Kwa ufupi Hayati Magufuli aliwachukia watumishi wa umma

Kwa ufupi Hayati Magufuli aliwachukia watumishi wa umma

Mkataba wa Ajira yako unakwambia kila mwaka utaongezwa salary?
Ndio unasema hivyo! Sema kwasababu wewe huna uelewa wowote na ajira za serikali, ila umeambiwa tu uje upambanie legacy ndio ukaja kichwa kichwa kama hivi...
 
Alikuchukia wewe kwa kuwa ulikuwa na cheti fake lakini sisi watumishi wa vyeti original hatukuwa na shida naye kabisa.
Hashangai balozi mbelwa kairuki yuko China mkewe waziri bi Angela kairuki yuko Tz na siku zinasonga since sherehe za Beijing kwa akina mama, hili suala ni zaidi ya JPM (hasa hapo alipohusisha mambo ya uhamisho/wanandoa kuwa mbali), maadili yatamomonyoka hadi kama... R. I QEE JPM
 
Ajira ya 2014 wapo waliopanda 2019 tena mwaka huu 2023 wamepanda tena
Watu wasichikijua mishahara ilikuwa inaongezwa Kimya kimya na madaraja watu walipanda.

Kama mtu alikuwa ni kiaze kama mleta Uzi hawakufikiriwa kabisa
 
Watu wasichikijua mishahara ilikuwa inaongezwa Kimya kimya na madaraja watu walipanda.

Kama mtu alikuwa ni kiaze kama mleta Uzi hawakufikiriwa kabisa
Kwahiyo iliongezwa kwa wachache ambao walikuwa ndugu zake na hayati tu sio
 
We boya nna uwezo wa kukufuga ww pamoja na nzengo yako yote! Halaf naish kwa jasho langu sijawah kumnyima au kumnyanganya mtu! Jaribu kujifunza kutoka kwa wenzako waliokuzidi maarifa! Umma sio serikali kama unavyojilisha materia feki!
Umezungukwa na ndugu zako masikini wengi sana,nakushauri aanza nao kuwasaidia,acha kujimwambafy kwenye mitandao masikini wwe!!
 
Ebu fikiria, mtu kama wewe ndiyo matunda ya watumishi tulio nao! Hiyo ni ishara tosha kabisa kuwa hakuna ufanisi wowote huko makazini, watu wanafanya kazi tu bora liende.
Umeacha alama gani duniani wewe,kuwadharau watumishi wa umma ni alama tosha kwa wapumbavu.
 
Kwa ufupi sana JPM alitamani kuona Wafanyakazi nchi hii wanaishi kama mizuka, mizimu au mazombi.. hakuna ajuae ni kosa Gani haswa aliwahi kufanyiwa na watumishi wa nchi hii, yapo mambo ambayo mama amejitahidi angalau kuyarudisha lakini mengine inabidi mchakato au hata hekima tu, ngoja niwaonyeshe Machache,

1. Kupandisha Madaraja , kwa Mfano wafanyakazi walioajiriwa mwaka 2014, haikujulikana ni LINI, wangepanda Madaraja! Imagine Miaka 7, na hatimaye wakaja kupanda mwaka 2021! Baada ya mama kuingia madarakani! Just imagine

2. Nyongeza za kawaida za Kila mwaka ambazo zipo kisheria kabisa yeye alifuta! Tena Bila shaka hakutaka kusikia, haijafahamika mara moja ni kwanini!

3. Kazi maalum kwa walimu Mfano (kusahihisha mitihan ya taifa)
Walimu waliokuwa wakifanya Kazi iyo kabla ya JPM kuingia madarakani, mbali na kwamba walilipwa vizuri pia walikula chakula kizuri, lakini pia waandaaji walifanya kama kuwamotisha walimu kwa kuwapa kama utalii wa ndani, maana yule wa kigoma angeenda Tanga wa Tanga akaenda Tabora huko n.k...

Hii iliwafanya baadhi ya watu kufurahia na angalau kubadilisha mazingira!
Sasa Mzee baba alivyoingia akapiga marufuku akisema wa Tabora abaki Tabora na WA Mwanza abaki mwanza! Hakuishia hapo na malipo akapunguza! Akidai walimu hiyo ni kazi Yao, hivyo ikibidi wasilipwe chochote! Na Sasa kuanzia pale kazi ikawa Haina morali kwani kazi kubwa, malipo kidogo na masimango juu.

Mpaka tunakwenda mitamboni haikujulikana sababu haswa kwanini Mzee baba aliwachukia wafanyakazi kiasi hiki.
Hii inaonyesha wewe ni mmojawapo wa watu ambao hawakuwahi kupata kabisa nafasi ya kuweza kumuombea JPM alipokuwa yupo madarakani.

Kama una uelewa mpana wa mambo na huwa unayaangalia na kuyachambua vizuri, basi safari hii ninakuomba sana umuombee Mama; ili huko mbele ya safari, usije ukaingia kwenye mtego wa kumporomoshea lawama ambazo siyo zake
 
Sale wanao msifia Magufuli,wawe tayari kusikia na upande wa pili.
 
Mnaosema eti wanaohoji walikuwa na vyeti feki,

Mmejiuliza baada ya kuwaondoa hao mafisadi na wenye vyeti feki,
Hao waliobaki ambao wana vyeti original pamoja na wale ambao hawana ufisadi wowote aliwafanyia Nini?
Zaidi ya kuwakalisha Miaka 7 Bila chochote?
Yaani ilifikia hatua hata mtumishi ukivaa ukipendeza unaelekea kazini,
Mzee ananuna.,

Kwakweli acha Mungu aitwe Mungu
Yule alikuwa shetani kweli kweli
 
Back
Top Bottom