MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Kitendo cha Klabu ya Yanga kuja na Taarifa ya Pole kwenda kwa Simba SC, Wapenzi wa Simba SC na Familia yake Marehemu kama Mdau mkubwa wa Simba SC nimekipokea kwa Picha iliyo Chanya kabisa.
Yanga SC na Simba SC tunataniana mno na Kufanyiana Fitna za kila aina ila kwa huu Uungwana, Ustaarabu, Utu na Uamamichezo uliotukuka nitakuwa Mnafiki nisiposhukuru na Kuwapongeza wana Yanga SC wote.
Najua kuwa hata Sisi Simba SC kukitokea Msiba huko Kwao Yanga SC pia huwa tunatoa Pole hivi ila kwa jinsi tulivyokuwa na Uhasama kutokana na Usimba na Uyanga wetu kwa Siku za karibuni hili lillofanywa na Watani zetu Yanga SC sikulitegemea.
Kwa Uungwana na Utu huu wa Yanga SC Kwetu Simba SC nami Mightier naahidi kuanzia Leo Jumamosi mpaka Siku atakayozikwa Hanspoppe sitowatania au kuwachokoza au kuwakasirisha Yanga SC hapa JamiiForums kwa Threads zangu ila Zoezi hili litaendelea baada ya Maziko ( Mazishi )
Hata hivyo kwakuwa Sisi Simba SC na Yanga SC ni Watani nami Mightier nichukue fursa hii ( Kiutani Jamani ) ya Kuwaambia Yanga SC kuwa ina maana Mganga wao kule Avic Town Kigamboni waliko aliwaomba Roho ya Zackaria Hanspoppe ili wawafunge Rivers United FC Kesho kwa Mkapa badala ya Roho ya Injinia Hersi Said?
Akhsanteni mno wana Yanga SC wote na nichukue nafasi hii kuwatakieni Kila Ia kheri Kesho mshinde katika Mechi yenu ya Kwanza ya CAF CL dhidi ya Wanaijeria ( Wapopo ) akina Rivers United FC ila mkifungwa hiyo Kesho kama kawaida yangu mtanikoma Mightier hapa Jamvini.