Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,812
- 107,628
Be warned, This post is strictly for God's Believers. If you'll find it useless, you're strongly advised not to provoke or outrage targeted Audiences.
Natumaini nyote mko salama, and so do I.
Tatizo la wa toto kutoku[patina na wazazi lipo sana, haijalishi ni mzazi wa kiume au wa kike wengi wetu humu inawezekani mzazi mojawapo kati ya baba na maama hatupatani nae. Achilia mbali mawasilianao kua hafifu bali unakuta mtoto Fulani na mzazi Fulani katika familia hawapatani kabisa, kutokana na nature ya maisha mara nyingi mzazi asiyekua na mahusiano mazuri na watoto au mtoto hua ni baba.
Lakini pia kwa watoto wa kike mara nyingi hua mzazi wao wa kike ndio hua hawapatani nae, lakini kwa sie wakiume ni aghalabu kusikia hatupatani na mama zetu. Ila rate ya baba kutopatana na watoto/mtoto wake ni kubwa Zaidi kuliko ya mama.
Kuna baadhi ya sababu zisizo rasmi zinazoweza kumfanya Baba asiwe na mahusiano mazuri na mwanae:- 1. Baba kutosimama kwenye misingi ya ubaba katika familia na kujikita katika uzinzi,uhuni, ugomvi,ubabe na ukorofi usio na msingi,kutekeleza familia nk. 2: baba kusahau kwamba wanawe wameshakua watu wazima hivyo wanaweza kujiamlia mambo yao katika maisha pia kuamua mustakabali wa familia yao, hivyo baba anakua anataka awachukulie kama watoto tu wasioweza kuamua chochote katika familia yake na hawana uwezo wa kumshauri,kumpinga,kumkosoa na kumuelekeza juu ya jambo Fulani katika famiia.
Baadhi ya sababu hizi zimewafanya wazazi wengi wa kiume kutokua na mawasiliano mazuri na watoto zao, unakuta mtoto anakaa miaka hana mawasiliano kabisa na baba. Kutokana na tabia au makossa anayoyafanya mzai yanaweza kumfanya mtoto asimpende wala kumuheshimu baba yake tena, pengine mtoto anaweza declare kabisa kwamba yeye hana Baba kwa ajili ya madhila anayofanya baba yake.
Inawezekana kutokana na tabia alizonazo baba yako amepoteza misingi ya ubaba hivyo Hupatani nae, labda amekua mlevi sana hadi anachukua vitu ndani ili akalewe akishalewa basi anajikojolea kabisa na kuongea matusi…tabia hiyo imekufanya umchukie,kumdharau na ukate mawasiliano nae. Nipende kukuambia kwamba unakosea sana..tena sana.
Katika Amari za Mungu kumi anasema kwamba Torati 5:16 “Waheshimu baba na mama yako kama BWANA Mungu wako alivyokuamuru,siku zako zipate kuzidi nawe upate kufanikiwa” katika amri zote alizotoa Mungu ukizivunja utakua na la kujibu siku ya hukumu lakini ukivunja amri ya kutowahehimu wazazi hukumu yake utaipata hapa hapa duniani. Kasema kwamba ukiwaheshimu wazazi basi utaishi miaka mingi yenye heri katika dunia lakini kama hutawaheshimu utapata taabu na karaha hapa duniani.
Inawezekana matokeo usiyaone sasa ila ukaja kuadhibiwa kupitia watoto wako, watoto wako wakaja kukusumbua na kukudharau hadi ukajutia kwanini uliwazaa kumbe ni kwakua ulishindwa kuwaheshima wazazi.
Haijalishi baba yako ana tabia gani na mabaya kiasi gani hata kama ni mlevi aliyepindukia hadi anajikojolea mbele yenu na kuwatukana au kumtukana mama yako matusi mbele yenu. Mafundisho yaanasema mkubwa amuheshimu mdogo na mdogo amuheshimu mkubwa , lakini pia yule mkubwa anaweza kumbariki yule aliye mdogo.
So kama mkubwa anaweza kumbariki mdogo hivyo hivyo pia si anaweza kumlaani?? haijalishi baba yako yupo katika hali gani, hata kama kashapoteza ile nafasi ya ubaba katika familia kwa ulevi wake, ukorofi, matusi, umalaya nk…tambua Kamba baba yako huyo bado kashikilia mlango wa Baraka mashani mwako hivyo anaweza kukufungulia Baraka au kukufungia maana yeye ni mzazi wako ulitoka maungoni mwake.
Inawezekana ni mtu mwema uliyeshika dini lakini labda siku moja baba yako kwakuambia kwamba inatakiwa mfanye tambiko la familia, au muende mkanywe au umpe pesa akanyw. Kwakua wewe ni mtu wa ibada hujihusishi na mambo hayo basi ulighafilika na kumjibu labda kwa tone ya hasira kuonyeshwa kutokupendezwa na jambo hilo, elewa hapo umetenda kosa kubwa.
Mungu anasema Zaburi 138:6 “Ingawa bwana yupo juu lakini humuona mnyenyekevu na kumjua mwenye kiburi kutokea mbali” Mithali 3;34 “Hakika bwana huwadharau wennye kiburi bali huwapa wanyenyekevu neema” Kama tulivyoona hapo kwenye maandiko unyenyekevu ndio nguzo kuu kuna sehemu Mungu anasema kwamba yeye hakai nyumbani kwa mwenye kiburi bali kwa mtu mwenye unyenyekevu.
Hivyo basi wewe mtu wa Mungu baba yako anapokuambia maneno mbalimbali yasiyofaa mjbu kwa uyenyekevu kwamba baba haapana jambo hili haliwezekani kwa sababu Fulani lakini ukipandisha sauti kwa mzazi wako basi Mungu atajitenga nawe hata kama wewe ndio ulikua kwenye haki maana yeye kamwe hakai kwa mtu mwenye majivuno na kiburi.
Baba yako kama kakukosea usimchukie na kumdharau kwani yeye ndio mzazi wako, unachotakiwa umuombnea neema ana Baraka aweze kurejea katika hali yake ya kawaida ili aweze kusimama katika ubaba. Ila pindi unapomuhukumu kwamba baba hafai, baba simtaki tena kutokan na tabia zake basi Mungu atajitnga nawe maana unakua umejivisha majivuni na kiburi japokua haki inakua yako ila pindi unapofanya hivyo basi utaoata laana kwani hukumu ni ya mungu sisi tunatakiwa tuombeane rehema na neema.
Nawausia ninyi na kuihusia nafsi yangu kwamba tujitahidi kurejesha mahusiano na mawasialiano mazuri kwa wazizi wetu japokua inawezekana wametenda mambo mabaya, lakini bado hao ni wazazi wetu wanauwezo wa kutulaani na kutubariki maana wao wameshikilia Baraka zetu. Najua ni ngumu sana kwa roho zetu hizi za kibinaadam basi tuombe rehema za kutuwezesha kufanya hivyo.
Kuna wakati kweli mzazi wako anakutenda kitu hadi unajutia kwanini ulizaliwa na baba wa namna hiyo, lakini ndio ishakua kwani hakuna mtu aliyepata privilege ya kuchagua azaliwe wapi na kwa nani. Wazazi pia acheni kufanya maisha ya watoto wenu hasa ya kiroho yawe magumu kutokana na matendo yenu. Mambo mengine hua mnafanya kwa makusudi kabisa ili kuwakomoa watoto wenu eti kwakua nyie ndio mmeshika mpini watoto wapo kwenye makali. Sio vyema kabisa, mnatuumiza na kutuweka katika wakatoi mgumu.
Inspired from true Events.
Da’Vinci