Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 48,474
- 125,866
Naunga mkono hoja kwa 100% with vivid exampleKuna wazazi ni miyeyusho Sana niishie hapo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naunga mkono hoja kwa 100% with vivid exampleKuna wazazi ni miyeyusho Sana niishie hapo
Niliwai kumkalisha chini nikamwambia ,baada ya kumwambia ukweli tangu siku hiyo mimi na yeye tumekuwa kama chui na paka anasema kwamba mimi nimemdharau, sijamuheshimu wakat nilikua namwambia ukwel tuu kwamba asifanye vitendo vya hovyo anaitia aibu familia
Wazazi ndo walivyo ukiwashauri wanasema umewadharau, wakitaka ufanye watakacho ukakataa wanasema umewadharauNiliwai kumkalisha chini nikamwambia ,baada ya kumwambia ukweli tangu siku hiyo mimi na yeye tumekuwa kama chui na paka anasema kwamba mimi nimemdharau, sijamuheshimu wakat nilikua namwambia ukwel tuu kwamba asifanye vitendo vya hovyo anaitia aibu familia
Kuna wazazi ni wajinga pia.Wazazi ndo walivyo ukiwashauri wanasema umewadharau, wakitaka ufanye watakacho ukakataa wanasema umewadharau
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kuna wazazi wanazingua sana, ngoja mi nikae kimya tuKuna wazazi ni wajinga pia.
Mtu anataka kutumia uzazi kama kigezo cha kupewa heshima kumbe na yeye ni mjinga tu .
Mzazi anaye jielewa hapangii mtoto maisha yeye akisha timiza wajibu wako wa malezi ana kuacha uka fight sasa kivyako vyako
We ni mimi aisee!Sina shida na mzazi wala ndugu.. ila nina changamoto ya kuwa mvivu kuwapigia simu.
Kuna mama wakubwa wakianza kunisemea kwa mdogo wao ambaye ndio mama sasa, mama anakuja ananisema. Nikijitahidi ni hiyo week niliyosemwa, kisha narudi kuwa vile vile.
Sijui hata natokaje kwenye hicho kisanga.
Umesema kweli kabisa yani.hujakosea kabisa. Home sisi pia ivyo hivyo yani japokua sie pia wachagga.Hapo shida inawezekana ni utamaduni ambao wazazi wako wameutengeneza wa kutowaweka karibu na ndugu zenu ikiwamo kutowashirikisha katika shughuli mbali mbali za kifamilia. Hii itakuja kuwaathiri ninyi watoto wao hamtakuwa karibu hata kidogo.
Unajua mnaweza ona wachagga kama wachawi vile wanakwenda kila mwezi wa kumi na mbili kwa gharama kubwa ila lengo ni kuweka ukaribu wa watoto watambuane na ndugu zao, wahimize upendo kati yao, kujaliana na kuheshimiana na kusaidia popote wanapokuwa mbali.
Pia inasaidia hata kutazamana tabia sio mtu anakuwa na matukio ya kipuuzi puuzi kama wizi, magendo sijui uhalifu gani kila wiki yupo polisi, au dada zetu kuzaa hovyo na wanaume wasioeleweka mwishowe wanashindwa kumudu gharama za maisha wanaanza kusumbua ndugu kwann sasa wasikukimbie na kukuona kero.
Ukaribu ni muhimu sana ila unaharibiwa na wazazi kutokuwa na utamaduni wa kusema fulani haya jiandae weekend hii tunakwenda kwa baba mkubwa au kwa mama mdogo kutembea. Au tunakwenda kuwatembelea akina binamu.
Watoto wakikuzwa na hizi tabia utaona wanakuwa pamoja na wanakuwa karibu sana.
Binadamu wajifunze kutafakari na kujiassess kama kweli wanaweza kuwa wazazi. Kazi kuhamasishana kuzaa wakati uwezo wa kuwa wazazi bora hamna!
