Nikipata tatizo kubwa, mfano changamoto ya magonjwa yaliyoshindikana hospital mtu wa dini akaniponya, nitaamini anachoamini.
Jumapili iliyopita ni kiwa kwenye gari moja, nilisikia shuhuda mbalimbali toka kwenye radio ya gati, sijui ilikua radio gani, ila kuna mchungaji ana kikombe kipya, kupitia kikombe kipya, watu hupata uzazi, kuona magonjwa, biashara yako kama huuzi unauza.
Ila kilichoniacha hoi simulizi ya Dada mmoja, aliejitambulisha kwa majina mawili ambayo waislamu hutumia, Yeye ni Dada lishe alikua hauzi ila tangu apate kikombe kipya, maji yake akaenda kumwagia sehemu ya biashara, wateja wote wanakula kwake tu, kwa wengine mpaka amalize yeye.
Nikatafari nikajiuliza inayofanya kazi ni nguvu ya Yesu au nguvu ya ulozi.