Kwa Utashi wangu binafsi, baada ya kuona Chuki zinazidi Kwake na Wahusika wamenyamaza namuombea Msamaha Hayati Rais Magufuli kwa Mapungufu yake

Kwa Utashi wangu binafsi, baada ya kuona Chuki zinazidi Kwake na Wahusika wamenyamaza namuombea Msamaha Hayati Rais Magufuli kwa Mapungufu yake

Kama ulikuwa haujamsamehe ni shida yako tuu. Tangu day one mpaka 21, watanzania tulimlilia kwa kujipiga vifuani kwa kumuomba mwenyezi mungu amasamehe yale yote ambayo alitenda kwa bahati mbaya au makusudi ila kwa lengo la kuinyosha nchi. Kati ya watanzania mil60 na hao wa vijiweni kwako wasiozidi watu50 haina athari hata kwa mwenyezi mungu. Mwenyezi mungu mwenyewe ni Baba wa Vita ana wapigania watu wake, na hata aliruhusu watu wauwawe kwa sababu ya kukiuka matakwa yeke. So, HAYATI JEMEDARI JPM pumzika kwa amani, watz tutazidi kukuombea hadi mwisho wa dahali.
Lile jamaa halipati msahaha wangu.
 
Namna pekee ya kutufanya tumsamehe ni kuacha kumsifia kinafiki. Kwa vyovyote vile mtu akileta uzi wa kumpaka mafuta lazima tutamwagika kuzuia upotoshaji wowote.
Mleta mada huyohuyo kachangia thread nyingine anamsifu dikteta eti "aliwaheshimisha masikini", unafiki mtupu! Hawajui hawa hata kumtaja tuu kama hivi wanawatia hasira wananchi wengi?

Yule dikteta alikuwa muongo, katili, hana heshima, amejaa kiburi, mnafiki na mwizi.

Aliowaumiza ili wamsahau basi wafidiwe au ajitokeze #1 na mke wa marehemu hadharani na kuomba toba wakikiri kuwa huyo mtu aliumiza watu.

Nashauri hata vitu vyetu vyote Watanzania vilivyo pewa heshima ya jina lake virudishwe na majina yatolewe kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.
 
Yule mtu alivuruga maisha ya watu kupita kiasi.

Alichokifanya kwenye kuvunja nyumba za wananchi Kimara-Mbezi bila mshipa wa huruma, kuvuruga chaguzi za marudio, uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, Watu wasiojulikana, unyang'anyi wa korosho, kutoheshimu katiba ya nchi, kunyima stahiki za watu hasa za wafanyakazi, kutuwekea makato bodi ya mikopo 15%, Propaganda za kutukana watu kupitia Musiba, Kubambikizia watu kesi, Extortion ya Pesa kwa wafanyabiashara, Kuchomoa watu mshiko kupitia Plea Bargain ya DPP, Kuminya uhuru wa habari na kuvuruga bunge na siasa za manunuzi ya watu. Inahitaji moyo mkubwa sana kumsamehe mapema namna hii!
 
Sasa nenda hatua Moja Mbele.

Nenda kamueleze haya Babaake na Ben Saanane, Physically, yule Mzee hayupo humu.

Usisahau pia kwenda kwa Wazazi wa Binti Akwilina, kawaeleze haya.
Ukimaliza Nenda Kigoma kwa Wazazi wa Azory Gwanda, ukirudi pitia Geita kwa Mama Mzazi na Binti wa Alphonce Mawazo.
Ukipata chance Nenda Kwa Mke wa Azory Gwanda, Eric Kabendera yule haina haja ya kwenda Kwake, am sure huwaga anapitia JF.
 
Fikiria namna bora ya kuwaomba msamaha hawa:

1. Wale waliopotea na waliopotelewa na ndugu zao katika mazingira tata
2. Wale waliochukuliwa mali zao kidhalimu na ma-task force
3. Wale walipelekwa magerazani kwa miezi na miaka kwa kesi za kubumba
4. Walipoteza maisha katika chaguzi kama Akwilina
5. Waliopoteza biashara kama Kwanza TV na Mbowe
6. Walionyang'anywa passports Kama Eyakuze
7. Waliochafuliwa wanafanya biashara za madawa na kipendwa chake bashite
8. Waliopoteza kazi zao kwa mkono na niaovu kama Fatma Karume
9. Wakulima Ambao hawakupewa pesa zao za korosho
10. Waliobomolewa nyumba zao Kimara

Haya maneno yako machache hayatoshi kabisa.Hawa wanataka maridhiano na ukweli na kuhakishiwa hayatajirudia tena.
 