Always napenda kukusoma, umeiweka vizuri zaidi mamdogo.Mamdo hayo ndiyo exactly yalikuwa mawazo yangu wakati nasoma hivi visa vya humu. Huwa tunahimizana kweli kuzaa watoto; tunaamini tunakuwa "fulfilled" tukishakuwa na watoto na Ile "mtoto raha jamani". Mtu akisema hataki kuzaa mtoto tunamshangaa na kumuona hamnazo; lakini kumbe that's the most "selfless" decision. Je hawa watoto wanaona maisha yao yapo fulfilled kwa sababu ya sisi wazazi wao au ndiyo tunaishia
kuwa -traumatize tu? Kulea ni kujitoa sadaka kwelikweli otherwise utajikuta unazalisha kizazi chenye majeraha na uchungu mwingi
Ukiumizwa na mtu kama mzazi au dada, kaka, shangazi, mamdogo, mamkubwa, mjomba, binadamu etc watu ambao walitakiwa kukulinda na kukupa faraja huwa inakuja na traumatizing effect maana hawa ni watu wapo katika life yako na ni sehemu ya familia yako.Always napenda kukusoma, umeiweka vizuri zaidi mamdogo.
Mi nilisoma michango nikawa very worried, nikawa sina la ziada zaidi ya kuwaombea wapone. Unajua kuumizwa duniani ni kawaida, ila kuumizwa na watu wako ni waliokuleta duniani...... inaogopesha sana!
Btw, you are missed maa.
Heee .. niko hapa namwangalia mwanangu naomba Mungu aniepushie hayo yote nisije kukwaza wananguKuna makosa mengine mtu hawezi kumsamehe mzazi mfano mzuri ni rafiki ndugu yangu mmoja ambaye baba yake ni mganga wa Jadi huko Shinyanga, huyu mzee alikuwa na wivu wa wazi kwa mtoto wake na mara zote alipinga jamaa kwenda shuleni na hata tupo advance level mzee wake alikuwa hampi sapport yoyote mpaka tuna maliza tunaingia chuoni mzee hana mawasiliano na jamaa wala hatumi pesa.
Sisi ndiyo tunamsaidia hapa na pale jamaa alipomaliza chuo na kupata kazi mzee akaanza maneno kuwa jamaa hasaidii familia kwanza kamtelekeza baba yake kisa amesoma anadharau. Mimi nikamshauri omba msamaha kwani mzazi hakosei ( hizi ni fikra zangu wakati huo saivi nimebadilika).
Kikawekwa kikao jamaa akaomba msamaha mambo mengine yanaendelea. Alivyotaka kuoa ikawa shida mzee hamtaki mwanamke wa jamaa ila tuli force tukamaliza vizuri.
Baada ya ndoa mzee akaleta maneno kuwa mwali akae pale nyumbani ili wachunguze kumbe yule mzee ana nia mbaya na mke wa jamaa. Kwa kutumia dawa zake za kiganga alifarakanisha uhusiano kati ya jamaa (mtoto wake) na mkewe.
Baadaye ikaja kugundulika huyu mzee anamahusiano na mke wa mtoto wake baada ya mke kushika mimba jamaa akaikataa. Sasa wewe hapo unaweza kusamehe uchawi wa hivo? Mimi sio mnafki hapa nilimshauri mwamba akate mawasiliano.
Mfano Mimi sijawahi kuungwa mkono kitu na baba yangu wala mama yangu. Ila waliwapenda sana mpaka sasa wanawapenda dada na kaka yangu na wadogo zangu ila mimi nikawa kama black sheep sihirikishwi kwa chochote lakini sasa hivi nishajua ile familia ni karmic relationship. Hakuna picha hata moja nimepiga nipo na wazazi wangu au nimepiga na baba au mama hakuna wala hawajawahi kuniweka status.
Ila sina ubaya nao japo siongei nao kila mtu na maisha yake na sasa nina familia nimeoa lakini sikuwa shirikisha kitu wala sikutaka mchango wao. Na wala hawana taarifa za life yangu kuwa nina watoto lakini hawajawahi kuwaona.
