Kwa uteuzi wa Prof. Kabudi katiba na sheria tukubaliane tu Mwambukusi atanyoosha mikono kama ilivyokuwa kwa Lissu na kudhibitiwa

Attachments

  • IMG_1534.jpeg
    27.7 KB · Views: 2
  • IMG_1535.png
    91.9 KB · Views: 3
  • IMG_1536.png
    85.5 KB · Views: 1
  • IMG_1537.png
    95.3 KB · Views: 2
Fikra duni sana. Pole sana kwa kukosa uelewa.

Yaani kwa fikra zako, sheria , katiba na kanuni huwa zinabafilika mtu akiwa mjuaji!! Kwani Kabudi au mwingine yeyote anayeweza kuwekwa kuwa waziri wa katiba na sheria, huwa anakuja na za kwake?
 
Lissu aliyasema hayo lini? Na huo ubobezi wa Kabudi ulisaidia vipi kipindi kile ndege za serikali zilizokuwa zinakamatwa kila mara na serikali kushindwa kesi?
Tuna watu wana fikra duni sana. Hawa ndio wanaamini kuwa mtu akiwa na weledi wa sheria, basi anaweza kufanya kosa lolote halafu hataonekana kuwa amefanya kosa kwa sababu anajua sheria.

Ujuaji na weledi wa sheria upo kwenye umakini wa kujizuia kufanya makosa, siyo ufanye makosa, halafu makosa yafutike kwa sababu unajua sheria.
 
Una fikra TUNDUIZI kabisa ,bravoo[emoji2956]
 
[emoji2956][emoji2956]
 
Wee chawa labda nikukumbushe tu kuwa hakuna mashindano hapo kila mtu ana kazi yake. Kabudi kazi yake ni kutunga sera na kulinda taasisi ya sheria na Mwabukusi kazi yake ni kulinda mawakili na kutetea wananchi na rasilimali zake dhidi ya ubabe wa serikali kwa mujibu wa Katiba na sheria.

Sasa tatizo liko wapi? Kabudi hataenda mahakamani kutetea serikali lakini Mwabukusi ataenda mahakamani kutetea wananchi na rasilimali za nchi.

Litakapokuja suala la kutetea serikali na nchi kimataifa Kabudi hataenda mahakama za kimataifa bali Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiona uzito wa kesi anaweza kuomba msaada wa Mwabukusi na timu yake ya TLS kusaidia.

Kwa hiyo kuwa muelewa hakuna mashindano baina ya Kabudi na Mwabukusi bali kuna win win situation kwa manufaa ya Taifa.
 
Kwa hiyo una maana Rais Samia anamuogopa saasna Mwabukuzi kiasi ameamua kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ili kupata mtu nje ya Cabinet yake wa kuweza ku match na Mwabukusi? Hivi unatumia kiungo gani cha mwili wako kufikiri? Maana wakati mwingine huu uchawa ukizidi inakuwa ujinga unafikiri unasifia kumbe unamponda Samia kuwa ni dhaifu hadi ahitaji msaada wa mtu ambaye alishampiga kibuti, ndiyo yale yale ya Awadh kufanya ujinga akifikri anamfagilia njia Samia kwa kuihujumu Chadema kumbe anaiharishia kazi ya Samia aliyoifanya kwa miaka mitatu.
 
Nyie si ndio mlisema tutashtakiwa MIGA kilikuwa wapi?? Tusisingizie sheria wakati ziko wazi na kinavhopaswa ni utekelezaji, mtu akikutafuta hakosi Sababu
Kwa akili yako kisoda hatujashitakiwa na kulipa mabilioni na kesi nyingine bado zinaunguruma huko ughaibuni?
 
Huyo Profesa wa "Jalalani" ana jipya kweli?!🤔
 
Mzee wa kuongea huko katoa macho kodokodo ndio mnamuita mbobezi wa kitu gani??
Nikikumbuka ile safari yake ya Madagascar kwa ndege yetu watanzania na kwenda kuleta dumu na chupa za juisi nimemtoa maana kabisa hana usomi wowote zaidi ya UCHAWA.
 
Hakuna jipya! Pale mihimili inapokiuka katiba na Sheria za nchi lazima TLS wasimame kueleza ukiukwaji huo. Maana tumeshuhudia pia vyombo vya kusimama na kutoa haki( mahakama) vikishindwa kufanya hivyo kwa shinikizo kutoka kwa watawala.
 
Kwa akili yako kisoda hatujashitakiwa na kulipa mabilioni na kesi nyingine bado zinaunguruma huko ughaibuni?
Tatizo lako ni kiherehere na sio kingine, sasa sheria ina tatizo gani??? Kuhakikisha kuwa Tanzania inafaidika na maliasili ndio ubaya wa sheria??


Sasa kama watendaji wameamua kwa makusudi kutotimiza wajibu wao na kupelekea nchi kuingia kwenye migogoro unailaumu vipi sheria??

Je kabla ya hiyo sheria hatujawahi kushtakiwa??? Jibu ni ndio ni kwanini

Ndio ujue kuwa Sheria ni nzuri ila watekelezaji ndio wanaliponza Taifa, either kwa kusudi au kutokukusudia lakini twende mbele ama turudi nyuma

Hakuna kushtakiwa pasipo na kosa, ujiulize kosa letu liko wapi

Maana kila mkataba unaendana na sheria
 
Kosa ni kuvunja mikataba kihuni
 
Mwabukusi, si Mwambukusi.

Una ugonjwa wa kukutatiza kusoma?
 
Kabudi huyu huyu aliyeleta dawa ya Covid toka Madagascar?
 
Kwani Mwambukusi majukumu yake ndo majukumu ya Waziri wa Sheria?? Mbona naona hoja yako ipo Kichawa zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…