Kwa wale ambao hamna maelewano mazuri na wazazi wenu

Pia Da'Vinci soma LUKA 12: 51- 53 . Yesu anasema " Je, mnafikiri nilikuja kuleta amani duniani? Hapana, si amani bali mgawanyiko, watatu dhidi ya wawili na wawili dhidi ya watatu. Baba dhidi ya mwana, mwana dhidi ya baba, mama dhidi ya binti, binti dhidi ya mama.
Pia LUKA 8: 20 - 21

" Basi akaambiwa: mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kukuona. 21 akawajibu: mama yangu na ndugu zangu ni hawa wanaosikia neno la mungu na kulitenda.

Mbarikiwe sana, jenga ukuta, tena wahi mapema kabda hujapatwa na mental case. Dunia ya sasa watu wamevurugwa sana.
 
Mimi kwa upande wangu niliharibiwa kisaikolojia tu

Stori ipo iv

Sijawahi kukosa kitu kwa mzazi wangu (baba), ila shida ilikua moja tu.

Wakati nakua mm nilikua sisikilizwi hata kwa vitu vya kawaida, kila jambo ni lazma waseme wenzangu ndo litatekelezwa ila nikilianzisha mm haliwez kufanyiwa kazi, hapo ni hadi vile vitu vinavyonihusu mm binafsi ni lazma nipate back up ya walionitangulia (ambao wamekulia maisha hayo watakua wanajua).

Nakumbuka kuna safafari nilikua naenda shule so mm na rafiki zangu tukakubaliana tupande gari moja na kila mmoja amuombe mzazi wake nauli akakate tiketi mwenyewe, kwa upande wangu nilinyimwa wakati wenzangu wote walipewa hela na wazazi wao kasoro mm tu (hili jambo liliniharibu sana), ikabidi niwadanganye marafiki zangu kwamba sitosafiri hyo siku but ilivyofika asubuhi wakaniona napanda kwenye wanteni kwa bei sawa na magari mazuri waliyopanda wao, niliumia sana

Hiyo hali iliendelea mpaka nilipokua chuo.

Kisa kingine kilichonifanya niache chuo

Nakumbuka nilikua mwaka wa pili na ilitakiwa niwe na laptop kwaajili ya kufanyia mazioezi ya autocard(wale mliosoma engineering mtanielewa umuhimu wa laptop kwenye hili somo)

Nilivyoomba laptop mzee akaniambia nimwambia kwanza ndugu yangu na yeye ndo atamwambia ili amtumie hela, nilifanya kama alivyoniambia ila shida ikawa hela ilivyotumwa sikupewa hiyo laptop kwa wakati

Hapo taa nyekundu ikawaka kichwani mwangu nikajiona kama msukule ivi, kwa haraka sana nikaanza kutafuta kazi ili niachane na chuo, mungu ni mkubwa nikapata kazi na nikaachana na habar za chuo ili nianze kuishi maisha yangu mwenyewe

From there nikitaka kufanya jambo nilikua sisikilizi mtu ninafanya kile ninachojiskia mwenyewe.

Mpaka leo hii namuone huruma wife na ndugu wanaopenda kunishauri vitu coz hata wanishauri kitu cha heri huwa siwasikilizi nafanya kama nilivyokuwa nafanyiwa mimi.

Nimelaumiwa sana kwenye upande wa familia ila hawajui kwamba wao ndio wamenifanya mimi niwe hiv nilivyo sasa


Kwa sasa hela ya kubadili mboga ninayo ila ndo hivyo tena saikolojia ishajiendea kibra.
 

Stry ya maisha yako ni kama yangu tu, mpaka nahisi labda mzee alinizaa kwa bahat mbaya.?![emoji3061]
 
Hawawezi kuelewa unachopitia. Hizi story zipo nyingi. Wazazi wanahisi wakishakulipia ada, wakikupa chakula na sehemu ya kulala wameshamaliza kazi mengine hayana umuhimu.

Ni vema kufahamu kuna vitu unaweza mfanyia mtoto akajiona anaishi na watu baki matokeo yake akipata upenyo wa kuondoka nyumbani na kuanza kujitegemea anakata mawasiliano na kuwa outcast wa familia.

Jamii ijifunze. Mimi hadi muda huu nina hofu ya kuanzisha familia kwasababu sitaki mtoto wangu yoyote apitie nilichopitia mimi maana unajikuta unachuma dhambi za bure za kuchukia watu hadi kutotaka kukutana nao au kukaa nao sehemu moja.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Me Mzee wangu kavurugwa na mama wa kàmbo ili anione Mimi kinyesi, inafika muda Mzee unampigia Simu hapokei kwa kuhofia nitamlilia shida haya Mzee wangu uliikuta missed call basi nitafute uniulize kunani kijana wangu mbona ulinipigia Simu mida Fulani.

Hana kabisa time kisingizio ubuzy wa kazi kweli Mzee wangu, au akipokea hata haniulizi mwanangu unaendeleaje na majukumu. Mzee anafahamu fika kuwa maisha yangu yameharibiwa na walimwengu hivyo msaada wake nauhitaji lakini Hana time na Mimi.

Anyway namuacha apande mazao yake kikamilifu kwani atakachokuja kuvuna Mungu ndiye anajua.
 
Aisee
 
Duh
 
Pole sana ndugu... nakuelewa, wengi wanapitia kutengwa na kunyanyapaliwa na familia au wazazi wao wa kuwazaa. Hawawasaidii wala kutaka kushiriki na kujua nini kinaendelea maishani mwao.


Ungehama zako na nchi kabisa! Na watoto wako uje uwaambie "nyinyi hamna ndugu!... ndugu ni nyinyi wenyewe, mimi baba yenu na huyu Mama yenu"
 
Nimesahu Ni Nani ..lkn Kuna mdau humu aliweka Uzi..akisema hapatani na Mama yake mzazi..maana Kila Jambo ambalo alikiwa akimshirikisha Mama yake kwa Nia njema Jambo Hilo linakwama.
Ni Mimi mkuu. Siku hizi nimejitenga, Ni mwaka mmoja Sasa hawajui nilipo na Mimi sijui wapo hai au wamekufa and I don't care kwa sababu hakuna atakayeishi milele
 
ur not alone kwenye hilo wapo is wengi wana pitia hiyo hali ya kubaguliwa tangu watoto,ni ngumu kurudi nyuma
mimi wakati nakua nilikuwa namuona mama angu ananibagua lakini saivi naona alikuwa sawa tu,wakati mwingine tabia zetu watoto zinakuwa so nzuri tusiishie tu kulaumu wazazi
 
Hata wazazi hukosea. Akikosea muweke sawa - mwambie, sio kisa mzazi basi unaogopa kumchana.

Miaka kama 8 hivi iliyopita, mama angu aliwahi kunipigia simu na kuanza kunilalamikia kwanini simpigii simu, na ni kweli nilikuwa sipigi simu kwasababu nilikuwa nimevurugwa na maisha, na akili haikuwa sawa.

Sasa mimi kitu kimoja huwa sipendi ni mtu anilalamikie, huwa sipendi hilo jambo, nikamuambia mama 'we ukiona sikupigii uwe unapiga wewe'

Nikaona ameshangaa ile ya kichaga 'haya baba angu, na usipige kabisa'

Na kweli sikupiga simu tena zaidi ya mwezi, yeye ndo alinipigia siju moja ndo tukaongea kama kawaida.

Tangu wakati huo hakuwahi kunilalamikia tena kwamba sipigi simu, japo naweza pitisha mpaka wiki tatu sijaongea naye
 
Ipo siku utatamani kuongea nae ila utakua ushachelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…