Kwa uchafu wa mama ntilie wa Tanzania, Bibi na Bwana Afya wako likizo?

Kwa uchafu wa mama ntilie wa Tanzania, Bibi na Bwana Afya wako likizo?

Kwa kipato gani wanachoingiza hadi wabadilike? Wangapi wanahela ya kwenda kula sehemu nzuri?

Wakikosa wateja watajirekebisha. It's demand and supply.

Nipo around mazee.
 
Ukiwaandekeza unapotea wale usiwaone vile wanamajumba ambayo mfanya kazi wa serikali hadi ana staafu bado hawezi kujenga wewe wadharau tu
Mama Lishe tunaishi nao, maisha yao tunayajua.

Wapo wachache waliofanikiwa lakini walio wengi wanatafuta Kodi ya nyumba tu.
 
Hotel na migahawa mingi hupika vyakula kwa njia ambayo si safi.
Vyakula hujenga utando ila hawamwagi sababu ya hasara

Nyanya wanaenda nunua masaro, wao wanazisaga na kutupia

Mchele wananunua wa hali ya kawaida

Maji watumiayo si masafi


Kwenye juisi, ukienda sokoni kuna maembe na matunda wanayaita ya juisi, yale yameoza kwa asilimia 50


Nyama ambayo hutumika ni nyama ambayo ni ya hali ya chini

Mboga za majani nazo chafu
 
Kwa kipato gani wanachoingiza hadi wabadilike? Wangapi wanahela ya kwenda kula sehemu nzuri?

Wakikosa wateja watajirekebisha. It's demand and supply.
Kwasababu kanuni za Afya zinaanza na:
  • Provisions
  • Food handlers Medical check up ( interval of 6 months )
  • Garments ( Apron, Hairnet )
  • Ndoo ya kunawia na sabuni ya MAJI.

Sasa Mama Lishe mwenye mtaji wa elfu 50 ataweza kufanya ghafla tu?
 
Kati ya watu wanaojua kulalamika ni mama ntilie yaani wakipigwa faini au kufungiwaa biashara wataliaaa weee na kutoa kila laaana na lawama wakati wao ndio wenye makosa.
Watajiita wanyonge ndio maana wanaonewa
 
Nenda kale chakula hotelini huku kwa mama ntilie tuachie sisi wenywe.

Au kapike/kapikiwe kwako

Kama huna pesa njoo tujumuike kwa mama ntilie lakini acha unoko wako
 
Siyo wote mkuu ni baadhi ndiyo wanakasumba hiyo, ila tambua mkuu kuna maprofessir waliosomeshwa na haohao unaowaita wachafu.

Ila tambua wanatusave sana mabachela, ukute mtoa mada ameoa na anafamilia yako lakini bado unafanya fekenyuzi za kuwaharibia watu biashara zao,
 
Hivi hawa Bibi na Bwana afya wapo?
Migahawa ya Tanzania ni michafu sana na hao wapishi wenyewe ni wachafu mno.
Hatukatai haki za watoto lakini kwa nini mtu mwenye mtoto mdogo asiejiweza aruhusiwe kufanya biashara ya chakula?
Mtoto mdogo anakunya, mama ntilie anamtawaza muda huohuo keshaenda kupakua chakula tena hajanawa na sabuni hapo ikitokea magonjwa ya milipuko inakuaje kwa mfano.
Vitu vingine tungeni sheria ndogo ndogo zinazoambatana na adhabu, piteni mara kwa mara kukagua usafi mkikuta dosari waandikieni faini hiyo itasaidia kuboresha huduma,
Bibi afya na Bwana afya nadhani ni kundi la watu wasio na kazi ndio maana ni walevi sana , hata kukagua mazingira ya makazi usafi wake ukoje hakuna unakuta mapori kwenye makazi ya watu, pita piga faini uone kama hawatofanya usafi huko majumbani.

Kiukweli inasikitisha sana asee,shida kubwa ni umasikini na siasa za kipuuzi ndio zinafelisha hii nchi.
 
halafu cha ajabu chakula chao kama wali wanafunikia nailon ili iwive wakati nailon kemikali yake inaingia kwenye wali kwa ajili ya lile joto na husababisha cancer kwa walaji ndio maana cancer imekuwa nyingi, mabibi afya wapo mabwana afya wapo wao wanakimbilia hoteli kubwa ili kukagua wapate rushwa
 
Kufuata kanuni za Afya ni hulka binafsi.

Mama Lishe hawako kwenye mfumo rasmi wa biashara, ni Kama wamachinga na hivyo control yao ni ngumu.

PILI, Mama Lishe hawatafuti utajiri.

They are just fighting to survive, kwahiyo ubinadamu lazima utumike.

Mama Lishe mtaji wake kiasi gani, mpaka umpige fine, elfu 50?

kwahiyo watu waumie kwa sababu ya mitaji yao midogo waachiwe tu na uchafu wao
 
Kachumbari inavyoandaliwa utashangaa.imagine! Anamtawaza mtoto na kucha zake ni ndefu bila kunawa kwa kutumia sabuni, anaadaa kachumbari!!
 
halafu cha ajabu chakula chao kama wali wanafunikia nailon ili iwive wakati nailon kemikali yake inaingia kwenye wali kwa ajili ya lile joto na husababisha cancer kwa walaji ndio maana cancer imekuwa nyingi, mabibi afya wapo mabwana afya wapo wao wanakimbilia hoteli kubwa ili kukagua wapate rushwa

Inasikitisha sana,kuna migahawa ukila chakula lazima umeze fragly ili kujinusuru na kuhara.
 
Inashangaza sana Mama ntilie wakati wa kuweka vitafunwa (Maandazi, chapati, kachori n.k) kwenye kabati anashika na mkono

Afu mteja akija anamtolea akiwa amevaa mfuko mkononi

Huu ni ujinga uliopitiliza

Yan behind the scene huwa wanafanya mambo ya hovyo mnoo
 
Umaskini, Uchafu na Uholela ni dugu moya!

Hivi ninini kigumu katika kusafisha mazingira yawe masafi either biasharani, au nyumbani?

Mtu hata kama vyombo vyako ni vya plastic safisha vizuri na sabuni na maji ya moto vinatakata, futa meza, kausha paka dawa ya kuua nzi.
 
Back
Top Bottom