Inahitajika zaidi ya maneno matupu. Inahatijika ukweli, maridhiano na uhakika kwamba hayatajirudia.
Yule mtu alivuruga maisha ya watu kupita kiasi.
Alichokifanya kwenye kuvunja nyumba za wananchi Kimara-Mbezi bila mshipa wa huruma, kuvuruga chaguzi za marudio, uchaguzi serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, kutoheshimu katiba ya nchi, kunyima stahiki za watu hasa za wafanyakazi, kutuwekea makato bodi ya mikopo 15%, Propaganda za kutukana watu kupitia Musiba, Extortion ya Pesa kwa wafanyabiashara, Kuchomoa watu mshiko kupitia Plea Bargain ya DPP, Kuminya uhuru wa habari na kuvuruga bunge na siasa za manunuzi ya watu. Inahitaji moyo mkubwa sana kumsamehe mapema namna hii!
 
Hivi unamuombea msamaha kwa mapungufu yapi kwa mfano? Ungetaja mapungufu unayoyajua angalau mawili matatu halafu uysombee msamaha. Hii itafungua mlango kwa wengine kumuombea msamaha pia kwa yale watakayoyakumbuka na kuyataja. Naomba tusiongelee msamaha wa jimla jumla wa makosa ambayo hayajaorodheshwa. Let's be more specific. Hayo ndiyo mawazo yangu
 
Hawezi kusamehewa kirahisi namna hiyo, tunahitaji mjadala wa kitaifa na utashi wa serikali kuwaomba watu radhi kwa maovu mengi yaliyofanywa na huyu mtu.

Kweli ameumiza wengi mno na kuna laana kubwa kwa nchi inatakiwa kufutwa kwa ridhaa ya wote walioumizwa na pia kwa ridhaa ya watanzania wote! Tuliumizwa!
😆 ila bavicha nikama mnafikiria kwakutumia matarcall.
 
Dah huyu mzee huyu ila mwachenzi mwendazake kaenda na mambo yake
 
Mimi Sijakamilika sina alichonikosea na nyie mnaomshambulia Mzee ombeni radhi mkiwa hai hakuna mkamilifu chini ya jua ...wengine hata wakizikwa kaburi zao hazitaota majani kinakuwa kijangwa kidogo kwa uovu waliofanya ila kwa kunyoosha vidole hamjambo...Pumzika Mzee wangu damu yako iwasamehe hawa ndio uanadamu...haishangazi..
 
Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.

Tokea Kifo chake GENTAMYCINE nimekuwa nikiona Lawama nyingi Kwake (Hayati Rais Dkt. Magufuli) kutokea humu Mitandaoni na hata katika Vichochoro (Vijiwe) ambavyo huwa najivinjari navyo 24/7.

Baada ya kuona Lawama, Chuki dhidi yake huku hata Wengine wakionyesha Furaha zao kwa Kifo chake nilidhani Kibusara tu basi Rais wa sasa Mama Samia au Chama Tawala chake (CCM) kingejitokeza Kwanza Kukiri Mapungufu yake au Matatizo aliyatengeneza ndani ya Tanzania yetu hii na Kiungwana kabisa Kuwaomba Radhi (Msamaha) wale Watanzania wote waliojeruhiwa au kuwa Wahanga wa Utawala wake.

Hivyo basi leo GENTAMYCINE kwa Utashi wangu binafsi (na hapa simlazimishi Mtu yoyote yule) nipo chini ya Miguu yenu nawaombeni TUMSAMEHE Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa yale Mapungufu yake yote au kama aliwakwaza na kuwaumiza Watu kwa namna yoyote ile.

