Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa ndo kwenye tatizo mkuu, bond mbovu kati yangu na mazaa inatutesa sasa hivi.uhusiano ni kama daraja kama hukunipenda na kuweka uhusiano mzuri na mimi utotoni usidhani ukubwani nita kupa time wala nafasi Never
Dahh! Pole sana ndugu yangu... bin-Adam sisi... mhhhh! Kesho kwa mungu kutakuwa na mengi sana hadharani 😔😔😔Me Mzee wangu kavurugwa na mama wa kàmbo ili anione Mimi kinyesi,,,, inafika muda Mzee unampigia Simu hapokei kwa kuhofia nitamlilia shida haya Mzee wangu uliikuta missed call basi nitafute uniulize kunani kijana wangu mbona ulinipigia Simu mida Fulani,Hana kabisa time kisingizio ubuzy wa kazi kweli Mzee wangu,,, au akipokea hata haniulizi mwanangu unaendeleaje na majukumu,,,, Mzee anafahamu fika kuwa maisha yangu yameharibiwa na walimwengu hivyo msaada wake nauhitaji lakini Hana time na Mimi. Anyway namuacha apande mazao yake kikamilifu kwani atakachokuja kuvuna Mungu ndiye anajua.
Kumbe unakuaga na akili bwana Himars eeh?! 😀🤔Biblia hiyo hiyo imewaasa wazazi wasiwachokoze watoto wao
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Mzee hakutaka majukumu... alitaka zake kula mtungi na kugonga tu! 😅👍🏾Kwakweli nimejitahidi kurudisha mahusiano na baba yangu ila nimeshindwa..japo kosa ni lake mwenyewe. Ila mwenyewe hataki tena anapokea simu tu kwakua namba yangu hajaisevu.
Najitahidi kumsamehe nashindwa kabisa. Maana anayofanya sio kwangu tu hadi kwa ndugu wengine...kiufupi hataki uzao wake wote.
Daaa!Hahaha mkuu! Kama kuna kitu ni kigumu kukucontrol duniani basi ni ngono na aina zake zote.
Ata kushindwa kuchukia unapochukizwa au kuendelea kujikomba kwa watu wasio kuthamin ni tatizo la akili piaWatz wengi wanamatatizo ya Afya ya Akili
Yaani Mimi Akili yangu bado hipo vizuri siwezi kumchukia Mtu awe au ndugu maana njaa na umasikini na Matatizo ya Afya Akili vikiungana lazima muwachukie watu. Eti Mtu anamchukia Mzazi au Mzazi anamchukia mtoto what a kid?
Aiseee, pole sana inaumiza mno.!Ukiacha yote aliyowahi kunifanyia ikiwa ni pamoja na haki ya kumjua baba lkn hii kauli ( NATAKA KUAGIZA GARI LINGINE KWA SASA HVYO SIWEZI KUKUTUMIA MATUMIZI HUKO CHUONI )ndio ilinfanya nione ilikua bahati mbaya sana yeye kunizaa ingawaje hata upendo wa kinafki nimeushindwa. Yan una mzazi si fukara lkn unaishi maisha ya kuomba omba yeye yupo busy kuhangaika kulinda ndoa yake and worse yeye ni mama, boalra angekua baba huenda ningempa excuse kalishwa limbwa na mke wake sasa mama nae kapewa limbwata na mume wake aisee wazazi ni mtihan mkubwa
ITS SEVEN YEARS NOW NAONA VEMA KUKAA MBALI NAYE
YANI MZAZI ANAKUCHUKIA MPAKA HUELEWI ULIKOSEA NINi
NAKAZIA.Ata kushindwa kuchukia unapochukizwa au kuendelea kujikomba kwa watu wasio kuthamin ni tatizo la akili pia
Hahahaha,,,,, kwani ni lazimaIpo siku utatamani kuongea nae ila utakua ushachelewa.
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]Pole sana man,i can feel your pain bro
Mkuu wakati mwingine siyo akili zao,,,tusiwalaumu sana,,,aliyelishwa Limbwata hajijui kama karogwaKupitia uzi huu nimejifunza mambo mengi Sana nilidhan mm pekee ndyo napitia magumu ya familia yangu kumbe tupo wengi Sana
Kikubwa tuchukulie changamoto hizo tulizopitia kurekebisha familia zetu (watotowetu) tiwatendee mema tuwasikilize na tuwashaur vyema
Binafsi mzaz wangu wa kiume alinipa kila kitu kadir ya uwezo wake lakn kitu kimoja pekee udikteta Tena kwangu tuu kutonisikiliza Wala kinishirikisha kwa Jambo lolote badala yake wanasikilizwa watoto wengne na wanakaa nakupanga mambo ya familia mm naambiwa tu
Jambo hili lilinipa msongo wa mawazo Sana ukizingatia mm nilikuwa mtoto mkubwa kat ya wote lakn n mtoto wa nje ya ndoa na nilijipeleka tu kwa baba yangu baada ya shida kuwa nyingi huko nilokokuwa nakaa (kwa Bibi) ujio wangu pale unaonekana uliharibu kanuni na taratibu zao lakn nifanye nn n mm shida zilinikimbiza wakat mzaz wangu anakila kitu alikuwa engineer wa tanroads mkoa X
Hali ya kutengwa kimaamuzi iliendelea had nilipofika chuo pesa za matumizi had nimpigie mdogo wangu ndyo itumwe ukimpigia mzee hapokei simu na akipiga atanilaumu kwanini nilimpigia mda wa kazi ukipiga jion atakuambia yupo na marafk zake nisimsumbue
Amekuja kustaafu mm nipo chuo mwaka wa 4 namalizia akawagawia wanae wote Kia's Cha pesa Kama 5M kwa kila mtu mm sikupata hata shilingi na hii nilikuja kuambiwa na mdogo wangu alikuja kufunga mzgo wa biashara akaniambia wewe pesa yako utafanyia Nini ? Ndipo nikajua kumbe wamepewa pesa
Lakn MUNGU n mwema maisha Sasa yanasonga Nina familia yangu najitahid kuilea kwa upendo ili nisije kosea Kama mm nilivyoona nakosewa
Kwa Sasa mzazi wangu anailaumu simshirikishi katika maamuz ya mambo yangu najitenga Sana na familia sipigi simu mara kwa Mara
Sent using Jamii Forums mobile app
Natambua sana mkuu jinsi wazazi wetu walivyo changamoto ndio maana nimeandika mada hiiMkuu hongera kwa bandiko bora sana,ila tambua kwamba kuna wazazi ni changamoto sana yani. Sitaki kusema sana ila tambua hivyo,mpaka likukute ndipo utajua ni nini namaanisha.
Hivi nama akiwa changamoto si ndio inauma zazid??Mimi mpaka kufikia umri huu sijawahi kushuhudia wala kuona upendo wa dhati kutoka kwa mtu yeyote. Kwanza sijalelewa kabisa na mzazi yeyote yule. Nilibahatika kuishi na mlezi kidogo tu nae nikaona ananiongezea mapicha picha tu katika maisha yangu nikatemana nae.
Ninae mzazi mmoja, wenyewe mnamuita "Mama", ila kuhusu huyu Mama naomba niishie hapa hapa.