mshumbusi
JF-Expert Member
- Oct 24, 2011
- 457
- 232
- Thread starter
- #21
ongera sana kwakupenda hii biasharaMimi ninataka kuifanya hii kazi unanishauri nianzie atua gani kabla sijaanza na pakununulia na kujua haya ni madini gani na bei ya kuuza na changamoto zake japo madini yapo mengi sana unisaidie zinazopatikana kwa wingi zsidi hapa kwetu?
kifupi mm nilianza biashara hii kwa kupata hasara sana na nilikua sijui bali nilifata hobi yangu ya kupenda hii biashara.nilianza biashara waka2009 na nilikua na jamaa yangu ambae niliamini anajua kumbe na yeye alikua hajui .hivyo nilinunu mawe kwa bei juu na kupata hasara
mara nyingine nilipewa fake na kupeleka sokoni na kupata hasara ., lakini mara zote nilikua sikati tamaa niliamini ipo siku nitaijui hii biashara ... nakumbuka niliwai kununu madini ambayo ni ya kiwango cha chini na nikapeleka dar es salaam ila sikuweza kuuza na nilirudi nayo home kipindi hicho nilikua naishi songea .... ila sikukata tamaa nikatoka nikaend amsumbiji nikaanza kuchimba na ila tulipata madini na tulivamiwa na askli wakatupiga na kutunyanganya madni ....mm niliwaacha wenzangu na kurudi home
nilipo rudi nilianza upya kutafuta mtaji nikata pesa kidogo nikaenda sumbwawanga nilipofika nilitafuta watu nikawambia natafuta madini wakanipa jamaa ambaye alijifanya anayajua mawe na atanileteeea baade alitoroka na pesa yangu ikabidi nirudi home nilipofika nikapiga kazi tena lakin nikapata kama mil2 then nikaenda kongo kufata madini yanayo itwa tomalin nilifanikiwa kumuona jamaa ila sikufanikiwa kupata ya quality nzur mudahuu nilikua tayari naya jua mawe then nikarudi home
baada ya hapo
nikaanza kufahamu kuwa biashra ya mawe sio rahisi inaitaji kujitoa nakujua kuwa biashara hii inaitaji kuwa serious sana kuliko biashra nyingine maana unadeal na vitu usivyo vijua kama vipo ala ndio nikaanza kuchimba kwa kuwapa watu pesa na kuchimbisha nakuona faida
nimekueleza haya yote ujue
(1) ina matapeli
(2) sio rahisi kama wengi wanavyo zania
(3)hutakiwi kuta tamaa
(4)nikazi kama kazi zingine yaani inaitaji kujua unachokifanya
jinsi ya kufanya kama unataka kufanya biashara hii
kunanjia mbili
1. uwe broker
2.mchimbaji
3.super deals
broker
huyu niyule anae nunua madini kutoka kwa wachimbaji wadhabu wanaitwa digaras.hapa unaitaji sana kuwa na pesa na pili unaitaji kuwa vifaa vya kuangalia mawe unayo nunu maana unaweza kupewa chupa au fake mawe . unatakiwa kuyafahamu mawe in details na jiwe linakuwa lina thamni gani mfn jiwe zuri linakua halina babo,cloud ,shape nzuri,no crack , pili inatakiwa ulipie leseni nadhani kwa sasa ni 250,000/=
na maweyenye than i ni yale yenye hardness kubwa kama ruby ,diamond ,sapphaya ,ya nayo bakia hayana thamani mani ya kawaida .... hubroker pia unauzuri wake maana wachimbaji wengi hawajui dhamn halisi ya bei
hii kwa kuanzia sikushaulio ufanye hii kuwa broker
uchimbaji
uchimbajio unaugumu wake ila au hitaji pesa zaidi ya pesa kidogo ya kuwapa wanao chimba na chakula .uchimbaj nimgumu kwakua unakaa polini kwa muda mrefu hadi unapo kuta njia au vein ya madini .... Kwa watu mlio zoea town hapa inakua ngumu sana wengi wanashindwa kukaa polini wanashindwa kuishi bina net work wanashindwa kuishi kwenye ugumu wa kula ugali na maharage .... hapa kwenye uchimbaji lazima ufate caption ndizo zinakupeleka kwenye gem mawe mazuri so inawenza kuchukua hata miezi 3 au zaidi na pia unaweza kukosa..kwa sasa kuna geologist wa kukodi unaweza kumkodi na akakuelekeza jinsi ya kuchimba na kupata kwa haraka
super deals
hawa niwele wanao nunu kutoka kwa blokers ..hawa kwa ruby wapo sana waphilipino . na wananunu kulingana na ubora nilio kueleza hapo mwanzo .pia wapo wanao kujaribu kujua kama unachokiuuza unakijua hii inaitaji mtaji mkubwa maana hawa ndio wanao uza nje ya nchi .unaweza umkauza hadio kwanza upate mteja kutoka nje na mara nyingi wanakuwa wannunua kwa kontena
mwisho
hakuna pesa rahis wangu inaitaji kujituma na kukubali kitu kilichpopo moyoni kwako
jaribu kama ukipata hasara usikate temaa komaaa