Kikubwa nawaombeni tu tumuombee Malazi mema ya Milele aliyonayo na Mwenyezi Mungu pia amsamehe Makosa yake ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu katika Uso wake na hata Moyoni mwake ( japo sina Darubini ) ya Kuuona upoje au unasemaje.

Naamini kabisa kuwa Marafiki wangu (JamiiForums Members) wote mtanielewa GENTAMYCINE na sasa mtashusha Jazba zenu Kwake na Kumsamehe kidhati kabisa Baba (Mzee) wa Watu kama hata Mimi pia nimemsamehe kwani kuna mahala alinivuruga (alinikera) kwa Utawala wake kwa mambo kadha wa kadha (hasa ya Kiutendaji) japo huko nyuma nilimpigania, nilimkubali na hata Kumtetea kwa kila aina hasa alopokuwa akipopolewa (akikosolewa) kila Kona nchini.

Tumsamehe, Tumsamehe na yaishe pia!
Mkuu,

Ni bora wewe umejitokeza na kutambua kwamba kumbe miongoni mwa wale waliokuwa wamemzunguka hayati mpaka viongozi wandamizi walikuwa ni wanafiki na pengine walitamani angetoweka mara moja mapema iwezekanavyo.

Pamoja na kwamba ulikuwa mkosoaji mkubwa kwa baadhi ya mambo lakini kwa hili nakupongeza na jitihada zako ndizo zitabeba thawabu ya hekima na busara. Hongera na ninakuhimiza ufanye kama ulivyonuia kwa malengo mema.
 
Hivi unamuombea msamaha kwa mapungufu yapi kwa mfano? Ungetaja mapungufu unayoyajua angalau mawili matatu halafu uysombee msamaha. Hii itafungua mlango kwa wengine kumuombea msamaha pia kwa yale watakayoyakumbuka na kuyataja. Naomba tusiongelee msamaha wa jimla jumla wa makosa ambayo hayajaorodheshwa. Let's be more specific. Hayo ndiyo mawazo yangu
MOJA KUBAMBIKIA WATU KESI ZIKIWEMO ZA UHUJUMU UCHUMI...UTAKATISHAJI FEDHA....KUPOTEZA WATU REFER BEN SA8 ... AZORI GWANDA SAIMON KANGUYE MAITI ZA VIROBA NK

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna waliotumbuliwa kwa vyeti feki
Kuna madanga yamafisadi jiwe kala vichwa
Kuna mtu alikua anakula mishahara yawatumishi hewa
Kuna wale chawa wawale maofisa wa TRA na bandari
Kuna wale chawa wama pedeshee

Hao wote nafamilia zao hawawezi kumsamehe mwendazake mpka dunia inatanduka. Tuwaache wateme nyongo zao maana miaka 6 yamwenda zake kwao ilikua nizaidi yajehanamu.
 
Binafsi sikuona shida kumsamehe marehemu kwa uovu wake wote tangu alipokuwa hai, isipokuwa ugumu wa pekee niliouona, ni pale nilipomfikiria Ben Saanane, Azory Gwanda, Tundu Lisu, Mdude, Yule diwani wa Dar na wa Kilombero waliouawa kwa mikono ya greenguards na wasiojulikana; nilipowafikiria wale ambao mpaka leo wapo kule Segerea kwa makosa ya kubambikiwa kuwa ni wahujumu uchumi, watakatishaji fedha haramu, wauzaji madawa ya kukevya; na wengine kuporwa pesa zao halali kupitia mikono ya TRA kwa maagizo yake marehemu.

Hivi kweli naweza kwenda kwa Baba yake, mama yake, mke wake,mdogo wake, watoto wake au dada yake Azory, Ben, Lisu na hawa wengine wote waliouawa na kufilisiwa, na ndugu wa hawa ambao bado wapo Segerea kwa uonevu - nikawaambie tumsamehe marehemu, watanielewa? Au naweza kurushiwa mawe kwa kudhaniwa nami nilikuwa sehemu ya watesi wao?

Maandiko yanatufundisha kusamehe bila kuhesabu, lakini kwa baadhi ya watu na baadhi ya familia, kuweza kumsamehe Marehemu Magufuli, ni mpaka washukiwe na neema ya Muumba wetu. Kwa ubinadamu tu, ni jambo gumu sana.

