Kwa Ukweli huu shetani ni tapeli na uwezo wake ni mdogo sana

Kwa Ukweli huu shetani ni tapeli na uwezo wake ni mdogo sana

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
2,536
Reaction score
4,621
Hapo vip!!

Nimekuwa najiuliza swali dhidi ya uwezo na mapenzi ya shetani kwa wafuasi wake najikuta naona shetani ni tapeli na muongo.

Najiuliza kama kweli shetani anauwezo wa kushindana na Mungu.

Mbona Mungu baba Jehova(bwana wa Majeshi au bwana wa mabwana)alivyoamua kuwapiga kiberiti wale watu waliokuwa wanampendeza shetani kipindi cha sodoma na gomoro na kushusha garika kipindi cha nuhu kwa kile kizazi kilichokuwa kinafanya ushetani mbona shetani hajajitokeza kuwatetea watu wake?

Kama kweli anauwezo wa kushindana na Mungu mbona hajajitokeza kuwatetea hata kwa sekunde moja?

Shetani alipo mdanganya Eva akala tunda,Mungu Jehova aliamua kumlaani Adam na Eva kwa adhabu ya kifo...Sasa kama shetani anauwezo na mkweli kuliko Mungu kwanini alishindwa kuuzuiya adhabu ya Mungu mpaka sasa..na watu wanakufaa kama kawaida kwa kauli moja tu tena ya siku moja ya Jehova Adonai, maana yake ni kwamba Mungu (Jehova), uwezo wake ni mkuwa sana na hauwezi kuulinganisha hata kidogo na ya huyu tapeli shetani

Lingine ni kwamba Mungu amekuwa akitoa neno moja tu linakuwa hai milele na milele mfano, endeni mkazaliane,adhabu ya kifo, uumbaji wa mambo yote kwa maneno na imekuwa kweli.

Shetani kama anauwezo kweli mbona hajawahi kutoa kauli inayohishi katika Dunia..maneno yake hayana mamlaka na uwezo wowote..hivyo basi kwa ushahidi huu shetani ni kiumbe chenye uwezo mdogo sana kuliko hata mwanadamu aliyepewa kipao mbele na Mungu..inashangaza kumuona mwanadamu akifuata kiumbe hichi,bora mtu afuate ila sio mwanadamu ni aibu.
 
Kimsingi kazi ya shetani ni kutuchonganisha na Mungu kwa hiyo hayo yalioyo tokea ndio lengo hasa la shetani kwa hiyo hapo alfanikiwa.

Shetani hanufaiki na madhambi yeyote ila hushawishi watu wayafanye ili kumkera Mungu.

Kwa hiyo shetani hana wema na binadamu na yaliyotea hapo juu ni ushindi mkubwa kwake mpaka sasa tunayo laana.

Hivyo usimchukulie poa bwana yule.
 
Shetani mshamba tu,andiko lazima litatimia juu yake.
Kimsingi kazi ya shetani ni kutuchonganisha na Mungu kwa hiyo hayo yalioyo tokea ndio lengo hasa la shetani kwa hiyo hapo alfanikiwa.

Shetani hanufaiki na madhambi yeyote ila hushawishi watu wayafanye ili kumkera mungu.

Kwa hiyo shetani hana wema na binadamu na yaliyotea hapo juu ni ushindi mkubwa kwake mpaka sasa tunayo laana.

Hivyo usimchukulie poa bwana yule.
 
Hivi kwanini Mungu alimuumba Shetani?

kama yeye anajua mwanzo na mwisho wa kila alichokiumba, je hakujua Malaika wake watakuja kumsaliti?

isitoshe baada ya ysaliti, bado anawasiliana na Shetani na anamwagiza akawatese wanadamu😅😅

Mungu na Shetani wana njama gani dhidi yetu binadamu?
 
Hili swali la mwisho binafsi nimekuwa najiuliza mara nyingi nakosa jibu. Ni kama mpango uliopangwa dhidi ya mwanadamu. Kwasababu Mungu anauwezo wa kumuondoa huyu mtesi katika ya watoto wake.
 
Embu futa kauli yako.kwanza shetani unamjua kwa kazi yake ilivyo.
Shetani hana future kwa mujibu wa vitabu vyote vya dini,anaishia katika moto wa jehanam...namlango wa msamaha kwake umefungwa..case closed.

Kama anauwezo akatengeneze ulimwengu wake aachane kushindana na Mungu ila anaishi ndani ya vyote vilivyoumbwa na Mungu(Jehova) kwa mazingira haya shetani amejichanganya.
 
Mungu ndio Shetani
Na Shetani ndiye Mungu.

Dunia ni ya Shetani
Ndio makazi yake
Ndio mtawala
 
Lengo la shetani ni kutugombanisha na Muumba wetu baada ya hapo hukaa kando na kufurahia.
 
Shetani huwa anapiga, ukipokea umeliwa 😀😀😀

MATHAYO 4: 5-10

5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,
6 akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9 akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
11 Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.
 
🙏,hii ilikuwa ni shule tu aliyetoa Yesu kristo kupitia shetani ila kuna watu bado watakuja kuumia kwa utapeli wake.
 
Back
Top Bottom