Lile jamaa halipati msahaha wangu.Kama ulikuwa haujamsamehe ni shida yako tuu. Tangu day one mpaka 21, watanzania tulimlilia kwa kujipiga vifuani kwa kumuomba mwenyezi mungu amasamehe yale yote ambayo alitenda kwa bahati mbaya au makusudi ila kwa lengo la kuinyosha nchi. Kati ya watanzania mil60 na hao wa vijiweni kwako wasiozidi watu50 haina athari hata kwa mwenyezi mungu. Mwenyezi mungu mwenyewe ni Baba wa Vita ana wapigania watu wake, na hata aliruhusu watu wauwawe kwa sababu ya kukiuka matakwa yeke. So, HAYATI JEMEDARI JPM pumzika kwa amani, watz tutazidi kukuombea hadi mwisho wa dahali.
Mleta mada huyohuyo kachangia thread nyingine anamsifu dikteta eti "aliwaheshimisha masikini", unafiki mtupu! Hawajui hawa hata kumtaja tuu kama hivi wanawatia hasira wananchi wengi?Namna pekee ya kutufanya tumsamehe ni kuacha kumsifia kinafiki. Kwa vyovyote vile mtu akileta uzi wa kumpaka mafuta lazima tutamwagika kuzuia upotoshaji wowote.
Yule mtu alivuruga maisha ya watu kupita kiasi.
Alichokifanya kwenye kuvunja nyumba za wananchi Kimara-Mbezi bila mshipa wa huruma, kuvuruga chaguzi za marudio, uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, kutoheshimu katiba ya nchi, kunyima stahiki za watu hasa za wafanyakazi, kutuwekea makato bodi ya mikopo 15%, Propaganda za kutukana watu kupitia Musiba, Extortion ya Pesa kwa wafanyabiashara, Kuchomoa watu mshiko kupitia Plea Bargain ya DPP, Kuminya uhuru wa habari na kuvuruga bunge na siasa za manunuzi ya watu. Inahitaji moyo mkubwa sana kumsamehe mapema namna hii!
Unapomuombea msamaha mimi natafuta namna ya kufika juu ya kaburi lake na kuitandika bakora.
😆 ila bavicha nikama mnafikiria kwakutumia matarcall.Hawezi kusamehewa kirahisi namna hiyo, tunahitaji mjadala wa kitaifa na utashi wa serikali kuwaomba watu radhi kwa maovu mengi yaliyofanywa na huyu mtu.
Kweli ameumiza wengi mno na kuna laana kubwa kwa nchi inatakiwa kufutwa kwa ridhaa ya wote walioumizwa na pia kwa ridhaa ya watanzania wote! Tuliumizwa!
Mkuu,Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.
Tokea Kifo chake GENTAMYCINE nimekuwa nikiona Lawama nyingi Kwake (Hayati Rais Dkt. Magufuli) kutokea humu Mitandaoni na hata katika Vichochoro (Vijiwe) ambavyo huwa najivinjari navyo 24/7.
Baada ya kuona Lawama, Chuki dhidi yake huku hata Wengine wakionyesha Furaha zao kwa Kifo chake nilidhani Kibusara tu basi Rais wa sasa Mama Samia au Chama Tawala chake (CCM) kingejitokeza Kwanza Kukiri Mapungufu yake au Matatizo aliyatengeneza ndani ya Tanzania yetu hii na Kiungwana kabisa Kuwaomba Radhi (Msamaha) wale Watanzania wote waliojeruhiwa au kuwa Wahanga wa Utawala wake.
Hivyo basi leo GENTAMYCINE kwa Utashi wangu binafsi (na hapa simlazimishi Mtu yoyote yule) nipo chini ya Miguu yenu nawaombeni TUMSAMEHE Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa yale Mapungufu yake yote au kama aliwakwaza na kuwaumiza Watu kwa namna yoyote ile.
Kikubwa nawaombeni tu tumuombee Malazi mema ya Milele aliyonayo na Mwenyezi Mungu pia amsamehe Makosa yake ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu katika Uso wake na hata Moyoni mwake ( japo sina Darubini ) ya Kuuona upoje au unasemaje.
Naamini kabisa kuwa Marafiki wangu (JamiiForums Members) wote mtanielewa GENTAMYCINE na sasa mtashusha Jazba zenu Kwake na Kumsamehe kidhati kabisa Baba (Mzee) wa Watu kama hata Mimi pia nimemsamehe kwani kuna mahala alinivuruga (alinikera) kwa Utawala wake kwa mambo kadha wa kadha (hasa ya Kiutendaji) japo huko nyuma nilimpigania, nilimkubali na hata Kumtetea kwa kila aina hasa alopokuwa akipopolewa (akikosolewa) kila Kona nchini.
Tumsamehe, Tumsamehe na yaishe pia!
MOJA KUBAMBIKIA WATU KESI ZIKIWEMO ZA UHUJUMU UCHUMI...UTAKATISHAJI FEDHA....KUPOTEZA WATU REFER BEN SA8 ... AZORI GWANDA SAIMON KANGUYE MAITI ZA VIROBA NKHivi unamuombea msamaha kwa mapungufu yapi kwa mfano? Ungetaja mapungufu unayoyajua angalau mawili matatu halafu uysombee msamaha. Hii itafungua mlango kwa wengine kumuombea msamaha pia kwa yale watakayoyakumbuka na kuyataja. Naomba tusiongelee msamaha wa jimla jumla wa makosa ambayo hayajaorodheshwa. Let's be more specific. Hayo ndiyo mawazo yangu
Hakuna mtu, hata awe mwovu kiasi gani aliyekosa wa kumsifia na kumkubali. Kule Ujerumani, mpaka leo, wapo wanaoamini kuwa Hitler alikuwa mtu mzuri.Kwani ametukosea nini sisi Watanzania? Kwa level ya Taifa sioni kosa lake labda kwa level ya mtu binafsi. Kama ni hivyo, basi ni jukumu la familia yake. But sisi kama Wananchi, we are proud of him and we would had wished him to live longer.
R.I.P JPM
Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Omba msamaha wa kwako mwenyewe kwanza. Magufuli hasameheki Mungu kesha fanya yake.Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.