Huu ni mwaka wa saba sijawahi kukanyaga nyumbani kwetu lakini sio kama kwa ubaya cz nina amani kila mtu sijamkosea kitu. Kama shida walianza wao na uhusiano ni kama daraja kama hukunipenda na kuweka uhusiano mzuri na mimi utotoni usidhani ukubwani nita kupa time wala nafasi Never.
Umeongea safi sana Ila sio wazazi tu hata ndugu kuna ndugu ni nongwa asikwambie mtu, sasa mama hapo yaweza ikawa jamaa akimwambia na yeye anaenda kueleza kwa ndugu mwingine sasa huyo ndugu ndio hataki jamaa atoboe kwa hio anampiga pin, jamaa ilibidi amuulize mama info zake anavujisha kwa nani mwingine?Wapo wazazi ambo Ni barakankwa watoto wao, lakn pia wapo wengine ambao wanajihusisha na nguvu za Giza Ni balaaaa kwa familia. Mungu atupe mwisho mwema...
Huo sio mfumo dume. Mfumo dume ni kitu cha tofauti sana ukilinganisha na hicho umesema hapo. Hapo umeongelea shida ya mtu binafsi.Niwaambieni tu ukweli ndugu zangu.
Kinachowacost wazazi wengi ambao hata humu mmo na nawashangaa mnachangia mada utasema familia zenu mnaziendesha sawa. Kinawacost MFUME DUME!!!!
Mna ujinga mwingi sana kichwani. Huwa mnaamini wewe kama baba huwezi kukosea, yaani we uwe kilaza darasani miaka yote uje upelekeshe familia nzima uzeeni kweli? Kubali kushauriwa kubali kukosolewa. Kubali kusaidiwa na watoto au mkeo.
Huwa nasoma sana comment zenu mna mawazo ya kiduanzi sana na ndo matokeo yake watoto wenu nao watakuja kuandika nyuzi kama hizi mbeleni. Jitu linainua sharubu linachangia mada unajiuliza huyu huwa anamzalisha mkewe kabisa na anajiita Baba?
Badilikeni. Watoto wanatakiwa kulelewa kwa kueleweshwa, sio ubabe. Na unayomfanyia mzazi mwenzako nayo yanawaathiri. Unadhani kama unamnyanyasa mkeo, mtoto wako atakupenda? Acheni ujinga badilikeni lasivyo watoto wataendelea kuwachukia milele nawatawatelekeza hivyo hivyo
Ukitaka nichambue yote nnayotaka kusema ntamaliza kitabu cha page 800. Kwanza nimeongelea kitu ambacho nna experience nacho.Huo sio mfumo dume. Mfumo dume ni kitu cha tofauti sana ukilinganisha na hicho umesema hapo. Hapo umeongelea shida ya mtu binafsi.
So na hawa wamama wanaobakia kulea watoto wao wa kike hovyo wanakuwa na tabia za hovyo mfano akina kajala, akina Monalisa, akina shilole tuite mfumo jike?
Nadhani unatakiwa kufahamu askari anapokuwa mhalifu haifai kusema jeshi la polisi linatengeneza wahalifu wanaovaa uniform za askari ila tunasema askari polisi amekwenda kinyume na utaratibu wa kazi yake na matakwa ya weledi wake.
Sasa inapotokea Mwanaume anashida kwenye mfumo wake wa kuendesha na kuongoza familia yake hatusemi mfumo dume, bali tunamsema huyo muhusika pekee yake kama mtu baki na utaratibu wake.
Mara nyingi mwanaume akiendesha familia vema mnaanza kusema nyuma ya mwanaume mwenye mafanikio kuna mwanamke (kupenda sifa nzuri na kukwepa lawama) ila pale anapokuwa amekwenda vibaya basi mnasema mfumo dume ni shida. Mfumo dume haukuwahi na hautakuja kuwa shida.