Kwa Ulinzi wa Dotto Biteko, Serikali itunge sheria kudhibiti matumizi mabaya ya Ofisi

Kwa Ulinzi wa Dotto Biteko, Serikali itunge sheria kudhibiti matumizi mabaya ya Ofisi

🤣 Kwahiyo unataka kumixi na Rubisi?
picha: BBC
 
Naona sasa ni muda muafaka Serkali itunge sheria kudhibiti Haya matumizi mabaya ya Ofisi maana...

Leo hii nimeona video moja ikimuonyesha Naibu waziri Mkuu Mh Dotto Bitteko akiwa kajimilikisha Majeshi yetu na hasa Usalama wa Taifa na Kulindwa na jeshi kubwa Huku akiona sifa kama Anaigiza Muvi ya Kivita hivi..

Jambo kama hili aliwahi kulifanya aliyekuwa mkuu wa mkoa Wa Dar es salaam..
naona sasa imekuwa kama maigizo hivi... Hebu muone hapa chini...
View attachment 2748142


Picha Ya mkuu wa Mkoa enzi hizo

View attachment 2748144

Na hii nyingine..
View attachment 2748150
Eti kajimilikisha, tatizo ni lugha au umeamua kupotosha tu

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Nchi yetu imejaa wanafiki na machawa. Ukiwa kiongozi, usipokuwa na hekima, machawa yanaweza kukufanyia vituko vya kila aina ya kukupamba, na ukiwa mjinga utafurahia na kukenua meno.

Kwa hiyo watu wanaokuzunguka wanafanya kwa kuona wewe unapenda nini. Kama wakigundua unapenda sifa, watakupamba kwa sifa, nawe kwa ujinga utaona kama vile tangu Ulimwengu uumbwe, hakukuwahi kuwa na mtu mwema na anayefaa kwa uongozi kama wewe.

Wanayoyatenda wasaidizi wa Biteko au hata walinzi wake yatakuwa yanaashiria hulka yake, ndiyo maana Dr Mpango alipoona ujinga wa askari wa kusimamisha magari zaidi ya masaa mawili ili yeye apite, alikemea kwa nguvu, na ikaisha. Ila kwa huyu nadhani watu wanaweza kusimamishwa hata masaa matano, atabakia anafurahia. Unaibu Waziri Mkuu, ambao haumo hata kwenye katiba ya nchi, na wala hauna mamlaka yoyote ya dola, wala hachaguliwi na wananchi, mtu akamwue kwa nia ya kupata nini?
Well...

Mkuu si mh.Biteko anayepanga ulinzi /idadi ya walinzi..

Kitisho kipo mkuu.....

"Preventive measures" ni bora na ngumu zaidi ya "counter reactions"....

Kitisho kipo mkuu....

Hasa kutoka nje...majirani zetu na wengine....huweza kutaka "kupima maji" ya nguvu za DOLA....

Likitokea hilo....ni aibu kwetu sote....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Idadi hubadilika kulingana na mahali na tukio. Lakini kama lilikuwa swalanla kawaida, aisee hao ni wengi sana..

Nimeshakutana na VP mara kadhaa, hana walinzi wengi namna hiyo. PM pia hana cycle kubwa ya walinzi kama huyo VPM.

Ni wengi sana aisee!.
Sasa kama hapo kulikuwa na ulazima gani
 
Back
Top Bottom