleta ubishani wa kidini humu.
Mwisho unasema eti heshimu dini ya mwingine ww ungekuwa na heshima na dini za watu usinge uhusisha uislam kwenye huu utopolo wako, nyinyi mnajisikia vibaya kuitwa makafri ila nyinyi mnapo shinda makanisani kwenu mkiwananga waisilam kuwa ni wafuga majini mnaona ni sawa.
Muongo mkubwa lengo lake lilikua kudhalilisha uislamu tu hamba jingine, kulikua na haja gani kutaja dini nyingine, watu kama hao wana chuki na dini ya uislamu bila kuitaja taja hawapati usingizi.
 
Kwa ninavodhanii sikuiz watumish wapo wengii...wapo piaaa wanaotumika na nguvu za giza kwa kivuli cha dini (hii sijamshtumu mtu ila wapo wengi tu) lakini pia waliotumwa kufanya kazi ya Mungu kiukweli pia wapo...My take...tuheshimu dini za wenzetu ata kama hatuamini katika dini izo....Simama na imani yako ila heshimu dini nyingine....Kudhihaki au kushtumu dini nyingine direct ni Dhambi

Simlizi za kiimani hamna ugonjwa unao itwa sauti kupotea hizo zote ni comedy za wafuasi wa hizo imani kuvutia wengine
Mimi naamini Mungu, anaponya kwa kumuomba au kuombewa, ila mpaka uwe unaamini Mungu, usiwe Muamini Miujiza.
 
Kataa matapeli 🤣🤣🤣hakuna shuhuda za kweli maana tunao wengi hapa tunachangia pesa za matibabu ..
Sawa, naomba nijifunze, je mungu unayemuamini hawezi okoa nankuponya wajoli wake? Je vipi kuhusu shuhuda za Sharif Majini na mashehe wengine zenyewe zipoje? Je allah hawezi tumia wanaomuamini kuponya hata mdondo kwenye kuku?
 
Kwa ninavodhanii sikuiz watumish wapo wengii...wapo piaaa wanaotumika na nguvu za giza kwa kivuli cha dini (hii sijamshtumu mtu ila wapo wengi tu) lakini pia waliotumwa kufanya kazi ya Mungu kiukweli pia wapo...My take...tuheshimu dini za wenzetu ata kama hatuamini katika dini izo....Simama na imani yako ila heshimu dini nyingine....Kudhihaki au kushtumu dini nyingine direct ni Dhambi ya kujitakiaa kabisa
Kama unakili kuna watumishi wengine wanatumia mpaka ulozi, kuna tofauti gani na nilichokiandika.

NIkiandika mimi siheshimu dini za watu, ila ukiandika wewe sawa tu.
 
Sawa, naomba nijifunze, je mungu unayemuamini hawezi okoa nankuponya wajoli wake? Je vipi kuhusu shuhuda za Sharif Majini na mashehe wengine zenyewe zipoje? Je allah hawezi tumia wanaomuamini kuponya hata mdondo kwenye kuku?
Hakuna shekhe majini ,kqtaa utapeli 🤣🤣
 
Ni meishia kusoma pale nilivo ona kwamba ulipeleke maombini, ni ka kuona kijana mpuuzi, ingekua hivo hata kwenye theater za hospitali kungekua na maombezi tu,........mtoto wakiume anae amini maombezi ya walokole ana vyashilia vya jinsia ya kike. "Soul diseases are treated spiritually and physical diseases are treated biologically" don't mixup things plz nyie walokole mna kua na wrong absolute belief kitu ambacho ni hatari katika jamii zetu za kiafrica
Uache ujinga huu.
Hata Yesu hakuponya watu wote bali waliponywa waliotaka kuponywa.

Yesu huponya na huponya wenye imani.
Ukubali ukatae Yesu huponya.
 
Sawa, naomba nijifunze, je mungu unayemuamini hawezi okoa nankuponya wajoli wake? Je vipi kuhusu shuhuda za Sharif Majini na mashehe wengine zenyewe zipoje? Je allah hawezi tumia wanaomuamini kuponya hata mdondo kwenye kuku?
Mungu anaponya kwa maombi, ila hao akina Sharif majini ni aina ya hao wachungaji wanauza mafuta fulani, maji kikombe cha pili.
 
Ikiwa ushuhuda wako ni wa kweli, basi kipo kitu Mungu amepanda ndani yako kwaajili yake, Ndio maana sio wagonjwa wote wanapona ila akapona mama yako na hilo likakuingia moyoni sana, Basi nakuombea kwa Mungu upate nafasi wakati mwingine ya kusikiliza mafundisho kuhusu Yesu, pamoja na kwamba una heshimu ila vema ukapiga hatua mbele tena kujua habari zaidi za Yesu Kristo. Usiogope kabisa kuhusu dini yako hata kama ikitokea ukabadili basi utabadili kwa maamuzi sahihi ambayo utakuwa nayo kwa muda huo. Mwenyeenzi Mungu akubariki sana.
 
Back
Top Bottom