Miaka mingi itapita, ukitaja jina hilo la Magufuli, itakuwa ni kama umetaja laana. Waliokuwa wanalitumia hilo jina ni vema wakafanya process ya kuliondoa katika orodha ya majina yao, maana wanasema majina huumba. Katika Ulimwengu wa imani, hili jina la Magufuli kamwe halitaandamana na baraka, limejaa laana. Wengi wanalia wakilitaja hilo jina, na ifahamike kauli ya wengi ni kauli ya Mungu. Kama wengi wamelilaani hilo jina, mfahamu kuwa hilo jina litakuwa limelaaniwa na Mungu pia.
 
Kwani ametukosea nini sisi Watanzania? Kwa level ya Taifa sioni kosa lake labda kwa level ya mtu binafsi. Kama ni hivyo, basi ni jukumu la familia yake. But sisi kama Wananchi, we are proud of him and we would had wished him to live longer.

R.I.P JPM

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Hakuna mtu, hata awe mwovu kiasi gani aliyekosa wa kumsifia na kumkubali. Kule Ujerumani, mpaka leo, wapo wanaoamini kuwa Hitler alikuwa mtu mzuri.

Mathalani watu wanaofurahia mauaji, unyanyasaji, dhuluma, n.k. Watu kama hao hawatakosa kumsifia marehemu maisha yao yote.
 
Kama Binadamu (Mwanadamu) tulivyo Mimi na Wewe hatujakamilika kama walivyo Watakatifu na Malaika wa Mbinguni.

Tokea Kifo chake GENTAMYCINE nimekuwa nikiona Lawama nyingi Kwake (Hayati Rais Dkt. Magufuli) kutokea humu Mitandaoni na hata katika Vichochoro (Vijiwe) ambavyo huwa najivinjari navyo 24/7.

Baada ya kuona Lawama, Chuki dhidi yake huku hata Wengine wakionyesha Furaha zao kwa Kifo chake nilidhani Kibusara tu basi Rais wa sasa Mama Samia au Chama Tawala chake (CCM) kingejitokeza Kwanza Kukiri Mapungufu yake au Matatizo aliyatengeneza ndani ya Tanzania yetu hii na Kiungwana kabisa Kuwaomba Radhi (Msamaha) wale Watanzania wote waliojeruhiwa au kuwa Wahanga wa Utawala wake.

Hivyo basi leo GENTAMYCINE kwa Utashi wangu binafsi (na hapa simlazimishi Mtu yoyote yule) nipo chini ya Miguu yenu nawaombeni TUMSAMEHE Hayati Rais Dkt. Magufuli kwa yale Mapungufu yake yote au kama aliwakwaza na kuwaumiza Watu kwa namna yoyote ile.

Kikubwa nawaombeni tu tumuombee Malazi mema ya Milele aliyonayo na Mwenyezi Mungu pia amsamehe Makosa yake ila liwe ni Fundisho kwa Viongozi (Watawala) Wengine waliobaki kuwa wasije Kuyarudia yale yale na kwa nimuonavyo Rais wa sasa Mama Samia sioni hata hiyo Chembe ya ama Kuumiza au Kuwakomoa Watu katika Uso wake na hata Moyoni mwake ( japo sina Darubini ) ya Kuuona upoje au unasemaje.

Naamini kabisa kuwa Marafiki wangu (JamiiForums Members) wote mtanielewa GENTAMYCINE na sasa mtashusha Jazba zenu Kwake na Kumsamehe kidhati kabisa Baba (Mzee) wa Watu kama hata Mimi pia nimemsamehe kwani kuna mahala alinivuruga (alinikera) kwa Utawala wake kwa mambo kadha wa kadha (hasa ya Kiutendaji) japo huko nyuma nilimpigania, nilimkubali na hata Kumtetea kwa kila aina hasa alopokuwa akipopolewa (akikosolewa) kila Kona nchini.

Tumsamehe, Tumsamehe na yaishe pia!
Omba msamaha wa kwako mwenyewe kwanza. Magufuli hasameheki Mungu kesha fanya yake.
Siyo siri mimi nakuchukia sawa na nilivyomchukia Mwendazake.
 
Back
Top Bottom