Kupitia uzi huu nimejifunza mambo mengi Sana nilidhan mm pekee ndyo napitia magumu ya familia yangu kumbe tupo wengi Sana
Kikubwa tuchukulie changamoto hizo tulizopitia kurekebisha familia zetu (watotowetu) tiwatendee mema tuwasikilize na tuwashaur vyema
Binafsi mzaz wangu wa kiume alinipa kila kitu kadir ya uwezo wake lakn kitu kimoja pekee udikteta Tena kwangu tuu kutonisikiliza Wala kinishirikisha kwa Jambo lolote badala yake wanasikilizwa watoto wengne na wanakaa nakupanga mambo ya familia mm naambiwa tu
Jambo hili lilinipa msongo wa mawazo Sana ukizingatia mm nilikuwa mtoto mkubwa kat ya wote lakn n mtoto wa nje ya ndoa na nilijipeleka tu kwa baba yangu baada ya shida kuwa nyingi huko nilokokuwa nakaa (kwa Bibi) ujio wangu pale unaonekana uliharibu kanuni na taratibu zao lakn nifanye nn n mm shida zilinikimbiza wakat mzaz wangu anakila kitu alikuwa engineer wa tanroads mkoa X
Hali ya kutengwa kimaamuzi iliendelea had nilipofika chuo pesa za matumizi had nimpigie mdogo wangu ndyo itumwe ukimpigia mzee hapokei simu na akipiga atanilaumu kwanini nilimpigia mda wa kazi ukipiga jion atakuambia yupo na marafk zake nisimsumbue
Amekuja kustaafu mm nipo chuo mwaka wa 4 namalizia akawagawia wanae wote Kia's Cha pesa Kama 5M kwa kila mtu mm sikupata hata shilingi na hii nilikuja kuambiwa na mdogo wangu alikuja kufunga mzgo wa biashara akaniambia wewe pesa yako utafanyia Nini ? Ndipo nikajua kumbe wamepewa pesa
Lakn MUNGU n mwema maisha Sasa yanasonga Nina familia yangu najitahid kuilea kwa upendo ili nisije kosea Kama mm nilivyoona nakosewa
Kwa Sasa mzazi wangu anailaumu simshirikishi katika maamuz ya mambo yangu najitenga Sana na familia sipigi simu mara kwa Mara
Sent using
Jamii Forums mobile app