Kwa Ulinzi wa Dotto Biteko, Serikali itunge sheria kudhibiti matumizi mabaya ya Ofisi

Dr Mambo.

Kuna kitu labda wengi au wachace hatuifahamu. Ukishakuwa kiongozi siyo ila kitu utakuwa nacho huru.

Hakuna sehemu yoyote duniani ambayo viongozi hawana ulinzi ,Sweeden waziri mkuu Palme kama sitokuwa nimekosea jina hakuwa na alinzi na kilimkuta RIP. Hawa huwa wanatoa maamuzi mengi ambayo kuna mengine huwachukiza watu na mengine huwafurahisha watu hivo ulinzi kwo ni muhimu sana. Pili siyo wao wanaotaka ulizni wa watu wangapi au kukubali au kuukataa ni kuna kikosi maalum cha ulizni wa viongozi ndicho chenye jukumu la kuwalinda kulingana na wanavyoona inafaa.

Unaweza kuiona wakati mwingine kama walinzi hawapo ila siyo mara zote mpaka uone wamevaa suti au kaunda suti na ear phone sikioni. Wapo unaoweza wagundua kwa mavazi ila wapo wengine ambao huwezi watambua . Kuna advance team na ile ambayo anakuja nayo kiongozi.

Hivo Naibu Waziri Mkuu siyo takwa lake bali ni kutokana na Cheo chake hicho ndicho kilichofanya apewe ulinzi.

Wenye kufahamu haya mambo watakuja nisaidia zaidi ila huu ndiyo ukweli tutake tusitake Kiongozi ni kiongozi tu hawezi kuwa sawa na mimi au wewe zaidi kwa Mungu pekee sote ni sawa.
 
Ulinzi unatokana na nafasi yake, gharama kiasi gani kwenye ulinzi wa mtu! Kwa majukumu aliyokabidhiwa leo hii Mhe. Biteko kwa njia moja ama nyingine anasimamia mawaziri wenzake, binadamu wameumbwa na hulka na mioyo tofauti, rejea malalamiko ya JPM kutaka kuondolewa na wenzake. Biteko ataleta impact kubwa sana kwenye maendeleo ya nchi hii, mark my words.
 
Hao walinzi sio wanapangiwa na kitengo Cha ulinzi wa viongozi?
Mleta mada ni moja ya wale Biteko(Mbunge) alisema kuwa Kuna watu hawawapendi watu weusi tu Hata ufanyeje watakuchukia tu, Sasa dawa Yao anasema ni kuwapenda, hakuna haja ya "kuwasagasaga na kuwafanya juice".
 
Mkuu nashukur Sana kuelezea kwa hoja kamilifu lakini kulikuwa na haja gani ya walinzi kuwa wengi waliovaa uniform najua protocol za ulinzi zilivyo ila....

Kulikuwa na haja gani ya kuweka ulinzi wa Watu zaidi ya 10 kwenye eneo kma hilo kwanini asitumie Hiyo ulossma wewe advance team ambazo hawaonekani na wala huwez kujua kama wapo..?

Walishindwa nini kuficha au lengo kutengeneza attention kwa wananchi??
 
Huyu Mheshimiwa huwa hana makuu kabisaaa. Hapo ni amelazimika. Nahisi ni mipango ya wanausalama wa viongozi, ila si matakwa yake. Mchapakazi wetu Mungu azidi kumtangulia, aje aongoze nchi kabisa.
Kwani hawezi kukataa hilo rundo la walinzi? Kama kweli si mpenda makuu?
 
Acha wivu, NPM kujiamulia watu wa kumlinda au idara yenyewe ya usalama ndio imetoa hao walinda usalama wa viongozi! Nchi hii inamambo mengi ya kushauri na rais kasema anaona ushauri unaotolewa kupitia kikosi chake kwa jumbe za kushauri serikali kupitia mitandao ya kijamii. Hadi kulindwa kiongozi tunahoji unajua anachowaza aliyenyuma au mbele yako kuhusu wewe? Vijana ndio maana tutaitwa taifa la kesho mpaka milele
 
Sijahoji kuhusu kiongozi kulindwa nachowaza ni kuhusu Aina ya ulinzi na hasa wingi wa rasilimali watu katika ulinzi maana haiwezekani DPM kulindwa na watu 20....

Na swala la kwamba idadi ya walinzi ikumbukwe kuwa PM ndo Msimamizi wa shughuli za serkali zote na ndo amaweza kuandika proposal ya aina na kias cha ulinzi anaoutaka baada ya rais kuridhia ombi lake atakabidhiwa ulinzi huo ni simple ty
 
Ok hapo nimekuelewa Kiongozi swali zuri labda wataalam watakuja kutusaidia
 
Hio nchi bana daaa, sasa gafla hao jamaa wa protocol wameona huyo naibu ndiyo wamjazie ulinzi hivyo, kisa ni nini hapo ambacho anaonekana atakuwa hatari all over the place?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…