Nakuelewa sana mtu wangu. Hiki unachopitia ni kitu ambacho kuna watu wengi wanapitia halafu wanaamini ndio maisha so kuvumilia na kukubali upuuzi ndio namna ya kuishi. HII SI SAHIHI KABISA.
Mimi pia napitia the same story. Mimi mtoto wa pili kutoka mwisho. Tupo wa 5. Mzee wangu alikuwa mpambanaji sana kutoka mtoto wa mfugaji yaani wale watoto wa kuchunga ng'ombe na kutoroka kuja mjini kujipambania na kujiendeleza kwa elimu hadi akawa mhandisi wa mitambo na kufanya kazi wizara ya ujenzi chini ya magufuri kabla hajawa hata mbunge.
Mzee kapambana na kutafuta mali nyumba 3, biashara za maduka ya spare, trekta 2, mashamba matatu mbeya, mawilli morogoro, land Rover 110, land Rover 109, Isuzu tipper, na garage yenye vifaa vingi tu vya kisasa vya gereji. Hivi ni baadhi ya vitu vichache mzee aliacha. Na kulikuwa na salio Bank pia.
Picha linaanza mshua kafariki ghafla kwa shinikizo la damu. Tukabakia na bi mkubwa kama msimamizi na mshika mirathi. Watoto watano, wakwanza amemaliza form 6 kwa mbinde balaa mzee alikuwa kila siku anampa risala atulie asome yeye michezo, wapili nae mzee kuvuta alikuwa yupo kidato cha n'ne akasema yeye shule hataki, tusome sisi wadogo tu, watatu alikuwa form one, wanne ni mimi nikiwa darasa la 5, na wa mwisho akiwa vidudu ndio anataka kuanza la kwanza.
Sasa kutokea hapo ikawa bi mkubwa kwa kushauriana na sista wa kwanza ni kuuza kitu kimoja baada ya kingine bila consultation ya watu wenye ujuzi. Mfano waliuza gari Isuzu tipper kwa bei ya hasara ya 1 million kwa kupigwa sound na madalali. Then upotevu uliendelea kwa mali zingine ambazo ziliuzwa kwa bei za hasara. Me nikiwa mdogo na sina nguvu za kushauri au kukataa.
Haya yaliendelea kwa muda mrefu na mali nyingi zilitoweka katika mazingira ya uzembe sana. Na wahusika ni bi mkubwa, sista mtoto wa kwanza na bro mtoto wa pili, huyu watatu alikuwa mkoani alipokuwa akisoma boarding. Mimi na mdogo wangu tulikuwa nyumbani.
Mimi nilimaliza primary na kufaulu shule ya Serikali. Kipindi hicho ada kwa mwaka ni elfu 20. Lakini nilikuja kuilipa hiyo pesa mwenyewe nikiwa nakwenda chuo maana nilitakiwa kupeleka cheti na sio results slip. So nilikwenda kulipa ada ya miaka yote minne kwasababu sikuwahi kulipiwa ada na bi mkubwa. Kwakifupi pesa ambazo zilitolewa serikalini kwaajiri ya kusomesha watoto, maza alizigawanya kwa kuwapa wakubwa ambao hawakuwa shule, yule wa boarding alipewa account yake yote ambapo aliacha shule na kuanza kufanya upuuzi wa kujifanya mjasiliamali wa maswala ya miziki na kupromote wasanii akaishiwa kudhurumiwa pesa na mwenzake aliyekuwa mjanja wa mjini so akakosa shule na biashara chali.
Huku nyumbani pesa zangu mimi ambayo ilikuwa ni around 3 milion sikupata hata mia maana account ilikuwa ni ya kusimamiwa sikuwa nimetimiza miaka 18 kwa wakati huo. so bi mkubwa ndie alikuwa na access ya account yangu na ya mdogo wangu wa mwisho. Pesa zetu zilitumika bila sisi kujua na ziliisha haraka sana ndio maana nilipofaulu kwenda sekondari hakukuwa hata na 100 ya kunisapoti.
Huu uharibifu ulifanyika ndani ya muda mfupi na waliofanya ni bi mkubwa, sista mtoto wa kwanza, na bro mtoto wa pili. Bro alisema anataka kupambana akapewa tractor akaenda kulitelekeza huko hadi leo hii haijulikani kuwa aliuza au alifanyaje hiyo ni siri yake, sista kwa kushirikiana na boyfriend wake wa kipindi hicho waliuza mashamba na pesa kidogo wakamtumia maza nyingine sista akala bata na jamaa na kumhonga.
Maisha yakifika kipindi yakawa magumu maana ufujaji ulimaliza pesa zote zilizokuwapo kwenye akiba na asset ambazo zilikuwa za kuuzika kirahisi kama magari, trekta, mashamba, na mzigo kwenye maduka ya spea, waliviuza kwa bei za hasara chini ya bei ya soko so ni kama walivigawa bure na vingine kama tractor vilipotea bila taarifa.
