Kwa uchafu wa mama ntilie wa Tanzania, Bibi na Bwana Afya wako likizo?

Vyombo hawaoshi vizuri wanalipua tu Kwa kudumbukiza kwenye Maji na kutoa !

Ni hatari sana kula kwa mama lishe pamoja na bei zao kuonekana na afadhali lakini mtu akipata magonjwa kujitibia ni gharama kubwa sana.
 
Hivi hawa Bibi na Bwana afya wapo?
Migahawa ya Tanzania ni michafu sana na hao wapishi wenyewe ni wachafu mno.
Hatukatai haki za watoto lakini kwa nini mtu mwenye mtoto mdogo asiejiweza aruhusiwe kufanya biashara ya chakula?
Mtoto mdogo anakunya, mama ntilie anamtawaza muda huohuo keshaenda kupakua chakula tena hajanawa na sabuni hapo ikitokea magonjwa ya milipuko inakuaje kwa mfano.
Vitu vingine tungeni sheria ndogo ndogo zinazoambatana na adhabu, piteni mara kwa mara kukagua usafi mkikuta dosari waandikieni faini hiyo itasaidia kuboresha huduma,
Bibi afya na Bwana afya nadhani ni kundi la watu wasio na kazi ndio maana ni walevi sana , hata kukagua mazingira ya makazi usafi wake ukoje hakuna unakuta mapori kwenye makazi ya watu, pita piga faini uone kama hawatofanya usafi huko majumbani.
Shida yenu mnataka kumla na mama Lishe hasa akiwa na chura ni shida kubwa. Uchafu una uhusiano wa karibu na umaskini, unataka chakula cha buku jero, mboga tatu.🥳
 
Sisi huku Ruangwa Mama Ntilie wetu ni wasafi. Sijajua huko kwenye jiji lenu lakini sisi huku tunaenjoy[emoji847][emoji847]
 
Wali wanapoupalia wwnaweka lailoni juu kisha wanaweka sinia la moto wa mkaa.

Imagine moto unayeyusha lile lailoni kisha watu wanakula malailoni [emoji24] sijui madhara ya magonjwa wanayaju?!
Hapana napinga. Nailoni huwa haiyeyushwi.
 
Hivi hawa Bibi na Bwana afya wapo?
Migahawa ya Tanzania ni michafu sana na hao wapishi wenyewe ni wachafu mno.
Hatukatai haki za watoto lakini kwa nini mtu mwenye mtoto mdogo asiejiweza aruhusiwe kufanya biashara ya chakula?
Mtoto mdogo anakunya, mama ntilie anamtawaza muda huohuo keshaenda kupakua chakula tena hajanawa na sabuni hapo ikitokea magonjwa ya milipuko inakuaje kwa mfano.
Vitu vingine tungeni sheria ndogo ndogo zinazoambatana na adhabu, piteni mara kwa mara kukagua usafi mkikuta dosari waandikieni faini hiyo itasaidia kuboresha huduma,
Bibi afya na Bwana afya nadhani ni kundi la watu wasio na kazi ndio maana ni walevi sana , hata kukagua mazingira ya makazi usafi wake ukoje hakuna unakuta mapori kwenye makazi ya watu, pita piga faini uone kama hawatofanya usafi huko majumbani.
bwana afiya awezi fanya lolote akijalibu mbunge diwani waache wapiga kula wangu hivio hivio kwa boda wasio na leseni nchihi mtaalamu hana sauti mwenye sauti mwana siasa
 
Migahawa ya Tanzania ni michafu sana na hao wapishi wenyewe ni wachafu mno.
Hatukatai haki za watoto lakini kwa nini mtu mwenye mtoto mdogo asiejiweza aruhusiwe kufanya biashara ya chakula?
Mtoto mdogo anakunya, mama ntilie anamtawaza muda huohuo keshaenda kupakua chakula tena hajanawa na sabuni hapo ikitokea magonjwa ya milipuko inakuaje kwa mfano.
Hivyo vyeo vingefutwa tu vimejaa rushwa kibao
 
Mama Lishe hawako kwenye mfumo rasmi wa biashara, ni Kama wamachinga na hivyo control yao ni ngumu.
Kwahiyo waendelee kuua watu kwa kuwalisha sumu, niliteegemea Mamlaka husika ziwekeze kwenye kutoa elimu kwa walaaji kususia vyakula vinavyopikwa kinyume na kanuni za afya
 
Acha kula huko nachojua hata wateja wao n watu wa hali ya chini na kwao hayo mazingira mabovu sio issue kabisa
 
Kwahiyo waendelee kuua watu kwa kuwalisha sumu, niliteegemea Mamlaka husika ziwekeze kwenye kutoa elimu kwa walaaji kususia vyakula vinavyopikwa kinyume na kanuni za afya
Mimi nimesema waendelee kulisha watu sumu?
 
