Heart Wood.
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 982
- 1,179
Kama ni kweli ulifanyiwa figisu kwenye uchaguzi wa Kanda ya Nyasa nikupe pole sana ndugu Msigwa. Yote kwa yote, wazo la kuhama kwako CHADEMA kwa maoni yangu ni kuwa ulifanya maamuzi ya haraka kutokana na Jazba ulizokuwa nazo. Ulistahili kuwa mvumilivu ili kulinda status yako kisiasa uliyoijenga kwa muda mrefu.
Sasa ndugu Msigwa, Kwa mujibu wa wanaCCM, ulionekana ni kete nzuri kutokana na kumsakama sana Mbowe kwa kumuita kila aina ya majina.
Na siasa zako za kumsakama Mbowe ndio zilifanya CCM uonekane kete muhimu kwao.
Soma Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%
Sasa hatamu imechukuliwa na Lissu rafikiyo, itakuwaje huko kwenye majukwaa yako ya CCM maana kumsakama Mbowe ndio ilikuwa agenga yako muhimu na sasa Mbowe uliyemsakama yupo pembeni? Kwa maoni yangu inakubidi utafute mwelekeo mpya ili kuendelea kuwashawishi CCM waendelee kukupa safari za kuzunguka huku na kule. Au la, inabidi CCM wakusitiri kwa kukugawia angalau uDC.
Alamsiki!