Sasa ilifika kipindi naenda shule kwa shida napewa 200 ndio pocket money. Aisee nikikumbuka nashikwa hasira sana.
Fast forward leo, nilipita kwa shida sana ila MUNGU sio Jr makamba nikafika chuo na kumaliza salama kwa msada wa marafiki, na baadhi ya ndugu ambao walinisaidia kwa lawama sana kwa kuwa mzee alikuwa na mali walihisi mimi ni wale watoto wa kusema uongo jambo ambalo lilinifanya nikiwa na shida kufa na tai shingoni sikuwa tayari kumwambia ndugu bora nimuombe mtu baki au marafiki na familia zao wataweza nipa sapoti bila kuhoji.
Baada ya kumaliza elimu ilikuwa kama zari nilipata ajira ndani ya miezi mitatu tu. Kwa namna nilikuwa nachukia kuwa karibu na ile familia nilikopa hela kidogo nikaondoka nyumbani miezi minne tu baada ya mwezi wa kwanza kuanza kazi. Bi mkubwa alilalamika sana na kunitamkia kuwa naondoka kwasababu nimepata kazi badala ya kukaa na kuwasaidia mahitaji pale ndani.
Nilishajaribu kuweka mambo sawa kwa kulazimisha nyumba zile nyumba mbili kati ya tatu zipangishwe ili kodi isaidie maana nyumba walikuwa wakiishi ndugu so nilizungumza nao kiuungwana wakakubali kupisha. So kodi nikawa nashika mimi nampelekea bi mkubwa mahitaji yake ya ndani kama chakula na kadhalika.
Yule sista ambaye nae anaishi mkoani na jamaa mluga luga tu na bro nae asiyejisoma anaishi kwa mwanamke wake aliezaa nae, wakawa na mawasiliano maana bi mkubwa alikuwa na tabia za umbea za kuwaambia kila ninachofanya. Sasa sijui ni wivu wakaanza kusagia kunguni kuwa kwann nashika pesa za kodi nimuachie mama ashike mwenyewe, yule mtoto wa tatu alikuwa amepotelea mikoani huko maana aliacha shule asijue anafanya nini na maisha yake akarudi home kwa bi mkubwa na kuishi pale na akiwa anajifanya ni mtu wa kusali kumbe unafiki tu maana ndie alikuwa mchochezi.
Kuna siku bila taarifa bi mkubwa ananipigia simu kuwa yupo kwa wapangaji wamegoma kumpa kodi niwaambie kuwa yeye ndie mwenye nyumba na kuanzia sasa atakuwa anapokea yeye, aisee nilimind sana. Nikamuuliza kwann umeenda kwa wapangaji, akaanza kujibu kwa ukali kuwa nisimpande kichwani. Nikaona isiwe shida, ya nini kupata laana ya bure. Nikawaambia wapangaji wote kuwa huyo ni bi mkubwa watoe shaka.
Tokea siku ile nikaachana na maswala ya familia nikapiga kimya. Yule mtoto wa tatu na huyu mdogo wangu wa kike wakageuka masnitch namba moja wakiungana na wale wakubwa wawili kuwa wapinzani kwangu.
Kimsingi nikaamua kujitenga na familia kwasababu katika kitu sipendi ni kuishi na watu ambao hawaeleweki na wana mambo ya ajabu na upuuzi mwingi.
Haiwezekani watu kwa uzembe wenu mharibu na kufuja mali za familia halafu zinabakia chache anatokea moja wa wanafamilia anataka kuzisimamia vizuri mnamletea ligi kwa hoja za kipumbavu na za wivu wivu na mafigisu ya kifala. Mimi nikasema kama mtaniona. Huu ni mwaka wa tano naandika sijaenda tena na bi mkubwa ameshaniulizia sana. Naongea nae tu kwenye simu kumsalimia kawaida akianza kuniuliza nipo wapi au nafanya nini ntasitisha mazungumzo hapo hapo nikate simu na huwa siulizii chochote hapo nyumbani. Nikitaka kutoa sapoti nampigia mpwa wangu namuelekeza nilipo nampa kama vifurushi na pesa kidogo namtumia bi mkubwa napiga kimya.
Kuna familia nadhani tunakuwa tumezaliwa kimakosa. Sasa kulazimisha kublend nazo unaweza kufa kwa pressure. Mimi kama wewe nimeamua kukaa nao mbali na ninaona namna ninavyokwenda vizuri kwasasa maisha yangu yana utulivu na sina msongo wa mawazo
Huwa namuelewa sana mtu akizungumza kama wewe hivi.
Sent from my JKM-LX1 using
JamiiForums mobile app