Hapana napinga. Nailoni huwa haiyeyushwi.

Unapinga kuwa lailoni ikiwekwa juu ya sufuria na kupalia wali kwa mkaa wa moto haiyeyuki? Au ?

Kwa hiyo unategemea kuyeguka hadi uone Kwa macho uji uji au kwa microscope ?

Kwa unazani kuwa chemicals zote za hatari unaweza kuziona kwa macho yako?

Kwa hiyo Maabara hazihitajiki tena kwa uchunguzi?
 
Peleka hizo microscope kwa mama ntilie wawe wanachunguza kwanza kama wali una plastic.
 
Unaijua rushwa iliopo tz ww hao watu wanapita wakiwa na njaa wanakusanya chao wanasepa. Wife ashafungua biashara ya chakula alijitahidi usafi na muonekano wa wafanya kazi ila walikua wakija hawakosi dosari mwishoe yule bibi aliniambia jiongeze tusikusumbue niliwatafutia 50k japo wife alikua haelewi kwann nafanya vile ila walipokamata hiyo hela sijuwaona tena mpka tunahama jengo sijawahi muona na kibaya wanakuaminisha kabisa hapa hatukatizi jitahidi usafi sasa hapo usitarajie kama mtu ni mchafu awe msafi na faini ni faida ya serikali yule anaetoza anajengewa kinyongo na faida hapati hivyo wanaona bora wabebe 5k zenu kila wakija kuliko 50k iende serikalini
 
Kwahiyo waendelee kuua watu kwa kuwalisha sumu, niliteegemea Mamlaka husika ziwekeze kwenye kutoa elimu kwa walaaji kususia vyakula vinavyopikwa kinyume na kanuni za afya
Mtu ahangaike kutafuta pesa na bado asuse chakula cha bei nafuu cha msingi kama unajijua unataka usafi kale serena kule kuna ma QC usijidanganye kwamba serikali itasema watu wasuse na wakasusa kweli uzuri wa bongo unapata ulicholipia ukilipia serena utapata vya serena ukilipia latifa bokoboko utapata vya pembeni ya mtaro nzi debe funza kisado
 
Yaani kwangu mimi fundi umeme ninayeweza kuingia mpaka sehemu za jikoni/maandilizi ya vyakula vya migahawa mikubwa na baadhi ya hotel.Nitaendelea kula kwa amani na uhuru kwa mamanitilie anayepika huku naona kuliko huko migahawa mikubwa na hotels.
 
Baadhi ya mabibi Afya wa wilaya ya Ilala wako bize na biashara zao. Si ajabu na wao wakapata kipindupindu wakiwa bize kwenye kuchuuza bidhaa zao. Inasikitisha.
 
Unaijua rushwa iliopo tz ww hao watu wanapita wakiwa na njaa wanakusanya chao wanasepa. Wife ashafungua biashara ya chakula alijitahidi usafi na muonekano wa wafanya kazi ila walikua wakija hawakosi dosari mwishoe yule bibi aliniambia jiongeze tusikusumbue niliwatafutia 50k japo wife alikua haelewi kwann nafanya vile ila walipokamata hiyo hela sijuwaona tena mpka tunahama jengo sijawahi muona na kibaya wanakuaminisha kabisa hapa hatukatizi jitahidi usafi sasa hapo usitarajie kama mtu ni mchafu awe msafi na faini ni faida ya serikali yule anaetoza anajengewa kinyongo na faida hapati hivyo wanaona bora wabebe 5k zenu kila wakija kuliko 50k iende serikalini
Hizi mamlaka zote ni rushwa tupu.
 
Back
Top Bottom