Binafsi sikuona shida kumsamehe marehemu kwa uovu wake wote tangu alipokuwa hai, isipokuwa ugumu wa pekee niliouona, ni pale nilipomfikiria Ben Saanane, Azory Gwanda, Tundu Lisu, Mdude, Yule diwani wa Dar na wa Kilombero waliouawa kwa mikono ya greenguards na wasiojulikana; nilipowafikiria wale ambao mpaka leo wapo kule Segerea kwa makosa ya kubambikiwa kuwa ni wahujumu uchumi, watakatishaji fedha haramu, wauzaji madawa ya kukevya; na wengine kuporwa pesa zao halali kupitia mikono ya TRA kwa maagizo yake marehemu.
Hivi kweli naweza kwenda kwa Baba yake, mama yake, mke wake,mdogo wake, watoto wake au dada yake Azory, Ben, Lisu na hawa wengine wote waliouawa na kufilisiwa, na ndugu wa hawa ambao bado wapo Segerea kwa uonevu - nikawaambie tumsamehe marehemu, watanielewa? Au naweza kurushiwa mawe kwa kudhaniwa nami nilikuwa sehemu ya watesi wao?
Maandiko yanatufundisha kusamehe bila kuhesabu, lakini kwa baadhi ya watu na baadhi ya familia, kuweza kumsamehe Marehemu Magufuli, ni mpaka washukiwe na neema ya Muumba wetu. Kwa ubinadamu tu, ni jambo gumu sana.
Miaka mingi itapita, ukitaja jina hilo la Magufuli, itakuwa ni kama umetaja laana. Waliokuwa wanalitumia hilo jina ni vema wakafanya process ya kuliondoa katika orodha ya majina yao, maana wanasema majina huumba. Katika Ulimwengu wa imani, hili jina la Magufuli kamwe halitaandamana na baraka, limejaa laana. Wengi wanalia wakilitaja hilo jina, na ifahamike kauli ya wengi ni kauli ya Mungu. Kama wengi wamelilaani hilo jina, mfahamu kuwa hilo jina litakuwa limelaaniwa na Mungu pia.